Hekaheka Uzeeni

(iv). Uchaguzi pasi na uchaguzi


“…Sasa amua moja, waoe wote ili ijulikane moja uepukane na dhambi pia kuwanusuru hao mabinti wa watu ama ukate mawasiliano nao kabisa…”

Hiyo ilikuwa ni kauli ya Hamida baada ya kupata hisia kuwa nimetoka na mabinti wale wa Rwanda na Congo.
===

Siku ile tulivyotoka airport na kufika nyumbani muda ulikuwa umeenda sana hivyo baada ya kupata chakula chepesi cha usiku Hamida aliwaelekeza wale mabinti kuwa watalala pamoja. Moyoni wasiwasi ulinijaa tele maana sikujuwa hao mabinti watazungumza nini humo chumbani.

Kulivyokucha baada ya kupata kifungua kinywa, tulifanya kama kikao fulani hivi cha utambulisho ili wote tuwe ukurasa mmoja, na kwa kuwa mimi ndiye nilikuwa nawajuwa wote vizuri ilibidi nichukue jukumu hilo la kufanya utambulisho rasmi ili angalau Janeth na kaka yake wamfahamu Bosio. Kikao kilihusisha sisi watu watano tu na nilianza kuwatambulisha…

“Sweet heart, huyu hapa ni Bosio, anatokea Congo DR na tulifahamiana mjini Goma lakini tukapotezana hadi tulivyokutana bila kutarajia mpaka wa Rwanda na Uganda wote tukitaka kuvuka kuja Tanzania kutokea Rwanda kupitia Uganda….”

Nikavuta pumzi ndefu.

Utambulisho huo wala haukuwa mgeni kwa Wife, bali ni ile hali ya kufanya wote tuwe ukurasa mmoja. Hamida alikuwa ananiangalia kwa makini kama kawaida yake. Nikaendelea…

“…Na yule pale anaitwa Janeth, yeye tulifahamiana Kigali (hapa niliruka maelezo), na familia yake ndio ilinifadhili kipindi kile cha curfew na lockdown nchini Rwanda na yule pale pembeni yake ni mdogo wake…”

Nikavuta pumzi nyingine ndefu.

Utambulisha huu wa Janeth pia haukuwa mgeni kwa wife maana anaujuwa A-Z. Nikaendelea…

“…Janeth, Kulwa na Bosio, yule pale ni mke wangu kama ambavyo mnavyofahamu, karibuni sana Tanzania, mjisikie mpo nyumbani.

Baada ya utambulisho huo rasmi kwa muda huo hapakuwa na ziada ya mazungumzo, walipeana mikono na kila mmoja (Janeth, Kulwa na Bosio) wakisema wamefurahi kufahamiana na sisi tukajumuika katika kupena mikono kama ilivyo kawaida ya waafrika.
===

Ilibidi niwashikilie Janeth na kaka yake kwa siku zingine mbili ili tuweze kuwa pamoja ili tutembezane jijini na binafsi kutaka kujiridhisha hawa wawili wameongea nini usiku ule. Mzigo wa Janeth siku ile ya pili tayari ulikuwa umeshatolewa kule Majerwaa na kaka yake Dotto hivyo hapakuwa na haraka kihivyo ya Janeth na Kulwa kuondoka (kwa mujibu wangu)

Taratibu za kuandaa kuupokea mzigo wa Bosio tulizifanya kwa pamoja mimi Janeth na wale mawakala wake wa awali (waliomba msamaha kwa Bosio na kuomba kupewa kazi zingine zikitokea), Janeth akapata somo kiaina la kuagiza mizigo mizuri kutoka viwandani na uataratibu wa bandarini kwa ujumla.
===

Katika kulitalii jiji, nilitengeneza mazingira ambayo mimi nikapata nafasi ya kutembea na Janeth peke yetu lakini tukiwa na wife, Bosio pamoja na Kulwa ambao nao walikuwa wakitembea kama kundi huku wakizungumza kule ufukweni Kigamboni.

Nikamdodosa Janeth kuhusu usiku ule walipo lala na Bosio walizungumza nini. Akaniambia kuwa alimuuliza amenifahamia wapi mimi na Bosio asijue hili wala lile akafunguka na kumueleza kuanzia mwanzo tulivyokutana hadi siku hiyo (ingawaje sikumsikia ama kuhisi Janeth kuwa ameelezwa kuhusu ‘kulia’ kwa Bosio siku ile Sleep inn) hivyo kiasi roho ikatulia lakini sikuishia hapo nikatafuta ‘moment’ nyingine ya kuwa na Kulwa kuongea ongea huku tukitembea ufukweni, tuliongea ya kawaida tu hususani ya kibiashara na kumsisitizia ni muhimu kujituma na kufanya biashara kwa faida yake na familia yake atakayo itengeneza siku za usoni.

Pia kwa mtindo huo huo nikapata wasaa wa kuzunguka na Bosio ili naye nimdodose kutaka kujuwa aliyoambiwa na Janeth siku ile walipo lala pamoja. Bosio alifunguka kuwa alimuambia jinsi tulivyokutana mara ya kwanza hadi sasa…

“…Ina maana ulimwambia kuwa pia tulibukana kule Kariakoo?...” nilimuuliza

“iiiiiiii hapana Papaa, mie niko mutu mzima, nilimspikee tu vile uko mutu muzuri na vile umenisaidia kutosha mizigo yangu bandarini, ukaniokoa na wale walitaka kuniflapee faranga zangu…”

“…waliniita (walimpigia) kwenye telephone yangu juu numeroo zangu wanazo, mie za kwao nilizifutaga, wakaniomba niwahurumie (kuwasamehe) ndo vile nikasema nitawapatia duu-contenaa (kontena mbili)watoshe nikiagiza, na sasa wako wanapiganisha kutosha hizo kontena …”

Nikaridhika kwa maelezo yake kisha nikapata wasaa wa kutembea na Hamida ili naye nimsikie hisia zake maana kwa uangaliaji aliokuwa ananiangalia nilihisi kuna kitu anacho moyoni. Pia kwa kuwa nilikuwa na Hamida, wakina Bosio na Janeth nao wakapata wasaa wa kuwa pamoja na Kulwa yeye akajichanganya kwenye kundi fulani hivi palikuwa na kama mashindano yasiyo rasmi ya free style rapin’.

Nikatumia nafasi ile kumdodosa Hamida naye hakuacha kunichana.

“…Wewe unazeeka vibaya, umevikula vitoto vya watu halafu vyote umevialika nyumbani…, “…Sasa amua moja, waoe wote ili ijulikane moja uepukane na dhambi pia kuwanusuru hao mabinti wa watu ama ukate mawasiliano nao kabisa…”

Kijasho chembamba cha kwapa kilinitoka, hadi nikakihisi harufu yake japo upepo ulikuwa ukipuliza kiasi cha kuzuia kutokwa na jasho.

“…Ni Janeth tu sweet heart, na sababu nilishakueleza na adhabu ulishanipatia lakini na hiyo nyingine nitaitekeleza siku si nyingi, lakini huyu Bosio wala sijatoka naye! Hamida akanikatisha…

“..Mbona anakuangalia kwa jicho la mahaba, na hata siku ile kule Ubungo nilivyowapokea pia nilimuona akikuangalia jicho ambalo si la kawaida…”

Nikacheka kiasi (kinafiki huku roho ikinidunda….)

“Hapana mama Junior, yule macho yake ndiyo yalivyo, hata jina lake tafsiri yake ni macho mazuri, ndio maana wazazi wake walimpatia jina la Bosio kwa maana ya ‘macho mazuri’

Nilijizungumzisha pale na tukahitimisha kuwa atayaangalia vizuri macho yake na pia nisijisahaulishe suala ya kumpelea shopping Dubai. (katikati hapo alishanitamkia kuwa nimpeleke huko Dubai kwa ajili ya shopping kama moja ya sharti ya kusamehewa kujifunza kilimo cha umwagiliaji kwa Janeth)

Tulifurahia adhuhuri ile hadi jioni yake tulipoamua kurudi hadi maeneo ya Mnazi mmoja kwenye siku ya Mwafrika, Hotel Peackok (Afro Fusion Night) ambapo huwa kuna live band na burudani kadha wa kadha.

Tulifurahia usiku ule lakini moyoni nikiwa na mawazo ya ‘idea’ ya Hamida hahahahaha eti niwaoe wote Janeth na Bosio…

ITAENDELEA….



Je wewe unadhani ni idea nzuri ya kutamka kuwaoa Janeth na Bosio?! Au ndio nitazidisha hekaheka uzeeni?!
 

Attachments

  • Rwa20.jpeg
    188.5 KB · Views: 55
  • PH3.jpg
    70.2 KB · Views: 51
  • PH2.jpg
    88.5 KB · Views: 50
  • PH1.jpg
    33.8 KB · Views: 49
  • KG1.jpg
    11.6 KB · Views: 57
  • RDC19.jpg
    117.6 KB · Views: 60
mzee hapo kwenye mke umepata aisee,
mwanamke mwenye upendo kwa wageni ni furaha na baraka tele maishani.
Hakika,
Sijawahi kujutia chaguo hili.

Naona amerithi kutoka kwenye familia yao, maana wageni ni karibu kila siku...

Wa kuja na kukaa siku kadhaa

Wa kuja na kuondoka ndani ya siku chache...


Wageni wale wapita njia, yani nyumba ni full wageni muda wote.
 
(v) The Decision

Siku ya tatu jioni Janeth na kaka yake tuliwasindikiza airport na wakaruka kuelekea Kigali ambako walifika salama na Janeth alinipigia video call akiwa na familia yake kama kawaida yao kushukuru kwa yote.

Bosio aliendelea kubaki nyumbani hadi kontena zake zilipopata release na kwa utaratibu uleule zilisafirishwa kuelekea Bunjumbura kisha Bukavu.

Bosio alikuwa mtu mzima kiasi kulinganisha na Janeth, Bosio mama wa watoto wawili na mwenye kubeba umbo linaloakisi mama wa kiafrika alijenga ukaribu sana na Hamida hadi nikawa nina wasiwasi huenda wana agenda ya siri.

Labda kwa kuwa Bosio alikuwa anaongea Kiswahili ambacho angalau kilikuwa kinaeleweka kuliko Janeth ambaye muda mwingi alikuwa akiongea kiingereza ambacho nacho hakikuwa kimenyooka sana. Bosio alimletea Hamida zawadi za vitenge viwili vya pande tatu kila kimoja…

“…hii vikwembe viko byee ni lezepouz di ministr kule kwetu…” alisema Bosio akimaanisha kuwa hivi vitenge ni vizuri sana ni vya hadhi ya kuvaa wake wa mawaziri kule DRC.

Walikuwa wakipika na kupakua pale nyumbani na muda mwingi ambao haukuwa wa kwenda bandarini wao waliutumia pamoja. Hakika walitokea kuelewana sana.

Kontena zake zilipotoka na baada ya kusikia zimeshafika Isaka, Bosio alianza mipango ya usafiri ambapo safari hii alipanda ndege hadi Bunjumbura.
===

Hamida ambaye sasa amevuka nusu karne ya kuishi akiikimbilia miaka 60 bado alikuwa na uzuri wake na kila sifa njema. Nilijiona nimemkosea sana kwa kumsaliti uzeeni kwa vitoto vile ingawaje hadi muda huo aliamini nimetoka na Janeth pekee (not sure lakini). Hamida alikuwa ameenea kila idara kwenye mambo ya ndani ya nyumba…

“…Sikustahiki kumkosea kiasi hiki…” nilijikuta nasema na kuonesha kujijutia nafsi yangu.

Safari ya Dubai ikazaa safari ya Muscat kwa dada yake ambaye sasa ni mjane, tulitumia fursa hiyo kusalimia ndugu na jamaa lakini wakati tuko Dubai tulienda shopping mall fulani ili afanye shopping anayotaka.

Ila wanawake bhana! Safari yote ile eti alinunua vito vichache na mikufu ya dhahabu mitatu ya miundo tofauti na simu moja Samsung iliyokuwa toleo jipya wakti ule. Eti akawa ameridhika.!

Lakini pia tulitumia ‘vacation’ ile kutafakali mambo mengine pamoja na wazo lake la mimi kuwaoa Janeth na Bosio ili kuwapa nusra tusiendelee kutenda dhambi.

Janeth ndio kwanza alikuwa anaitafuta miaka thelathini na Bosio tayari alikuwa yupo juu ya thelthini akiitafuta miaka arobaini. Hata ile threesome aliyokuwa amependkeza mdao mmoja hapo nyuma ilikuwa ni ‘irrelevant’ kabisa. Hamida kuvua nguo mbele ya vile vitoto ilikuwa kama ni kuwalaani, maana wana utofauti mkubwa wa umri. Lakini mimi kuvua nguo mbele ya Hamida na Janeth na Bosio wakiwepo ni jambo lisio ingia akilini kabisa. Zaidi ya yote Hamida ni mke na hao wengine sio ‘wake’. Sijui mganga year yeye alifanya?! Its crazy fantacy!

Hapa kuna siri kubwa ipo. Hebu chukuwa mazingira kama haya yafuatayo, wewe una mwenza wako na rafiki yake. Lets say wewe ni mwanaume una girl friend wako na girl friend wako ana rafiki yake wa kike pia na wote mnafahamiana. Wewe unaweza kubadilisha nguo mbele ya girl friend wako. Na Girl friend wako anaweza kubadilisha nguo mbele ya rafiki yake huyo wa kike. Lakini ajabu ni wote mkiwa chumba kimoja huwezi kubadilisha nguo mbele yao au girl friend wako kubadilisha nguo mbele yenu. Vinginevyo kuwe na uchizi fulani upo ndani mwenu.
===

“…Haiwezekani mimi kwa umri huu kujitia hekaheka za kuoa mabinti wale wadogo…” nilimwambia Hamida tukiwa hotelini chumbani tumetulia huko Dubai.

“Hata kama gari bovu ndio huvujwa na gari zima lakini sio kwa namna hii, labda kama ungelikuwa wewe haupo lakini napo ningetafuta mzee mwenzangu ili tusogeze siku pamoja…”

“…Kwa miaka miwili mitatu ya awali mambo yanaweza kuwa mazuri, lakini kwa umri huu nitakuwa nimewadhulumu mengi ambayo wanatakiwa wayapate ambapo hawatayapata kutoka kwangu ilhali mimi niliyapata yote katika ujana wangu, hii si itakuwa dhulma hii….” Nilimuuliza Hamida

“Leo tunaweza kumwagilia vizuri mashamba, huenda na mazao yakapatikana, lakini siku si nyingi uwezo wa kumwagilia na kuridhisha utakuwa unapungua kila siku, je siwatafutii dhambi watoto wa watu…? Niliendelea kuhoji.

“Bosio alishaolewa na kufiwa na mumewe, huoni kuwa asipopata kile anachotarajia kutoka kwa mume nitamkumbushia machungu aliyonayo?

Mimi naona njia bora ni kuwatafutia waume bora watakaowaoa na sisi tushiriki kwenye harusi yao kuliko kukata mawasiliano nao kabisa. Au unaonaje? Nilimuuliza Hamida ambaye tayari usingizi ulikuwa unamchukuwa. Akanijibu kuwa atanijibu asubuhi.
===

Tulitumia siku sita Mashariki ya kati na siku mbili za safari kufanya siku nane tuwe nje ya Dar. Tukiwa Dubai tuliendelea kufurahia kilimo cha umwagiliaji jangwani ukijumlisha na kile kilimo cha sesa basi ikawa ni burudani tu ingawaje shamba lilikuwa likimwagiliwa mara moja tu jua likizama lakini kwa siku zote huko na kutofanya mwili uchoke kwa kazi ngumu ya utafutaji na umwagiliaji na kufanya tuzidi kupata afya ya mwili na akili. Ukweli ni kwamba kati ya miaka 45 hadi 65 ndio wakulima hufurahia zaidi wawapo kilimoni kuliko inavyodhaniwa na vijana wengi, muhimu tu afya iwe nzuri ya kimwili na kiakili.

Tulitua Dar tukiwa tume ‘refresh’ akili zetu na kwamba tayari Hamida aliridhia nisikate mawasiliano na akina Janeth na Bosio lakini nifanye huo utaratibu wa wao kupata wenza ili nafsi zao zitulie na kufanya yale yanayo mpendeza Muumba.

Bosio ni mfuasi wa Roman Catholic na Janeth ni mfuasi wa Adventista wa kisabato. Hivyo kama wazo la kuwaoa wote lingepita maana yake kulikuwa na hekaheka ya kuwabadilisha dini hao wote waje kwenye uislamu, maana kwa umri huu mimi na Hamida isingekuwa rahisi kubadili dini au vinginevyo nimwache Hamida na kuingia ama uromani au usabato na mmoja wapo kati ya Jane au Bosio ahame dhehebu mchakato ambao pia sio rahisi. Hivyo wazo la kuwatafutia wachumba lilikuwa muafaka na ikabaki hivyo.

Wakati yote haya yanafanyika si Janeth wa Bosio aliyekuwa akijuwa lolote ingawaje walijulishwa kuhusu safari yetu Dubai ‘kwenda kusalimia familia’.

Hekaheka sasa ikawa ni namna gani nafanikisha hili zoezi la kuhakikisha hawa mabinti wanapata waume. Niliamua kwanza nianze na Janeth ambaye bado hajapata kuolewa, nikaongea na baba yake Janeth na kumuuliza itakuwa vipi (in Hon. HM Mwinjuma voice) kama Janeth akiolewa na Mtanzania?!

Afande yule wala hakuwa na makuu, alijibu kuwa ni njia nzuri ya kujenga umoja baina ya Tanzania na Rwanda, lakini pia kuvunja ukabila kama bado umo kwenye damu ya Janeth na kujenga nasaba bora ya mchanganyiko wa udongo kutoka mataifa tofauti.

Moyoni ikanijia sera za vijana wa sasa wa kitanzania wanavyohimizana kukataa ndoa, yani hawajui tu utamu uliopo kwenye ndoa, basi tuwaache hadi yakini itakapo wadhihirikia. Nikaanza kujenga ukaribu na watumishi wa makanisa ya kisabato …

Kwa Bosio haikuwa tabu kwa kuwa tayari alishaishi na mume na pia aliwahi kuwa na boy friend mwingine waliyeishi nyumba moja, kazi itakuwa ni ndogo ya kumshawishi afungue moyo ili aweke nafasi ya upendo kwa mtu mwingine.

Kwangu binafsi ilibidi nichukuwe nafasi yangu halisi kwao “kama Baba” ili nifunge milango ya mapenzi na kuruhusu mioyo yao kuanza kufikilia uhalisia na kutenga nafasi kwa ajili ya waume watarajiwa.
===

Miezi ikakatika na siku ikafika Janeth akaja Dar kaka yake Dotto kwa ajili ya kununua bidhaa. Safari hii nikamuomba Janeth abaki Tz kwa muda mrefu zaidi lakini Dotto ndiye arudi na mzigo Kigali maana nilikuwa na ‘mambo ya kumuonesha’.

Jumamosi ikafika na nikampeleka kwenye moja ya kanisa kubwa la 7th Day Adventist Dar (kapuni kwa sasa) na kumwambia awe anasali humo. Mimi na Hamida tulikuwa tuna m-‘drive’ hadi hapo na baada ya misa zao tunampitia na kuendelea na kujamiiana (socialization)

Baada ya tafsiri maneno ya Janeth…

“…Nilivyoingia tu mule kanisani, kila mtu alikuwa ananitazama na kwakuwa niliona baadhi siti za mbele ziko wazi basi nilitembea huku macho yote kanisani yakinilenga mimi hadi nilipo keti…”

“…Baada ya misa wakati ule wa kusalimiana, watu wengi walikuja kunisalimia akiwemo mchungaji mkuu na kuniambia kuwa wiki ijayo nisikose maana atanitambulisha rasmi kanisani…”

“…Wanaume wa Kitanzania wakarimu sana, niliona wengi walikuja kunisalimia kwa heshima na kila mtu akitaka kunishika mkono…”

Janeth alituelezea hali ilivyokuwa kanisani kwake pale na kuonesha kufurahia ukarimu alio oneshwa, kwa upande wetu sisi (mimi na Hamida) moyoni tukawa tunafurahi maana tunajuwa fika huko moyo wake utafunguka kwa mwanume atakaye mpenda.
===

Kwa Bosio mbinu ilikuwa tofauti kwa kuwa alikuwa si mtu wa kusali kanisani, yeye hujifungia tu chumbani na kufanya ibada zake, hivyo niliamua nitumie mbinu ya kutoka naye out tukiwa watatu, yaani mimi, Hamida na yeye ili mzani usiwe ume ‘balansi’ na kufanya kuvutia wawekezaji kuja kubalansi mzani.

Nikakumbuka sana enzi ya Tazara Disco lakini nikaamua ngoja tutumie njia ya hoteli kubwa zenye watu wenye heshima zao na kuwa na tahadhali na vijana (wa mujini) pia.

Kwa kuwa alionesha sana kufurahia siku ile ya usiku wa mwafrika pale peacock, basi ikawa ndio chaguo la kwanza ili kila siku jioni awepo pale akiburudika (kwa malengo maalum kwa upande wetu) ili hatimaye ipatikane sababu ya yeye kuanzisha uhusiano.

“Hamida ameshinda…”

Nilijikuta najisemea baada ya kuona ile hali ya kuwaona Janeth na Bosio kuwa ni wapenzi wangu wa siri ikiondoka na kuanza kuwaona kama watoto wangu.

Bosio akawa maarufu pale peackock kwa kuwa alikuwa kwanza siku zote akija Dar anakuwepo pale jioni hadi usiku mwingi (alikuwa haachi kuja kulala nyumbani) lakini pia ikipigwa miziki ya Kikongo alikuwa ‘anayarudi’ vizuri kiustaarbu huku akiimba kilingala na kufanya awe kivutio kwa washereheshaji .

Hamida akawa na Amani ya moyo nami nikawa naendelea kuimarisha afya yangu ya mwili ili zoezi la kumwagilia lisikome bali ufanisi uongezeke na kufurahia maisha baada ya kustaafu nikiwa na amani furaha na upendo.


ITAENDELEA…
 

Attachments

  • JBS1.jpg
    9.7 KB · Views: 53
  • HBJB59.jpeg
    8.5 KB · Views: 46
  • bgg1.jpg
    10.9 KB · Views: 55
  • KG1.jpg
    30.8 KB · Views: 51
mpwayungu village njoo uone huku
 
Ahahahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…