Hekaheka Uzeeni

Hekaheka Uzeeni

(iv). Uchaguzi pasi na uchaguzi


“…Sasa amua moja, waoe wote ili ijulikane moja uepukane na dhambi pia kuwanusuru hao mabinti wa watu ama ukate mawasiliano nao kabisa…”

Hiyo ilikuwa ni kauli ya Hamida baada ya kupata hisia kuwa nimetoka na mabinti wale wa Rwanda na Congo.
===

Siku ile tulivyotoka airport na kufika nyumbani muda ulikuwa umeenda sana hivyo baada ya kupata chakula chepesi cha usiku Hamida aliwaelekeza wale mabinti kuwa watalala pamoja. Moyoni wasiwasi ulinijaa tele maana sikujuwa hao mabinti watazungumza nini humo chumbani.

Kulivyokucha baada ya kupata kifungua kinywa, tulifanya kama kikao fulani hivi cha utambulisho ili wote tuwe ukurasa mmoja, na kwa kuwa mimi ndiye nilikuwa nawajuwa wote vizuri ilibidi nichukue jukumu hilo la kufanya utambulisho rasmi ili angalau Janeth na kaka yake wamfahamu Bosio. Kikao kilihusisha sisi watu watano tu na nilianza kuwatambulisha…

“Sweet heart, huyu hapa ni Bosio, anatokea Congo DR na tulifahamiana mjini Goma lakini tukapotezana hadi tulivyokutana bila kutarajia mpaka wa Rwanda na Uganda wote tukitaka kuvuka kuja Tanzania kutokea Rwanda kupitia Uganda….”

Nikavuta pumzi ndefu.

Utambulisho huo wala haukuwa mgeni kwa Wife, bali ni ile hali ya kufanya wote tuwe ukurasa mmoja. Hamida alikuwa ananiangalia kwa makini kama kawaida yake. Nikaendelea…

“…Na yule pale anaitwa Janeth, yeye tulifahamiana Kigali (hapa niliruka maelezo), na familia yake ndio ilinifadhili kipindi kile cha curfew na lockdown nchini Rwanda na yule pale pembeni yake ni mdogo wake…”

Nikavuta pumzi nyingine ndefu.

Utambulisha huu wa Janeth pia haukuwa mgeni kwa wife maana anaujuwa A-Z. Nikaendelea…

“…Janeth, Kulwa na Bosio, yule pale ni mke wangu kama ambavyo mnavyofahamu, karibuni sana Tanzania, mjisikie mpo nyumbani.

Baada ya utambulisho huo rasmi kwa muda huo hapakuwa na ziada ya mazungumzo, walipeana mikono na kila mmoja (Janeth, Kulwa na Bosio) wakisema wamefurahi kufahamiana na sisi tukajumuika katika kupena mikono kama ilivyo kawaida ya waafrika.
===

Ilibidi niwashikilie Janeth na kaka yake kwa siku zingine mbili ili tuweze kuwa pamoja ili tutembezane jijini na binafsi kutaka kujiridhisha hawa wawili wameongea nini usiku ule. Mzigo wa Janeth siku ile ya pili tayari ulikuwa umeshatolewa kule Majerwaa na kaka yake Dotto hivyo hapakuwa na haraka kihivyo ya Janeth na Kulwa kuondoka (kwa mujibu wangu)

Taratibu za kuandaa kuupokea mzigo wa Bosio tulizifanya kwa pamoja mimi Janeth na wale mawakala wake wa awali (waliomba msamaha kwa Bosio na kuomba kupewa kazi zingine zikitokea), Janeth akapata somo kiaina la kuagiza mizigo mizuri kutoka viwandani na uataratibu wa bandarini kwa ujumla.
===

Katika kulitalii jiji, nilitengeneza mazingira ambayo mimi nikapata nafasi ya kutembea na Janeth peke yetu lakini tukiwa na wife, Bosio pamoja na Kulwa ambao nao walikuwa wakitembea kama kundi huku wakizungumza kule ufukweni Kigamboni.

Nikamdodosa Janeth kuhusu usiku ule walipo lala na Bosio walizungumza nini. Akaniambia kuwa alimuuliza amenifahamia wapi mimi na Bosio asijue hili wala lile akafunguka na kumueleza kuanzia mwanzo tulivyokutana hadi siku hiyo (ingawaje sikumsikia ama kuhisi Janeth kuwa ameelezwa kuhusu ‘kulia’ kwa Bosio siku ile Sleep inn) hivyo kiasi roho ikatulia lakini sikuishia hapo nikatafuta ‘moment’ nyingine ya kuwa na Kulwa kuongea ongea huku tukitembea ufukweni, tuliongea ya kawaida tu hususani ya kibiashara na kumsisitizia ni muhimu kujituma na kufanya biashara kwa faida yake na familia yake atakayo itengeneza siku za usoni.

Pia kwa mtindo huo huo nikapata wasaa wa kuzunguka na Bosio ili naye nimdodose kutaka kujuwa aliyoambiwa na Janeth siku ile walipo lala pamoja. Bosio alifunguka kuwa alimuambia jinsi tulivyokutana mara ya kwanza hadi sasa…

“…Ina maana ulimwambia kuwa pia tulibukana kule Kariakoo?...” nilimuuliza

“iiiiiiii hapana Papaa, mie niko mutu mzima, nilimspikee tu vile uko mutu muzuri na vile umenisaidia kutosha mizigo yangu bandarini, ukaniokoa na wale walitaka kuniflapee faranga zangu…”

“…waliniita (walimpigia) kwenye telephone yangu juu numeroo zangu wanazo, mie za kwao nilizifutaga, wakaniomba niwahurumie (kuwasamehe) ndo vile nikasema nitawapatia duu-contenaa (kontena mbili)watoshe nikiagiza, na sasa wako wanapiganisha kutosha hizo kontena …”

Nikaridhika kwa maelezo yake kisha nikapata wasaa wa kutembea na Hamida ili naye nimsikie hisia zake maana kwa uangaliaji aliokuwa ananiangalia nilihisi kuna kitu anacho moyoni. Pia kwa kuwa nilikuwa na Hamida, wakina Bosio na Janeth nao wakapata wasaa wa kuwa pamoja na Kulwa yeye akajichanganya kwenye kundi fulani hivi palikuwa na kama mashindano yasiyo rasmi ya free style rapin’.

Nikatumia nafasi ile kumdodosa Hamida naye hakuacha kunichana.

“…Wewe unazeeka vibaya, umevikula vitoto vya watu halafu vyote umevialika nyumbani…, “…Sasa amua moja, waoe wote ili ijulikane moja uepukane na dhambi pia kuwanusuru hao mabinti wa watu ama ukate mawasiliano nao kabisa…”

Kijasho chembamba cha kwapa kilinitoka, hadi nikakihisi harufu yake japo upepo ulikuwa ukipuliza kiasi cha kuzuia kutokwa na jasho.

“…Ni Janeth tu sweet heart, na sababu nilishakueleza na adhabu ulishanipatia lakini na hiyo nyingine nitaitekeleza siku si nyingi, lakini huyu Bosio wala sijatoka naye! Hamida akanikatisha…

“..Mbona anakuangalia kwa jicho la mahaba, na hata siku ile kule Ubungo nilivyowapokea pia nilimuona akikuangalia jicho ambalo si la kawaida…”

Nikacheka kiasi (kinafiki huku roho ikinidunda….)

“Hapana mama Junior, yule macho yake ndiyo yalivyo, hata jina lake tafsiri yake ni macho mazuri, ndio maana wazazi wake walimpatia jina la Bosio kwa maana ya ‘macho mazuri’

Nilijizungumzisha pale na tukahitimisha kuwa atayaangalia vizuri macho yake na pia nisijisahaulishe suala ya kumpelea shopping Dubai. (katikati hapo alishanitamkia kuwa nimpeleke huko Dubai kwa ajili ya shopping kama moja ya sharti ya kusamehewa kujifunza kilimo cha umwagiliaji kwa Janeth)

Tulifurahia adhuhuri ile hadi jioni yake tulipoamua kurudi hadi maeneo ya Mnazi mmoja kwenye siku ya Mwafrika, Hotel Peackok (Afro Fusion Night) ambapo huwa kuna live band na burudani kadha wa kadha.

Tulifurahia usiku ule lakini moyoni nikiwa na mawazo ya ‘idea’ ya Hamida hahahahaha eti niwaoe wote Janeth na Bosio…

ITAENDELEA….



Je wewe unadhani ni idea nzuri ya kutamka kuwaoa Janeth na Bosio?! Au ndio nitazidisha hekaheka uzeeni?!
 

Attachments

  • Rwa20.jpeg
    Rwa20.jpeg
    188.5 KB · Views: 55
  • PH3.jpg
    PH3.jpg
    70.2 KB · Views: 51
  • PH2.jpg
    PH2.jpg
    88.5 KB · Views: 50
  • PH1.jpg
    PH1.jpg
    33.8 KB · Views: 49
  • KG1.jpg
    KG1.jpg
    11.6 KB · Views: 57
  • RDC19.jpg
    RDC19.jpg
    117.6 KB · Views: 60
mzee hapo kwenye mke umepata aisee,
mwanamke mwenye upendo kwa wageni ni furaha na baraka tele maishani.
Hakika,
Sijawahi kujutia chaguo hili.

Naona amerithi kutoka kwenye familia yao, maana wageni ni karibu kila siku...

Wa kuja na kukaa siku kadhaa

Wa kuja na kuondoka ndani ya siku chache...


Wageni wale wapita njia, yani nyumba ni full wageni muda wote.
 
(v) The Decision

Siku ya tatu jioni Janeth na kaka yake tuliwasindikiza airport na wakaruka kuelekea Kigali ambako walifika salama na Janeth alinipigia video call akiwa na familia yake kama kawaida yao kushukuru kwa yote.

Bosio aliendelea kubaki nyumbani hadi kontena zake zilipopata release na kwa utaratibu uleule zilisafirishwa kuelekea Bunjumbura kisha Bukavu.

Bosio alikuwa mtu mzima kiasi kulinganisha na Janeth, Bosio mama wa watoto wawili na mwenye kubeba umbo linaloakisi mama wa kiafrika alijenga ukaribu sana na Hamida hadi nikawa nina wasiwasi huenda wana agenda ya siri.

Labda kwa kuwa Bosio alikuwa anaongea Kiswahili ambacho angalau kilikuwa kinaeleweka kuliko Janeth ambaye muda mwingi alikuwa akiongea kiingereza ambacho nacho hakikuwa kimenyooka sana. Bosio alimletea Hamida zawadi za vitenge viwili vya pande tatu kila kimoja…

“…hii vikwembe viko byee ni lezepouz di ministr kule kwetu…” alisema Bosio akimaanisha kuwa hivi vitenge ni vizuri sana ni vya hadhi ya kuvaa wake wa mawaziri kule DRC.

Walikuwa wakipika na kupakua pale nyumbani na muda mwingi ambao haukuwa wa kwenda bandarini wao waliutumia pamoja. Hakika walitokea kuelewana sana.

Kontena zake zilipotoka na baada ya kusikia zimeshafika Isaka, Bosio alianza mipango ya usafiri ambapo safari hii alipanda ndege hadi Bunjumbura.
===

Hamida ambaye sasa amevuka nusu karne ya kuishi akiikimbilia miaka 60 bado alikuwa na uzuri wake na kila sifa njema. Nilijiona nimemkosea sana kwa kumsaliti uzeeni kwa vitoto vile ingawaje hadi muda huo aliamini nimetoka na Janeth pekee (not sure lakini). Hamida alikuwa ameenea kila idara kwenye mambo ya ndani ya nyumba…

“…Sikustahiki kumkosea kiasi hiki…” nilijikuta nasema na kuonesha kujijutia nafsi yangu.

Safari ya Dubai ikazaa safari ya Muscat kwa dada yake ambaye sasa ni mjane, tulitumia fursa hiyo kusalimia ndugu na jamaa lakini wakati tuko Dubai tulienda shopping mall fulani ili afanye shopping anayotaka.

Ila wanawake bhana! Safari yote ile eti alinunua vito vichache na mikufu ya dhahabu mitatu ya miundo tofauti na simu moja Samsung iliyokuwa toleo jipya wakti ule. Eti akawa ameridhika.!

Lakini pia tulitumia ‘vacation’ ile kutafakali mambo mengine pamoja na wazo lake la mimi kuwaoa Janeth na Bosio ili kuwapa nusra tusiendelee kutenda dhambi.

Janeth ndio kwanza alikuwa anaitafuta miaka thelathini na Bosio tayari alikuwa yupo juu ya thelthini akiitafuta miaka arobaini. Hata ile threesome aliyokuwa amependkeza mdao mmoja hapo nyuma ilikuwa ni ‘irrelevant’ kabisa. Hamida kuvua nguo mbele ya vile vitoto ilikuwa kama ni kuwalaani, maana wana utofauti mkubwa wa umri. Lakini mimi kuvua nguo mbele ya Hamida na Janeth na Bosio wakiwepo ni jambo lisio ingia akilini kabisa. Zaidi ya yote Hamida ni mke na hao wengine sio ‘wake’. Sijui mganga year yeye alifanya?! Its crazy fantacy!

Hapa kuna siri kubwa ipo. Hebu chukuwa mazingira kama haya yafuatayo, wewe una mwenza wako na rafiki yake. Lets say wewe ni mwanaume una girl friend wako na girl friend wako ana rafiki yake wa kike pia na wote mnafahamiana. Wewe unaweza kubadilisha nguo mbele ya girl friend wako. Na Girl friend wako anaweza kubadilisha nguo mbele ya rafiki yake huyo wa kike. Lakini ajabu ni wote mkiwa chumba kimoja huwezi kubadilisha nguo mbele yao au girl friend wako kubadilisha nguo mbele yenu. Vinginevyo kuwe na uchizi fulani upo ndani mwenu.
===

“…Haiwezekani mimi kwa umri huu kujitia hekaheka za kuoa mabinti wale wadogo…” nilimwambia Hamida tukiwa hotelini chumbani tumetulia huko Dubai.

“Hata kama gari bovu ndio huvujwa na gari zima lakini sio kwa namna hii, labda kama ungelikuwa wewe haupo lakini napo ningetafuta mzee mwenzangu ili tusogeze siku pamoja…”

“…Kwa miaka miwili mitatu ya awali mambo yanaweza kuwa mazuri, lakini kwa umri huu nitakuwa nimewadhulumu mengi ambayo wanatakiwa wayapate ambapo hawatayapata kutoka kwangu ilhali mimi niliyapata yote katika ujana wangu, hii si itakuwa dhulma hii….” Nilimuuliza Hamida

“Leo tunaweza kumwagilia vizuri mashamba, huenda na mazao yakapatikana, lakini siku si nyingi uwezo wa kumwagilia na kuridhisha utakuwa unapungua kila siku, je siwatafutii dhambi watoto wa watu…? Niliendelea kuhoji.

“Bosio alishaolewa na kufiwa na mumewe, huoni kuwa asipopata kile anachotarajia kutoka kwa mume nitamkumbushia machungu aliyonayo?

Mimi naona njia bora ni kuwatafutia waume bora watakaowaoa na sisi tushiriki kwenye harusi yao kuliko kukata mawasiliano nao kabisa. Au unaonaje? Nilimuuliza Hamida ambaye tayari usingizi ulikuwa unamchukuwa. Akanijibu kuwa atanijibu asubuhi.
===

Tulitumia siku sita Mashariki ya kati na siku mbili za safari kufanya siku nane tuwe nje ya Dar. Tukiwa Dubai tuliendelea kufurahia kilimo cha umwagiliaji jangwani ukijumlisha na kile kilimo cha sesa basi ikawa ni burudani tu ingawaje shamba lilikuwa likimwagiliwa mara moja tu jua likizama lakini kwa siku zote huko na kutofanya mwili uchoke kwa kazi ngumu ya utafutaji na umwagiliaji na kufanya tuzidi kupata afya ya mwili na akili. Ukweli ni kwamba kati ya miaka 45 hadi 65 ndio wakulima hufurahia zaidi wawapo kilimoni kuliko inavyodhaniwa na vijana wengi, muhimu tu afya iwe nzuri ya kimwili na kiakili.

Tulitua Dar tukiwa tume ‘refresh’ akili zetu na kwamba tayari Hamida aliridhia nisikate mawasiliano na akina Janeth na Bosio lakini nifanye huo utaratibu wa wao kupata wenza ili nafsi zao zitulie na kufanya yale yanayo mpendeza Muumba.

Bosio ni mfuasi wa Roman Catholic na Janeth ni mfuasi wa Adventista wa kisabato. Hivyo kama wazo la kuwaoa wote lingepita maana yake kulikuwa na hekaheka ya kuwabadilisha dini hao wote waje kwenye uislamu, maana kwa umri huu mimi na Hamida isingekuwa rahisi kubadili dini au vinginevyo nimwache Hamida na kuingia ama uromani au usabato na mmoja wapo kati ya Jane au Bosio ahame dhehebu mchakato ambao pia sio rahisi. Hivyo wazo la kuwatafutia wachumba lilikuwa muafaka na ikabaki hivyo.

Wakati yote haya yanafanyika si Janeth wa Bosio aliyekuwa akijuwa lolote ingawaje walijulishwa kuhusu safari yetu Dubai ‘kwenda kusalimia familia’.

Hekaheka sasa ikawa ni namna gani nafanikisha hili zoezi la kuhakikisha hawa mabinti wanapata waume. Niliamua kwanza nianze na Janeth ambaye bado hajapata kuolewa, nikaongea na baba yake Janeth na kumuuliza itakuwa vipi (in Hon. HM Mwinjuma voice) kama Janeth akiolewa na Mtanzania?!

Afande yule wala hakuwa na makuu, alijibu kuwa ni njia nzuri ya kujenga umoja baina ya Tanzania na Rwanda, lakini pia kuvunja ukabila kama bado umo kwenye damu ya Janeth na kujenga nasaba bora ya mchanganyiko wa udongo kutoka mataifa tofauti.

Moyoni ikanijia sera za vijana wa sasa wa kitanzania wanavyohimizana kukataa ndoa, yani hawajui tu utamu uliopo kwenye ndoa, basi tuwaache hadi yakini itakapo wadhihirikia. Nikaanza kujenga ukaribu na watumishi wa makanisa ya kisabato …

Kwa Bosio haikuwa tabu kwa kuwa tayari alishaishi na mume na pia aliwahi kuwa na boy friend mwingine waliyeishi nyumba moja, kazi itakuwa ni ndogo ya kumshawishi afungue moyo ili aweke nafasi ya upendo kwa mtu mwingine.

Kwangu binafsi ilibidi nichukuwe nafasi yangu halisi kwao “kama Baba” ili nifunge milango ya mapenzi na kuruhusu mioyo yao kuanza kufikilia uhalisia na kutenga nafasi kwa ajili ya waume watarajiwa.
===

Miezi ikakatika na siku ikafika Janeth akaja Dar kaka yake Dotto kwa ajili ya kununua bidhaa. Safari hii nikamuomba Janeth abaki Tz kwa muda mrefu zaidi lakini Dotto ndiye arudi na mzigo Kigali maana nilikuwa na ‘mambo ya kumuonesha’.

Jumamosi ikafika na nikampeleka kwenye moja ya kanisa kubwa la 7th Day Adventist Dar (kapuni kwa sasa) na kumwambia awe anasali humo. Mimi na Hamida tulikuwa tuna m-‘drive’ hadi hapo na baada ya misa zao tunampitia na kuendelea na kujamiiana (socialization)

Baada ya tafsiri maneno ya Janeth…

“…Nilivyoingia tu mule kanisani, kila mtu alikuwa ananitazama na kwakuwa niliona baadhi siti za mbele ziko wazi basi nilitembea huku macho yote kanisani yakinilenga mimi hadi nilipo keti…”

“…Baada ya misa wakati ule wa kusalimiana, watu wengi walikuja kunisalimia akiwemo mchungaji mkuu na kuniambia kuwa wiki ijayo nisikose maana atanitambulisha rasmi kanisani…”

“…Wanaume wa Kitanzania wakarimu sana, niliona wengi walikuja kunisalimia kwa heshima na kila mtu akitaka kunishika mkono…”

Janeth alituelezea hali ilivyokuwa kanisani kwake pale na kuonesha kufurahia ukarimu alio oneshwa, kwa upande wetu sisi (mimi na Hamida) moyoni tukawa tunafurahi maana tunajuwa fika huko moyo wake utafunguka kwa mwanume atakaye mpenda.
===

Kwa Bosio mbinu ilikuwa tofauti kwa kuwa alikuwa si mtu wa kusali kanisani, yeye hujifungia tu chumbani na kufanya ibada zake, hivyo niliamua nitumie mbinu ya kutoka naye out tukiwa watatu, yaani mimi, Hamida na yeye ili mzani usiwe ume ‘balansi’ na kufanya kuvutia wawekezaji kuja kubalansi mzani.

Nikakumbuka sana enzi ya Tazara Disco lakini nikaamua ngoja tutumie njia ya hoteli kubwa zenye watu wenye heshima zao na kuwa na tahadhali na vijana (wa mujini) pia.

Kwa kuwa alionesha sana kufurahia siku ile ya usiku wa mwafrika pale peacock, basi ikawa ndio chaguo la kwanza ili kila siku jioni awepo pale akiburudika (kwa malengo maalum kwa upande wetu) ili hatimaye ipatikane sababu ya yeye kuanzisha uhusiano.

“Hamida ameshinda…”

Nilijikuta najisemea baada ya kuona ile hali ya kuwaona Janeth na Bosio kuwa ni wapenzi wangu wa siri ikiondoka na kuanza kuwaona kama watoto wangu.

Bosio akawa maarufu pale peackock kwa kuwa alikuwa kwanza siku zote akija Dar anakuwepo pale jioni hadi usiku mwingi (alikuwa haachi kuja kulala nyumbani) lakini pia ikipigwa miziki ya Kikongo alikuwa ‘anayarudi’ vizuri kiustaarbu huku akiimba kilingala na kufanya awe kivutio kwa washereheshaji .

Hamida akawa na Amani ya moyo nami nikawa naendelea kuimarisha afya yangu ya mwili ili zoezi la kumwagilia lisikome bali ufanisi uongezeke na kufurahia maisha baada ya kustaafu nikiwa na amani furaha na upendo.


ITAENDELEA…
 

Attachments

  • JBS1.jpg
    JBS1.jpg
    9.7 KB · Views: 53
  • HBJB59.jpeg
    HBJB59.jpeg
    8.5 KB · Views: 46
  • bgg1.jpg
    bgg1.jpg
    10.9 KB · Views: 55
  • KG1.jpg
    KG1.jpg
    30.8 KB · Views: 51
INAENDELEA…

“Well, its okay, lets share the room and I promise will not swallow you…” tukawa tunacheka huku tukielekea chumba husika maana mwenzangu pale inaonekana ni mwenyeji.


2. Sehemu ya pili – KISOMO CHA WATU WAZIMA

Tahadhari zote nilikuwa nazo, za kiusalama wangu na mali zangu pamoja na kifaragha maana matukio ya kusikitisha hutokeaga kama hivi. Hoteli ilikuwa ni ghorofa, sisi tulipata’ first floor’ na chumba kilikuwa kikubwa kiasi cha kusema kwa hela ile ni halali tu.

Nilikagua kila chumba kama kuna kamera-fiche, nikaona pako salama, nikawa nimekaa kwenye kochi na mwenyeji wangu wakati huo alikuwa kwenye kitanda. Mara simu ya mezani pale chumbani ikaita, Janeth akaipokea , kumbe aliweka oda tayari ya chakula kwa ajili ya watu wawili. Mlango ukabishwa na akaingia mhudumu kuleta chips kuku mbili na kuondoka.

“Tule kwanza kisha ndio tuangalie utaratibu wa kulala…” nilipendekeza na ikapita bila kupingwa.

Nilipendekeza pia tuanze sahani moja kwanza wote kwa pamoja na kama hatujashiba basi tuhamie sahani nyingine. Hii ilikuwa mbinu ya kujihami na madhara ya kwenye vyakula, kama yapo basi yatupate sote na wakati wa kula nilihakikisha nasoma lugha ya uso wake ili kujiridhisha.

Maskini binti wa watu wala hakuwa na makuu bali ni ukarimu tu wa kawaida na kama alikuwa na agenda ya siri basi sikuiona haraka ukiachilia mbali na suala la kushiriki tendo la ndoa.

Mfukoni kweli sikuwa na hela za kutosha kwa mambo ya ziada, zaidi ya yale niliyo jipangia hadi kufika Congo, hivyo sikuwa na mzuka maana boom la kustaafu lilikuwa bado kutoka na tayari nilishasota mtaani miezi kadhaa hivyo vihela vyangu vilikuwa vya kuunga unga. Nikatuma ‘txt msg’ kwa Jason Jr ili aniazime dola mia tano atume kwenye account yangu ya benki just incase. Kabla sijalala muamala ulisoma kwenye akaunti yangu.

Janeth alikuwa huru tu, akaingia bafuni na kibegi kidogo na alipotoka alikuja amevaa kaptura na juu alikuwa amevaa fulana nyepesi (haikuwa night dress hizi tunazozijua)

“I am in my period so don’t try anything nasty…!” aliniambia huku akiingia kwenye blanket tayari kuutafuta usingizi.

Moyoni nikajisemea afadhali maana umenirahisishia mambo mengi ambayo tayari nilikuwa nawaza kichwani. Sikuwa na soksi wa vipimo vya kupimia tanesco kama ipo. Nikaingia bafuni na kuanza kuoga, wala sikutumia muda mrefu nikatoka kuja kuungana na Janeth ndani ya blanket na kuanza kuzungumza mengi katika kutaka kufahamiana zaidi.

Saa sita kasoro hivi usiku, Janeth alipitiwa na usingizi akiwa bado amelalia mgongo, nilijuwa baada ya kumuuliza swali fulani ili niendeleze stori niliyokuwa namsimulia lakini hakujibu, kugeuka ndio nikaona amelala hana habari. Nikamfunika blanket vizuri nami nikavuta upande wangu nikawa kama nimelala lakini nipo hadhiri masikio waruuu!

Saa tisa na nusu hivi usiku aliamka kwenda maliwatoni , nilikuwa macho bado maana sikutaka usingizi unipitie hata chembe ingawaje nilifunga macho.

Huwa nina kawaida ya kuamka asubuhi saa kumi na robo kwa ajili ya maandalizi ya siku pamoja na ibada za asubuhi lakini siku hiyo sikusikia alarm hadi saa kumi na moja haja ndogo iliponibana nikaamka na kuangaliaa saa! Nilishangaa sana. Janeth bado alikuwa amelala. Nikaenda maliwatoni na kujimwagia maji safi ya moto tayari kwa maandalizi ya kuendelea na safari. Nilivyotoka bafuni nilimkuta Janeth naye ameamka amekaa kitandani.

“Goodmonring Jane! Leo nimechelewa kuamka na wala sikusikia alarm ya simu…” Nilimsalimia na akajibu…

“Goodmornind Dad, pole kwa uchovu…”

Nje pilika za bodaboda zilikuwa zinazidi kuongezeka, bajaji na magari madogo maana tulikuwa kando kando tu ya barabara ielekeayo stendi.

“Kumekucha, kajiandae tusije tukachelewa…” nilimwambia.

“Bado kuondoka, saa kumi na mbili ndio basi litaondoka, muda bado hata hivyo ngoja nijiandae haraka haraka…” alisema.

Kama nilivyoeleza awali kuwa katika kuandika najaribu kunyoosha maneno yake angalau wewe unayesoma uelewe, lakini ilikuwa ni lugha gongana kwenda mbele ingawaje tulielewana kwa kuchanganya lugha zote mbili Kiswahili na Kiingereza.

Awali nilimuona Janeth kama ni aina ya wale wanawake wafanya biashara ambao wapo tayari ku ‘risk’ chochote ili mradi aingize hela hivyo nami nika ‘adopt’ uelewa ule ndio maana nikaomba nitumiwe hela ambayo hata haikuwa kwenye bajeti ya safari yangu. Uchumi wangu ulikuwa ni wa kawaida tu wa kujikimu ndio maana fursa hii ya kufanya kazi siku 90 DRC niliichangamkia.

“Uko mubaba muzuri, hujanisumbua…” alisema Janeth wakati akimalizia kujipamba.

“My period ended the day before yesterday but I’m not that clean for the game ndio maana nilikuambia nipo kwenye siku zangu…” Aliendelea kujisemesha.

“it’s okay Janeth, mimi wala sikuwa na mpango wowote na nilidhani ningelala kwenye basi, ahsante kwa ushauri wa kupumzika lodge…” nami nilijiongelesha.

Tulitoka pale huku akikataa mimi kuchangia gharama za lodge na chakula, lakini nikawahi kulipia bodaboda mbili ambazo zilitufikisha stendi saa kumi na mbili kasoro dakika kumi.
===

Kifungua kinywa tulipata Ushirombo ambapo pia walitumia nafasi hiyo kujaza mafuta kwenye basi, baada ya hapo moja kwa moja hadi Nyakanazi tulipoacha lami na kuanza njia ya vumbi na mashimo kuelekea Rusumo. Ni kilomita chache tu lakini tulitumia muda mwingi sana kufika border ya Rwanda na Tanzania.

Baada ya kukamilisha taratibu za border na kuvuka, nikaenda kwenye ‘restaurant’ upande wa Rwanda sasa ili nipate chakula, wakati huo Janeth yeye na wafanyabiashara wengine walikuwa wakikaguliwa mizigo yao hapo border ya ajili ya mambo ya ushuru nk. Alinirusuhu nikale maana huenda yeye angechukuwa muda mrefu kukamilisha zoezi. Ni kwamba hapo mpakani kwenye basi hushuka abiria wote na mizigo yote hushushwa ya kwenye buti na ndani ya basi na kila mmoja kupitia ukaguzi kulingana na mzigo wake kisha kwenda uhamiaji kama taratibu za kuvuka boda zilivyo.

“Nipatie mashilingi hayo nikupe faranga, ‘rate’ nzuri kabisa nakupatia…” alisikia ‘husler’ mmoja hapo nje ya restaurant.

Nilibadili dola mia kwake na nikamwomba anipatie kijana anayesajili line ya mtandao wa MTN ili nipate simcard ya Rwanda.

Zoezi la kuvuka hadi basi kuwa tayari kuondoka lilichukuwa zaidi ya saa tatu na kufanya tuwe nyuma ya ratiba ya kawaida ya basi. Abiria wengi walikuwa na mizigo ambayo ilikuwa na utata katika kuvusha lakini hatimaye wote tulifanikiwa kuvuka.

Baada ya kuvuka, dereva tuliyetoka naye Dar alipumzika kwenye siti namba moja na yule dereva wa pili, Mnyarwanda alichukuwa nafasi.

Sasa sijui kwa kuwa tulikuwa nyuma ya ratiba ama ndio uendeshaji wake, ee bwana ee, mwendo ulikuwa si wa kitoto, kuna wakati kwenye gps yangu speed ilisoma hadi 160kph ikabidi niinuke niangalie dashboard ya basi. Njia ilikuwa ya lami lakini nyembamba halafu basi lilikuwa linatembea upande wa kulia, kila mara nikajikuta nabana breki mimi ilhali siye ninaye endesha maana si kwa kuhisi hatari zile! Tena mpambe nilimsikia akisema amsha amsha!

Kabla ya kufika Rusumo, njiani kuna baadhi ya abiria washuka, mmoja tulimwacha pale kizuiani maana watu wa uhamiaji walimtuhumu ame ‘overstay’, wengine walishukia Lusahunga, Benaco na Mizani. Hivyo basi ilipata nafasi kiasi cha kupakia abiria wengine pale boda baada ya kuvuka. Mmoja wa hao abiria nadhani alikuwa wakala wapo ndiye alikuwa akihamasisha sana kuwa gari imechelewa.

Nilikuwa nadhani Rwanda mabasi hayakimbii kama nilivyosikia awali lakini ilikuwa kinyume chake hadi tuliposogea mbele mbele sana na giza likaanza kuingia ndip mwendo ukawa wa kawaida. Ni wastani wa kilomita 160 hivi kutoka Rusumo border hadi Kigali, lakini huwezi kuamini, tulifika saa tatu hivi usiku iwakuwa wakati tunakaribia mjini Kigali tukakuta foleni ndefu sana iliyotulazimu kutembea ‘jino moja moja’.

Safari ilichosa sana kipande cha Nyakanazi hadi Rusumo, tulitembea taratibu mno kwakuwa njia ilikuwa na mashimo na rasta baadhi ya sehemu, haikuwa njia rafiki kwa kweli licha ya umuhimu wake njia kuu hiyo. Nadhani sikuhizi pako vizuri, sijapita tena kwa barabara.

Janeth alinipa ofa ya kwenda kufikia kwao, ingawaje niliikataa na kumweleza kuwa mimi ni mpita njia tu naelekea Rubavu (nilimdanganya). Rubavu ni moja ya majimbo ya Rwanda jirani na Congo huko. Akaniambia basi kesho yake nisiondoke ili anitembeze Kigali kwenye ‘sabasaba’ yao. Focus yangu haikuwa kwenye kutalii bali kibarua kinachonisubiri huko Goma. Lakini nikaangalia kalenda nikaona bado nipo mbele ya muda na nina siku 4 mbele kabla ya kuripoti nikamkubalia ombi la kunitembeza Kigali.

Haikuwa mara yangu ya kwanza kuwepo Kigali lakini nilitaka nipate ‘experience’ nyingine kupitia huyu Janeth ambaye naona kama anataka kunizibia kufurahi na watoto wengine wa Kinyarwanda. Alikuwa anakaba sana kana kwamba tumekubaliana chochote.

Wajihi wangu ni bonge la mtu, mrefu futi sita hivi, maji ya kunde, heavy weight 105Kgs, ndevu zote mvi kichwani nimenyoa unga kuficha wingi wa mvi, nilivalia kawaida tu suruali ‘cadet’ na shati ‘cadet’ la mikono mirefu nililovaa Kahama maana kutoka Dar nilivaa ‘tshirt simple’. Sura yangu haijazeeka ingawaje ukiniangalia kwa makini ndio utaona kilomita zimeenda, hivyo nadhani nilikuwa naonekana bonge la Bwana. Yeye Janeth alibadili nguo zote pale Kahama, mimi suruali sikubadilisha. Alivaa gauni refu na mapambio yake.

Tulibadilishana namba za whatsapp na nikampa namba yangu ya MTN. wote tulishuka Nyabugogo bus terminal. Yeye Janeth alichukuliwa na pickup townhiace ambayo pia ilipakia na mizigo yake, mimi nikachukuwa TOYO (bodaboda) na kunipeleaka Kaizen Hotel ambayo haikuwa mbali na stendi.

Pamoja na mambo mengine, chumbani nilipokelewa na kitanda chenye godoro lenye ‘finishing’ ya material yasiyopitisha maji. Mawazo yakarudi kwa Janeth.

“Hawa si ndio mabingwa wa kurusha maji katika harakati za kilimo ya umwagiliaji!, kwanini nisitumie fursa hii kupata elimu ya watu wazima…” niliwaza. Nikaanza kuona saa haziendi. Kabla ya saa tano usiku kwa saa za Bongo nilikuwa nimeshaegesha, na usingizi haukuchukua muda kunipata kwa kuwa nilikuwa na uchovu uliotokana na usingizi wa mang’amng’am wa Kahama na uchovu wa safari. Nikakumbuka maneno ya Janeth kuwa nisilale kwenye basi nitachoka sana, nikaona kumbe alinishauri vyema ingawaje uchovu mwingi ulitokana na mimi kutolala vema kule Kahama.

Saa kumi na robo simu iliniamsha, nikachungulia nje bado giza sana, ikabidi nirekebishe saa yangu iendane na majira ya kule, hivyo nikarudisha dakika sitini nyuma. Nikaendelea kuegesha huku nikitafakari baadhi ya mambo. Usingizi ukanichukuwa tena hadi nilipostuka saa moja asubuhi kwa saa za Rwanda. Nikaamka na kujiandaa kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.

Restaurant wageni wenzangu walikuwepo wengi wakijihudumia kupata breakfast, nami nikaungana nao, wengi wao walikuwa wakiongea kinfaransa na baadhi Kinyarwanda. Wahudumu wa kike wa hoteli walikuwa kama wale tunaowaona kwenye mitandao lakini huko mitaani wanawake wengi sana ni wa kawaida tu tena wengine wala si warefu ama warembo kivile ama wenye maumbile hamasishi. Nikakumbuka ule usemi, ukitaka kuifaidi Kigali, fikia hotel zenye hadhi ya juu ama tembelea kwenye ma-‘shopping mall’ na sehemu kama hizo huko ndiko kuna vile vitu wabongo wengi tunababaikaGa navyo.

Wakati nikiendelea kupata staftahi nilipokea simu ya kwanza kwenye line ya MTN kutoka kwa Janeth, nilijuwa tu ni yeye maana namba bado sikuwa nimeigawa kwa watu wengine.

“…I will be at Nyabugogo terminal at ten thirty, lets meet at Trinity Bus office…” aliniambia.

Ilipofika saa nne kasoro kidogo nami nikakabidhi mzigo wangu mapokezi na kushuka chini kuchukuwa toyo ili inifikishe jirani hapo stendi. Saa nne na dakika chache nikaona nafwatwa kwa ishara ya kukumbatiwa, alikuwa na tabasamu na mwenye uso uliokunjuka.

Baada ya kumbatio motomoto pale na kupeana pole za uchovu akaniambia kuwa yeye hakai mbali sana na hapo, anaishi maeneo ya Kacyiru. Akaniahidi kunipelea kwao. Nikakubali. Lakini akaniambia tuelekee kwenye maonesho kwanza ili tuzunguke humo wee kisha ndio tuende kwao kisha kuzurura jijini Kigali.

Akaniambia tuchukuwe taxi.

“Nyamuneka utujyane i Magerwa…” alisema Janeth akimwambia yule dereva wa teksi atupeleke sehemu iitwayo Magerwa.

Dakika chache tu baadaye tukafika hapo Magerwa, ni kama vile bandari kavu fulani hivi, hatukuingia ndani badala yake akaniambia tutembee kuelekea upande uliouoneshea kidole.

“We are heading to Gikondo area, sio mbali ni paleeee…” alisema.

Kumbe hapo Gikondo ndio kuna sabasaba yao, tukalipa kiingilio na kuingia ndani. Pamoja na mambo mengine ya ki-‘trade fair’, nilikutana na visu hasa, yani Jane wangu nilimuona wa kawaida sana, ingawaje yupo vizuri kisu haswa lakini asikwambie mtu, macho ya wanaume hayachoki kuona vitu vizuri. Tulijifunza mengi humo na baada ya kuchoka tuka kaa sehemu kama mghahawa hivi mumohumo kwenye maonesho na kuanza kuongea mawili matatu huku tukipata viazi mbatata, maharage na samaki kama sato.

Baada ya hapo tulifanya mzungukowa pili ambao sasa huu ulilenga sehemu maalumu tulizoziona kwa ajili ya kununua baadhi ya bidhaa alizotaka nami nikaambulia kununuliwa mkanda wa ngozi pamoja na wallet kutoka kwa wafanyabiashara waliotoka Misri.

“Zawadi yako uwe unanikumbuka…” alisema Janeth.

Baada ya muda kidogo tulitoka tukiwa na mizigo yetu na kuchukuwa Taxi.

“…Kacyiru…” Janeth alimuambia yule dereva na tukaanza kuondoka.

Nilifurahia nidhamu ya barabarani ya madereva wa kule, yani madereva wote wa vyombo vya moto. Sheria za usalama barabarani zilikuwa zinafuatwa vyema.

Baada ya kona mbili tatu nikaona dereva akiuliza maelekezo ya ziada, alipopatiwa nikaona amekuja tena kona kadhaa kisha tukafika eneo tulivu lenye nyumba nzuri yenye ‘umatemate’ fulani hivi.

Nilikaribishwa vizuri na tulikuja kupokelewa na watu wengine mle ndani. Baada ya utambulisho mle ndani mwao kwa waliokuwepo tukaletewa chakula. Kulikuwa na ndizi nyama na vikorobwezo vingine, tukala huku tukiendelea na mazungumzo ya kawaidia.

Baada ya kama saa moja hivi akaniambia twende sasa nikutembeze Kigali. Tukatoka mle ndani, akawasha gari yake vw golf (baby walker) na tukaelekea katikati ya jiji moja kwa moja kwanza kwenye duka lake. Awali nilidhani ni duka dogo tu la wajasiri-amali, lakini kumbe dooo! Ni bonge la duka lililosheheni nguo za wanawake tu.

Alinitembeza kwa gari pale mjini, kisha kwa miguu hadi ilipofika saa moja jioni kwa saa za Rwanda tukarudi dukani kwake ili achukue gari turudi nyumbani kwao. Kwa kweli nilifurahia kubaki Kigali siku hiyo. Tulifika kwao saa mbili kasoro hivi kwa saa za kule na kukaribishwa. Safari hii nilikuta familia imeongezeka, yaani baba yake alikuwepo, mama yake, dada zake na kaka zake. Ilikuwa ni familia yenye furaha. Ilikuwa ni familia ya aina yake ambayo baba ni Mhutu na mama ni Mtutsi, ni familia ambayo imejaribu kuvuja jambo la ukabila katika nchi hiyo na Baba ni afisa wa Polisi katika Serikali ya Rwanda.

Niliwaza hapa nikijichanganya tu napata ndoa ya uzeeni, maana si kwa ukarimu ule sijui hata Janeth aliwaambia nini. Janeth alikuwa mtoto wa tatu kuzaliwa akitanguliwa na dada zake wawili kisha kufuatiwa na kaka zake wawili. Dada zake wote walikuwa wameshaolewa, lakini yeye na kaka zake walikuwa bado hawajapata ndoa. Baada ya chakula cha jioni, niliaga ili niwahi kupumzika maana asubuhi nilitaka nianze safari kwenda Gisenyi -Rubavu Province kama nilivyomuambia Janeth. Sikutaka ajuwe kama nitavuka mpaka na kuingia Congo kwa wakati huo.

Tulitumia gari ya Janeth hadi aliponifikisha Hotelini kwangu na nikamkaribisha hadi chumbani.

Dhambi iliyofuata nilishaitubu na ugomvi wake na Hamida ulishaisha maana hata yeye alifurahia elimu ya watu wazima niliyoipata huko Kigali niliporudi. Nilikuwa najuwa ‘katerero’ lakini hapa nilipata elimu ya ‘kuyanza’, sijui hata kama nimepatia inavyoandikwa. Ni hatari sana.

Katika kuitumia elimu hii ni muhimu wote muwe na afya njema vinginevyo mtaambukizana maradhi yatokanayo na kujamiiana (ngono). Ni kama vile katerero lakini hii tuseme ni katerero promax. Mtanisamehe, siwezi kuielezea hii hapa kwa sababu ya kuepuka matumizi mabaya ya hii kitu kwa wasiokuwa na ndoa.

“Usiondoke na basi za asubuhi, ondoka saa nne ili upate kupumzika vizuri…” yalikuwa maneno ya Janeth baada ya kumuomba anifundishe kilimo cha umwagiliaji kama kifanywavyo na wanyarwanda.

Nilipata elimu murua, na hakika wana haki ya kuweka sheria ya kila nyumba ya kulala wageni kuwekwe zile foronya zisizopitisha maji. Ewe kijana unayefikiria kuoa Mhaya ama Mnyarwanda, hakikisha unajifunza kilimo cha umwagiliaji maana kwao ni muhimu na haki ya msingi vinginevyo tarajia kutembelewa na kutambulishwa ndugu zake wa kiume usiowajuwa ama kuombwa safari ya kurudi kusalimia mara kwa mara alipotoka ili mradi tu kilimo cha umwagiliaji kifanyike.

Nilikubaliana na wazo lake la mimi kuondoka saa nne asubuhi, hivyo sehemu kubwa ya usiku nilikuwa darasani hadi maji yalipoamua kukatika kabisa, tukalala.

Saa nne na nusu tayari nilikuwa stendi kuu, pale kulikuwa na basi ziendazo Gisenyi, kila baada ya dakika kadhaa basi moja hutoka. Nilipanda RITCO, kampuni yenye huduma bora kabisa Rwanda ambayo baadaye nikaja kujuwa ni mpango mzuri wa viongozi wa Jeshi lao kubuni mradi huo. Safari ilikuwa nzuri na mwendo mzuri kwa sheria za kwao lakini nilikerwa na waendesha baiskeli ambao hushikilia malori kwa nyuma na kupata lifti hatarishi isiyo rasmi.

Kuna sehemu nimeshapasahu, tulipumzika kupata chakula kisha tukaendelea na safari. Yes panaitwa Nyirangarama, nimeona kwenye picha niliyopiga. Njia ni ya milima na mabonde, dereva huko inabidi awe timamu kuweza kuendesha bila kusababisha ajali. Takribani kilomita 150 kutoka Kigali nikaanza kuona ziwa upande wa kushoto, nilipouliza nikaambiwa ni ziwa Kivu, basi lilikuwa linashuka mlima taratibu maana kona ni kali mlima una mwinamo mkali lakini hatimaye tukafika Stendi kuu ya Gisenyi mpakani kabisa na mji wa Goma – Congo, Kivu Kaskazini.

Kwakuwa ilikuwa jioni, sikupenda kuvuka mpaka siku hiyo, bado nilikuwa nina siku mbili za ziada kabla muda wa kuripoti kibaruani. Hivyo niliamua kutafuta sehemu nzuri ya kupumzika. Baada ya kuuliza wenyeji sehemu ya bei nafuu lakini patulivu na usalama mkubwa ndio nikaaelekezwa sehemu Fulani wanapaitwa kwa Mapadri. Nikachukuwa bodaboda hadi huko. Ile sehemu ni kama Msimbazi centre ya Dar es Salaam. Wana rest house nzuri na tulivu sana. Hapo ndipo akili ya kazi ikaanza kurudi upya maana nilitulia na kuanza kutafakari kibarua ninachokiendea.

Ilikuwa siku ya Ijumaa jioni nikiwa hapo kwa Mapadri, nikapata wasaa wa kutembea kwa miguu hadi ufukweni mwa ziwa Kivu sehemu ambapo watu hupenda kutembelea jioni kama vile Coco beach ya Dar. Hapo uzalendo ukanishinda ikabidi niingie kuogelea na kuchanganyika na wenyeji lakini sehemu ya upande wa watu wazima maana kama vile watu walijigawa, hapo nikakutana na visu vingine hatari. Pia kulikuwa na boti kadhaa za wajasiri-amali ambao walikuwa wanapiga debe ili wapate wateja wa kuwatembeza ziwani kwa ujira wa fulani (dola 10).

Siku yangu iliisha vizuri na giza lilipoingia nilitembea kurudi kiotani kwangu hapo kwa Mapadri. Baada ya chakula cha jioni ambacho nilikipata jirani na hapo kwa Mampadri nilirudi chumbani na kuendelea kuandika simulizi ya Hamida nikisogeza ‘episode’ kuwapunguzia arosto wafuatiliaji wa kila siku mwaka huo. Baadaye nikaanza kupitia yanayohusu kinachonipeleka Goma kwa kuhakikisha nimehabarika ipasavyo kufikia tarehe ya siku hiyo.


INAENDELEA…
mpwayungu village njoo uone huku
 
MSIMU WA PILI
Season II

Hekaheka
Uzeeni

(i). Ugomvi, Suluhu, Faida.

Ilikuwa siku ya alhamisi mchana Hamida alipokuja kunipokea Ubungo bus terminal. Nikiwa mwenye furaha ya kumuona mke wangu lakini yeye alikuwa amenuna njia nzima tulipokuwa tunaelekea Kariakoo kumsindikiza Bosio hoteli ambayo aliambiwa na wakala wake afikie. Aliendesha Nadia yake kwa kasi ingawaje foleni za hapa na pale zilikuwa zinamzuia asikimbie kwa muda mrefu.

“Atafikia Sleep inn hotel ya Kariakoo…” nilisema wakati mwendo wa gari ulikuwa umekolea baada ya kupita taa za mtaa wa Msimbazi na Morogoro rd.

Ni kwa bahati tu taa nyekundu zilituzuia kuendelea lakini dalili za kulala na speed zote niliziona. Baada ya taa kuruhusu alikunja kuingia barabara ya Lumumba, njia ilikuwa na magari mengi hivyo hakuweza kulipelekesha gari.

“Ingia mtaa wa Mahiwa..” nilimuelekeza Hamida.

Mbele kidogo jirani kabisa na mtaa wa ‘jiwe linaloishi’ akapaki na Bosio akashuka na kushukuru kwa lifti.

“Merci Papaa pulabalade…” Alisema akimaanisha anashukuru kwa lift.

Nikafunga mlango na kurudi kwenye siti yangu na kufunga mlango na mkanda, mara nikasikia..

“Mercii ya nyoko!”

Nikamwangalia wife kisha nikatikisa kichwa na kukaa kimya. Safari iliendelea hadi tulipofika nyumbani tukiwa kama mabubu maana niliamua nijizuie kusema lolote. Nyumbani nikashusha mizigo vizuri na begi langu yeye akiwa bado amenuna na kuelekea jikoni.

Uzuri wa Hamida ni kwamba, hata kama amenuna huduma zingine zote anakupatia vizuri tu, hivyo sikuwa na wasiwasi wa kunyimwa huduma za nyumbani.

Baada ya kuoga kuliko nichukuwa muda mrefu, nikajiandaa na kuelekea sehemu ya maakuli ambako nilikuta ameniandalia chakula changu pendwa kama kawaida. Nikakaa chini ‘mkekani’ na kuanza kula peke yangu.

Baada ya chakula nikapitia mitandao ya kijamii kidogo kisha nikaenda kijilaza chumbani. Saa kumi na mbili kasoro hivi niliamshwa kwa voice call ya whatsapp kutoka kwa Janeth.

“Du hekeheka uzeeni hizi…”, nilijisemea.

“Halo, habari, ulifika salama?” ilikuwa sauti ya Janeth akiongea.

Nilimjibu na kuongea naye mawili matatu, mara Hamida akaingia na kukaa jirani huku akisikiliza. Ila nyie wanawake, Mungu anawaona. Muda wote mko na hisia hisia tu. ‘Anyway’ (siyo ‘anyways’), ndivyo jinsi mlivyoumbwa.

“Hii simu ni kutoka nje ya nchi, ni familia iliyonifadhili kule Kigali wakati wa ‘lockdown’ wanataka kujuwa kama nilifika salama…” nilijitetea baada ya kukata simu.

“Enhe, hebu niambie, yule mwanamke tuliye mshusha kule hotelini ni nani!” aliuliza Hamida kwa hamaki.

Ikanichukuwa muda mrefu kumuelezea kuanzia pale mpakani Gatuna jinsi tulivyokutana na safari yetu hadi tulivyofika na kwamba hakuna kinachoendelea. Baada ya majibizano ya muda mrefu hatimaye alikubali kushuka chini na kuomba afungue mizigo yangu akague. Ila wanawake! Nimewavulia kofia.

Akajifanya anatenganisha nguo chafu na safi na kuziweka sehemu zake, akakung’uta begi kuhakikisha hakuna kitu kilichobaki kisha akahamia kwenye mzigo mwingine ambao ndani kulikuwa na vitenge vyake.

Kwenye ule mzigo, vile vitenge vya dola 50 hamsini niliviweka juu na vile vya dola 80 themanini niliviweka chini. Sasa alivyoanza kufungua ule mzigo akaanza kusasambua na kuvirusha kitandani…

“Hivi si ni sawa tu na vya Kitumbini! Wala hakuna tofauti yoyote..” alikuwa aking’aka kama vile bado ana kitu rohoni.

Mara paap akavifikia vile wax orijino! Nikaona tu anatabasamu na kusema…

“Hivi sasa ndio vitenge…”

Aliendelea kuvichambua vyote na kuishia kusema vizuri sana, ahsante! Akanikumbatia pale kisha akaviweka vizuri.
===

Usiku ule ulikuwa murua kwani nilifanya zoezi la kilimo cha umwagiliaji na kufanikiwa kama wafanyavyo wakulima wa Kinyarwanda lakini nilibandikwa maswali ambapo majibu yake ndiyo yaliyoleta ugomvi na kusameheana baadaye.

Ni kwamba Hamida alikuwa anamfahamu Janeth na familia yao kwakuwa tulikuwa tunawasiliana kwa ‘video call’ na alikuwa ameongea na watu wote ndani ya ile nyumba (Kigali), lakini hakuwa amedhani kwamba nimechepuka na mmoja wao hadi aliponibana kwenye kilimo cha umwagiliaji.

Ilikuwa ni ulimaji tofauti na aliouzoea, tulio uzoea!, ingawaje hata kabla ‘kilimo kwa kumwagilia’ kilikuwa kunafanyika. Sasa hii ‘pro max’ aliona ni tofauti sana na kunibana nimueleze nilipojifunzia. Nikaamua kusema ukweli kuwa Janeth alinifundisha. Mama yangu! Kilichofuata hakiandikiki.

Lakini mwisho wa yote vile vitenge vilimpooza na kumwambia vile vya ziada yeye aamue nani ampe na nani asimpe lakini kali kuliko yote alitaka tena kumwagilia bustani.

Baada ya kuridhika kuwa bustani imelowana maji vya kutosha akatulia na kusema…

“…lakini tamu…” Nimekusamehe, lakini utanipeleka ‘shopping’ ninapopataka mimi kama fidia.

Kusikia hivyo mzee mzima nikataka sasa nipeleke moto ile kibongobongo lakini mjamaa kichwa wazi ‘akazila’ kabla hata moto haujakolea, nikajikuta tu nasema hii sasa ni hekaheka uzeeni. Ilibidi kuahirisha zoezi na kupisha mwili na akili vikae sawa hadi kulivyokucha asubuhi.

ITAENDELEA...
Ahahahahah
 
Back
Top Bottom