Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
- Thread starter
-
- #141
Mkuu, kwa hiyo kwa maoni yako mambo ambayo ni kinyume na TABLE MANNERS ndio haya pekee?...kula chakula uku mtu anaongea ni tabia mbaya....kula uku unaangalia wenzako machoni....au kutafuna uku Domo liko wazi Kama nguruwe iyo ni tabia mbaya
Tatizo kubwa kwa jamii za kiafrika ni kutokuwa wawazi na unafiki uliopiitiliza
Mkuu, unaweza kutoa hewa chafu mbele ya idadi kubwa ya wageni? Bado nitazidi kusisitiza;unaona aibu ni Jambo gani utakuwa huru kufanya mbele ya kadamnasi?
hahaha 16 castle lager cheeeKula Ni kipaji, nilikuwa na msichana anaitwa Queen. Alikuwa anakula zaidi ya kg tano za kitimoto peke yake na bia 16 castle larger.
Usimkaribishe harusini kwako
Kaka mkubwa, what do TABLE MENNERS honestly mean to you?...
Siku zote anza kwa kuchukua chakula kiasi ili wote mpate, kisha ongeza chakula kwani wapo ambazo kila kiasi cha mwanzo kimewatosha, hii ndiyo table manner sahihi.MADA YA LEO: NI MUHIMU SANA MTU KUWA NA NIDHAMU YA KULA KWA STAHA MBELE YA WATU (KADAMNASI)
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi. Kila siku tukikaa kujadili masuala ya wazungu ni nani atazungumzia ustaarabu wetu?
Ndugu zangu wa Tanzania;
Miezi kadhaa iliyopita nilipata kuhudhuria sherehe moja ya harusi ya mtoto wa kike wa ndugu yangu wa karibu sana iliyofanyika katika ukumbi fulani maarufu sana kule mkoani Arusha. Kusema ukweli wa Mungu harusi ile ilifana sana. Ndugu, jamaa na marafiki sote tulijumuika tukala na kufurahi kwa pamoja.
Tulipiga story mbalimbali pamoja na kukumbushana mambo ya zamani kwa maana ilikuwa ni fursa pia ya kuonana na watu ambao hatukuweza kuonana kwa muda mrefu sana. Sasa kama inavyofahamika na wengi kwamba sherehe huwa ni ratiba mahususi na ratiba ile huwa ina vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na kuwapokea maharusi, kutambulishana, kwenda kuchukua chakula pamoja na utoaji wa zawadi.
Hapa kwenye uchukuaji wa chakula ndio mada kuu ya mjadala kwa siku ya leo. Muda wa chakula ulipowadia ndugu mshereheshaji (MC) aliwaita maharusi kwanza, kisha wakafuata wazazi wa pande zote mbili na kumalizia na sisi akina Infantry Soldier (Kwa maana mimi kudandia sherehe ni kama ulimi na mate hahahaaaaaa I am joking....!!!!!!)
Bwana harusi alikuwa ni mtoto wa kiongozi fulani huko na yeye binafsi alikuwa anafanya kazi katika NGO moja kubwa tu huku Dar, hivyo ile sherehe ilikuwa ni ya budget kubwa kiasi. Hakika chakula kile kilikuwa ni kitamu sana sana tena saaaaana.
Kila mtu alikula na kufurahi lakini cha ajabu MC yule yule akatangaza kwa mara kadhaa kwamba ndugu wageni waalikwa mabibi na mabwana, CHAKULA BADO KIMEBAKI KINGI TU KWA ANAYETAKA KUONGEZA RUKSAAA hahahaaaaaa hapa ndio kasheshe ilipokuwapo. Amini usiamini, hakuna aliyethubutu hata kusimama kwenda kuongeza msosi isipokuwa jamaa fulani 3 ambao ni rafiki wa bwana harusi.
Kile kitendo walikifanya wao lakini aibu niliiona mimi. Inakuwaje mtu mzima na ndevu zake anashindwa kuizuia tamaa ya muda mfupi na kuamua kujidhalilisha namna ile mbele ya kadamnsi?
Sasa ndio nikajawa na maswaki mengi kuliko majibu kwamba;
Je, unafikiri ni jambo sahihi na busara mtu kukosa Busara na nidhamu ya chakula (Table Manners) mbele ya kadamnasi ya wageni?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
BIASHARA: Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher
MAONI YA MDAU
=======
Wewe ndio hujui Table Manners...kupakua chakula mara mbili(kuongeza) haina shida shida ni kujaza sahani mlimaa alafu unashindwa kumaliza.Haujui table manners wee jamaa wa uswazi
Aisee umemuelezea vizuri sana huyo bwana mdogo. Unajua tatizo hawa wamezoea kwenda kwenye kipaimara, vijiharusi uchwara na maulid za kiswahili so hawajui chochote kuhusu table manners.Sikia bwana mdogo; Katika sherehe moja ya mashamshamu ya sherehe ni msosi, na kulingana na kauli yako ni kwamba msosi huo ulipikwa kwa ajili ya ninyi mliohudhuria sasa kama chakula kilikuwepo na kuna watu ambao walikuwa hawajashiba na taarifa ikatolewa kwamba yule aliyekuwa bado hajashiba na akaongeze chakula shida hapo iko wapi?? au ulitaka chakula kitupwe??--- labda kama hao jamaa walienda kujipakulia bila kuambiwa hapo ndipo ingekuwa ni tatizo (bad manners).
Punguza dharau mdogo wanguUnajua tatizo hawa wamezoea kwenda kwenye kipaimara, vijiharusi uchwara na maulid za kiswahili so hawajui chochote kuhusu table manners.
Senior Member unamwita Expert Member mdogo wako! Mimi na wewe nani ana dharau?Punguza dharau mdogo wangu
This is not job interview homieMkuu, kwa hiyo kwa maoni yako mambo ambayo ni kinyume na TABLE MANNERS ndio haya pekee?...
Sawa boss.This is not job interview homie
Watu waliokaa! Kwanini tufanye vitu kisa tu nyie hamjafanyaMkuu, unaweza ukanyanyuka na lisahani lako kwenda kupakuliwa nyama ya kuku wakati watu wengine wote wamekaa?
Mfano wako wa kutoa hewa chafu ni irrelevant, hayo ni Mambo ya faragha na bado pia tunafeli sana upande huo, juzi tu hapa nimempa lift jamaa flan tumetembea karibu km80 mkojo umembana lakini alishindwa kuniambia nisimamishe chombo ajisaidie, you can imagine Kama kukojoa tu ambapo Kila mtu anafanya hivo mtu anaona aibu kusema utafikiri ni dhambi FulaniMkuu, unaweza kutoa hewa chafu mbele ya idadi kubwa ya wageni? Bado nitazidi kusisitiza;
Hekima, busara na nidhamu ya chakula (Table Manners) mbele ya kadamnasi ya wageni.
Sasa kwanini! Ufanye judgment kwa watu kisa tu malezi yako! Kila mtu afanye lake kutokana na uelewa wake usitake kulazimisha malezi yako kwa kila mtu mkuuTABLE MANNERS haikukaa sawa kulingana na malezi niliyokulia mkuu...
Asante sana watu Wana overate Mambo Hadi kero , imagine mtu yupo radhi alale na njaa ililmradi asionekane kaongeza chakula !!Sikia bwana mdogo; Katika sherehe moja ya mashamshamu ya sherehe ni msosi, na kulingana na kauli yako ni kwamba msosi huo ulipikwa kwa ajili ya ninyi mliohudhuria sasa kama chakula kilikuwepo na kuna watu ambao walikuwa hawajashiba na taarifa ikatolewa kwamba yule aliyekuwa bado hajashiba na akaongeze chakula shida hapo iko wapi?? au ulitaka chakula kitupwe??--- labda kama hao jamaa walienda kujipakulia bila kuambiwa hapo ndipo ingekuwa ni tatizo (bad manners).
mhhh, ila wee jamaa mawazo yako hata siyapendagiAsante sana watu Wana overate Mambo Hadi kero , imagine mtu yupo radhi alale na njaa ililmradi asionekane kaongeza chakula !!
Na hii ndio sababu tunatengeneza vizazi vya ovyo sana , watu wanapenda kufanya Mambo mengi gizani ili wasikosolewe au kusemwa vibaya ..
Hapo kwenye sherehe Kila mtu alionekana kashiba kumbe Kuna uwezekajo wengine walilala na njaa
Sijawahi faidi nyama za sherehe, kwanza ni kubwa, likuku likuuubwa kulishika kero, afu nakuwaga nimeshiba nakula kiduchu, kurudi home tumbo empty. Mi naona walevi ndo wanafaidi sherehe.Kuongeza msosi mm huwa naongeza sn tu tatizo moja ukifila kwenye kuku huwa wapakuaji wanalaza hvo wanataka uongeze vitu lkn kuku wanabana