TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Mungu aepushie mbali hata kama imeanguka kweli kusiwe na madhara makubwa kwa waliikuwemo.
 
Deo ni Mbunge wa Taifa. Taifa linamuhitaji sana sana mtu huyu
 
Yaani mpaka sasa hivi hakuna aliethibitisha kutokea au kutotokea kwa tukio..?
 
Oh my..! Habari hii isiwe kweli.
 
Upendo,utu,heshima na ubinadamu havina budi kututawala na kutawala fikra zetu,mihemuko yetu,maneno yetu,mawazo yetu,nia zetu,matamanio yetu despite having differences in political perspectives,ideologies etc...Mungu mwema ibariki Tanzania
 
Mungu aepushie mbali na kuzilinda roho zao binafsi namkubali sana FILIKUNJOMBE na siku zote amekuwa mbunge wangu wa mfano regardless chama anachotoka.

Kifo hakibagui
 
Hii ndo Chopa Filikunjombe anayoitumia kwenye Kampeni zake.
 

Attachments

  • 1444939371864.jpg
    1444939371864.jpg
    18.4 KB · Views: 1,299
  • 1444939398348.jpg
    1444939398348.jpg
    21.3 KB · Views: 1,232
Naona uchaguzi huu mungu anataka watanzania wamrudie, kwani matukio ya vifo na ajali za wagombea zimekuwa nyingi.
 
watanzania tunatakiwa tujue kuna maisha baada ya uchaguzi

wakenya wakituambia sie watanzania hatuna akili tunaanza kulalamika wakati matendo yetu tunayoyafanya yanamshangaza kila mwanadamu mwenye utu, hekima, nidham, na uoga wa mungu


haiwezekani thread nzito kama hii mtu anatoa comment eti wafe maiti zao zisionekane, mara mwingine anasema angekuwapo na fulani na fulani

mbaya zaidi utakuta aliyotoa hii comment ni msomi wa chuo kikuu

ndio maana kuna mtu mmoja alisema kuwa watanzania wengi sio wasomi ila wamekaa muda mrefu darasani...


This is so pathetic
 
Back
Top Bottom