Heri tukose misaada kuliko kuamrishwa nini cha kufanya na Ulaya

Kwani kuna anayelazimisha kusaidiwa au kukopeshwa? Mikopo huombwa na anayesaidiwa huomba asaidiwe....... Wenzako wanaomba misaada na mikopo, sababu ya umasikini.
 
Inasikitisha sana. Haya mashetani CCM, damu za hawa watu wasio na hatia zinawalilia kwa Mungu wetu. Laana ya damu za hawa wanadamu wote iwe juu ya watawala mashetani wa Tanzania na mashetani yote yanayowaunga mkono, akiwemo mleta mada.
Hao niliowaorodhesha hapo ni wachache tu wengi wanapotezwa na wengi wanabambikiwa makesi wako majela.
 
Pesa za ndani CAG kasema mnaziiba zote kila kona mnaiba na pesa zote mnazitumia kwenye matendo haramu ya kishetani kuwabambikia kesi chadema kuwatumia Polisiccm kupiga wapinzani
Kama ingekuwa zinaibwa zote basi tusingeona bwana la umeme, daraja la busisi na Barbara vinajengwa. Propaganda hazitafua dafu mbele ya virungu. Kaburu kashindwa sembuse nyie. Ulaya wana double standard ambazo hazitusumbui hata kidogo. Rwanda, Uganda, Gaza, Kenya, Somalia, Ethiopia, msumbiji kote huko wanafanya tofauti kulingana na maslahi yao.

Shida zipo lakini sio kivileee
 
Uhuru mnataka wa kuumiza wasiounga mkono serekali? Huo uhuru wa kuburuza wengine haupo. Na ikitokea hao wazungu wakaja kuvamia hapa nchini tutawaunga mkono hadi tupate mabadiliko. Uhuru maana yake sio kwa ajili ya kulinda utashi wa viongozi.
 
Jiulize kwanini yeye kati ya raia 63M? Sio kwamba Tanzania tuna utulivu kwa bahati mbaya tu, na usidhani kuwa hatujaribiwi na usifikirie kuwa hatuna vibaraka. Taasisi za usalama ziko macho sana, hata shindano wanaiona.
 
Uhuru wenyewe kama wa wanyapori, mwenye nguvu kumla mdogo
 
Huna akili kweli wewe... Tushachelewa
 
Ukiweza kujitegemea ndio unakuwa na maamuzi/kauli. Bajeti yenyewe asilimia 60/70 ni misaada kutoka kwa mabepari, achana na hizo chanjo na misaada miingine wakichomoa nyaya utaweza kufunga mkanda? Boss hanuniwi mbwa wewe
Kumbe Boss hanuniwi ???!
Duh 🙄 ! Nilikuwa siijui hii principal 🤣 !
 
Jiulize kwanini yeye kati ya raia 63M? Sio kwamba Tanzania tuna utulivu kwa bahati mbaya tu, na usidhani kuwa hatujaribiwi na usifikirie kuwa hatuna vibaraka. Taasisi za usalama ziko macho sana, hata shindano wanaiona.
Secret branch ya Wakoloni tulipochukua uhuru ikafanywa kuwa ndio usalama wa taifa wakajazwa vijana wa TANU ambao ndio Leo CCM.

Usalama wa taifa ni usalama wa CCM madarakani.

Kwahiyo hizo porojo zako ni za uongo za kujustfy mauaji utekaji na kupoteza wananchi kupiga mapadri kupiga wapinzani ili CCM iendelee kushika Dola kwa nguvu.

Kama yamewashindeni futeni mfumo wa vyama vyingi kuliko kuuwa kupiga na kupoteza Wananchi.
 
Yani wewe huijui vizuri tz na watanzania. Tz sio Lissu na wenzake. Kama Lissu na wenzake wangekuwa wanawakilisha mawazo ya watanzania waliowengi hali ya nchi isingekuwa hivi ilivyo Sasa. Vurugu hizo hata polisi wasingefua dafu. Shida ni kwamba anaongea ya kwake tu.
 
Uhuru upi unaongelea wewe.

Barabara zote za kuungani mikoa zimejengwa kwa misaada na mikopo na wala si hela za ndani.

Mradi wa reli ya SGR ni fedha za misaada mikopo.

Bandari zimewekwa rehani.

Bajeti ya nchi inafadhiliwa na mataifa ya nje.

Juzi tu hapo tumekopa bilioni 400 kwa ajili ya kujenga hospitali itakayokuwa mbadala wa MNH na badala yake zile pesa zimeelekezwa Zanzibar.

Madini wachimbaji wakubwa ni kutoka nchi za mataifa ya nje, gesi hatuna umiliki wake.

Hiyo nguvu ya kudai ni nchi huru umeitoa wapi? Labda uhuru unaongelea ni kuvuta pumzi na kujamba kila unavyojisikia.
 
Duh 🙄 !
 
Siku 20 tu wakigoma mikopo yao ya budget....Jeshi linaingia mtaani kupora na kuiba nchi inakuwa imeshajifia Rais atakimbia kujificha.....nchi masikini haiwezi kuwa msimamo milele Amina.....alie hapo magogoni anajua vizurisanaaaa
 
kodi zinakusanywa na kupeplekwa kusikojulikana na wasiojulikana....kazi bure.
 
Kodi peke yake hatutoboi. Fikiria kodi zikusanywe kisha wale kwa urefu wa kamba humo humo kuna kitu kitabaki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…