Heri Udikteta Kuliko Maigizo ya Demokrasia

Kwahio sababu hakuna cha maana kilichofanyika kwa kutokufuja pesa basi ni halali kwa hawa wafuje pesa ?

Hivi umevuta pumzi hata dakika mbili ku-observe implication ya unachosema ? Ukiwa Kiongozi mfujaji na watu wanaona kwamba wewe unafuja utawakemea vipi wengine wakifanya unachofanya...
Pesa ipi inafujwa?
 
Tukumbushane tu...,

Sisemi kwamba hili linatokea Sasa lakini Kutumika kwa Rasilimali Fedha na Muda kwenye Maigizo ya Demokrasia au Kutumia Pesa kwa Propaganda, ni bora Muda na Pesa hizo zikatumika kuleta maendeleo kwa Wananchi wanaojua Demokrasia haipo (Maigizo yana Gharama isiyo na Tija, Hususan pale yule unayemuigizia anajua ni Maigizo)

He is not deceived who knows himself to be deceived.​

Tatizo ni kwamba nchi kama Tanzania wananchi kana nyie ndiyo tatizo. Hatuna demokrasia kwasababu watu ni wavivu kudai haki zao watu wanaiba kura waziwazi tumenyamaza tu wengine, watu tunazuiwa kufanya mikutano tumenyamaza tu, watu tunapelekewa mizegwe kwenye uundaji wa katiba tunasubiria Chadema pekee! Demokrasia haiji kwa kukaa na kusubiria na kuweka uvivu mbele na woga wa kitoto ni kupigania. Watu tukidai serious katiba nzuri kwa maendeleo yetu tutapata mapema sana. Kama unataka udikteta wa kiongozi kukaa maisha yote na kumpa mtoto wake uongozi basi haututakii mema kama nchi. Tuna mifano ya Uganda na Rwanda nchi ni biashara ya familia.

Badala ya kulalama jiulize wewe binafsi unafanya nini kuleta demokrasia. Na unavyoandika unasaidia sisi kupata maendeleo au unacheza ngoma za watawala wa sasa kwamba mfumo ubaki kama ulivyo. Inawezekana unawasaidia hao hao ambao wewe unafikiri ni tatizo
 
Tukumbushane tu...,

Sisemi kwamba hili linatokea Sasa lakini Kutumika kwa Rasilimali Fedha na Muda kwenye Maigizo ya Demokrasia au Kutumia Pesa kwa Propaganda, ni bora Muda na Pesa hizo zikatumika kuleta maendeleo kwa Wananchi wanaojua Demokrasia haipo (Maigizo yana Gharama isiyo na Tija, Hususan pale yule unayemuigizia anajua ni Maigizo)

He is not deceived who knows himself to be deceived.​
Awamu ya 5 😂😂
Screenshot_20231006-174419.jpg
 
Tukumbushane tu...,

Sisemi kwamba hili linatokea Sasa lakini Kutumika kwa Rasilimali Fedha na Muda kwenye Maigizo ya Demokrasia au Kutumia Pesa kwa Propaganda, ni bora Muda na Pesa hizo zikatumika kuleta maendeleo kwa Wananchi wanaojua Demokrasia haipo (Maigizo yana Gharama isiyo na Tija, Hususan pale yule unayemuigizia anajua ni Maigizo)

He is not deceived who knows himself to be deceived.​
afadhali tamthilia na riwaya kuliko movie za kivita
 
Tatizo ni kwamba nchi kama Tanzania wananchi kana nyie ndiyo tatizo. Hatuna demokrasia kwasababu watu ni wavivu kudai haki zao watu wanaiba kura waziwazi tumenyamaza tu
Hao watu wanaoamka asubuhi na kulima na ku-toil kuweka mkate mezani siwezi kuwalaumu sababu at least wanafanya kazi yao na wengi wao ndio wanatulisha mimi na wewe..., sasa hao wengine ambao siasa ni kazi yao na hawaaminiki, flip-floppers ambao hawajaweza kumfikia huyu mkulima kwa aina moja au nyingine hao ndio wa kulaumu if anybody..., lakini kwa jicho la Siasa za sasa hata wao wakiingia ni mwendo wa mtumbo yao na kila mtu kivyake kinakachobadilika au kitakachobadilika sehemu nyingi ni chupa tu ila mvinyo ni ule-ule...., Hususan kwa nchi kama hii hata vyama huwezi kutengesha itikadi zao zaidi ya kuwa platform ya kupata kura ili kwenda kula....
wengine, watu tunazuiwa kufanya mikutano tumenyamaza tu,
Msinyamaze, na kama mnachoongea kina tija nyie ongeeni tu ukweli una tabia ya kujitenga na uongo

1696603299091.png

Ingawa tunapoelekea wala hakutahitajika mwanasiasa kuwaamsha watu..., ni kwamba mapinduzi yatatokea from bottom up sababu tunapoelekea ni pabaya ingawa tatizo la kutoka kwenye reli huenda kurudi ikachukua millenia na millenia kukaa tena sawa..., ndio maana nasema upuuzi wa sasa unaharibu kazi nzuri iliyofanywa na waasisi na itali-cost taifa big time....

watu tunapelekewa mizegwe kwenye uundaji wa katiba tunasubiria Chadema pekee! Demokrasia haiji kwa kukaa na kusubiria na kuweka uvivu mbele na woga wa kitoto ni kupigania. Watu tukidai serious katiba nzuri kwa maendeleo yetu tutapata mapema sana.
Wewe unaona Katiba ni be it end all mimi nakwambia Katiba hata ikitungwa na Malaika kwa watu / nchi na utamaduni wa kutofuata sheria hata sheria mama nyingine ikija haitafuatwa..., vilevile watu ambao ni uninformed na easily swayed by propaganda ukiwapa waislamu mahama ya kadhi, wasabato ijumaa siku ya kupumzika n.k. hata ukiwachanganyia madudu mengi amini nakwambia madudu hayo watayapisha kwa asilimia 100% Thus hata kabla katika haijafika au hii ya viraka kuwepo ni mangapi tunayavunja na yapo kisheria ?
Kama unataka udikteta wa kiongozi kukaa maisha yote na kumpa mtoto wake uongozi basi haututakii mema kama nchi. Tuna mifano ya Uganda na Rwanda nchi ni biashara ya familia.
Uongozi wa kweli wala sio raha na furaha bali ni karaha na utumishi.., ila since watu mmeshaona uongozi ni sehemu ya kupata kura kwenda kula na sio kufanya changes according to your ideologies ndio maana mnaona kwamba wakati wangu na mimi ufike na mimi nikapige / nikale..., lakini ingekuwa kiongozi anaweza kuwajibishwa instantly sababu hafuati kilichowekwa pangwa ili kifanyike kutokana na informed citizens kumwambia hapa hii sio sawa ni hapo tu ndio kungekuwa na Real Power to the People (sababu people could continually decide) na sio kusubiri miaka mitano kwenye tena kufanya betting ya huenda huyu ni bora kuliko yule.....
Badala ya kulalama jiulize wewe binafsi unafanya nini kuleta demokrasia. Na unavyoandika unasaidia sisi kupata maendeleo au unacheza ngoma za watawala wa sasa kwamba mfumo ubaki kama ulivyo. Inawezekana unawasaidia hao hao ambao wewe unafikiri ni tatizo
Kwa mimi kufanya ninachofanya kwa mtizamo wangu ni haki yangu nasema ninachokisema wakati wa my free time na kuendelea na kuwajibika kwa ninachofanya wakati mwingine..., hayo ya kutokuwa na changes waambia ambao ni wanasiasa na wanachukua ruzuku to excel the changes na sio kumlaumu yule anayewawezesha kwa his/her hard earned cash wafanye wanachotakiwa kufanya if at all huyo so called mkulima has done his / her part....
 
afadhali tamthilia na riwaya kuliko movie za kivita
Udikteta ni Vita ?

Sasa kwa taarifa yako maigizo ni hata wakati mnapigwa mabomu mnaambiwa hayo sio mabomu ni baraka, tena wale wanaowapiga mabomu ndio wanataka kuondoa demokrasia yenu (In short sioni tija ya Maigizo tena iwapo yule anayeigiziwa anajua kwamba hayo ni maigizo)
 
mie sitaki tamthilia na movie za kufia kwenye sandarusi kimyakimya na kutupwa baharini na kupotea kusikojulikana
 
Hakuna anayetaka hayo yatokee hayo hayafai kabisa kwa Binadamu ya aina yoyote.., Huo ni Unyama..., Sasa ni kuulize vipi hayo yanatokea alafu unafunikwa na mwanvuli wa Demokrasia kwamba hayo hayatokei and all is good ? Yaani unazabwa kibao alafu unalazimishwa kwamba hio ni busu...
 
Hupendi vip tena akati hiyo ndio identity ya aina ya uongozi unaupigia upatu?

kwenye unachopendekeze huo sio unyama ni kutuliza joto la kisiasa na kuimarisha dollar mamlakani.

Hiyo ni hali ya kupruni na kusawazisha vimbelembele kwahiyo huo sio unyama hata.

na hiyo tamthilia mimi hapana kabisa
 
Ndicho kipindi Wabunge wengi wa Upinzani waliingia Bungeni kuliko kipindi chochote tokea tupate Uhuru.

Huyu Mama kafanya nini so far zaidi ya kuzalisha Machawa?.
Sema na wewe una shida, ko unataka SSH afanyaje wapinzani waingie bungeni? Mana hata uchaguzi hakuna, ila am sure 2025 watarudi wengi hususani wale meza kuu wa upinzani
 
Hupendi vip tena akati hiyo ndio identity ya aina ya uongozi unaupigia upatu?

kwenye unachopendekeze huo sio unyama ni kutuliza joto la kisiasa na kuimarisha dollar mamlakani.

Hiyo ni hali ya kupruni na kusawazisha vimbelembele kwahiyo huo sio unyama hata.

na hiyo tamthilia mimi hapana kabisa
Unajua maana ya Dictatorship ? Ungejua hayo ungefahamu sasa hivi kinachofanyika ni Dictatorship kwa Kujivika kanzu ya Demokrasia..., Since hauna say (realistically) na maamuzi wanaamua genge la wachache wenye absolute power hio ndio definition ya dictatorship to put it mildly...,

Hayo ya kuua watu sila lazima yawepo kwenye Dictatorship na yanaweza kufanyika kwenye any so called Democracy..., tena yanaweza kufanyika legally kabisa kwa baraka za kila mtu kujua na kushangilia...., After all Argumentum ad populum...., Ndio maana kuna kipindi watu weusi Marekani Kuwa-lynched au mtu kumiliki Binadamu mwenzake kama mtumwa ilikuwa order of the day (as many thought it to be good and sound) na hata hilo lingepigiwa kura lingepeta kwa majority of votes...
 
unataka SSH afanyaje wapinzani waingie bungeni?
Samia yeye atengeneze mazingira ya usawa halafu CHADEMA tukizoa 45% ya Viti tutengeneze Serikali ya mseto.

Mambo ya Winner takes all ni ya kizamani sana.
 
Tukumbushane tu...,

Sisemi kwamba hili linatokea Sasa lakini Kutumika kwa Rasilimali Fedha na Muda kwenye Maigizo ya Demokrasia au Kutumia Pesa kwa Propaganda, ni bora Muda na Pesa hizo zikatumika kuleta maendeleo kwa Wananchi wanaojua Demokrasia haipo (Maigizo yana Gharama isiyo na Tija, Hususan pale yule unayemuigizia anajua ni Maigizo)

He is not deceived who knows himself to be deceived.​
Labda kama hujui maana ya maendeleo sawa. Maendeleo ni pa.ona ni kupigwa siasa kila Kona ili mzunguko wa pesa uwe mzuri. Kumbu kwa mfano kama chadema wakienda kufanya mikutano let say Mwanza, watalala hoteli na huko lazima wale, walale, wanywe nk hivyo mwenye hotel atapata pesa na ataajiri watu wengi ili hiduma iwepo masaa yote, kumbuka ambao hawana ajira wakiingia kwenye siasa tayari wamepata ajira, mfano mbowe bila siasa haajiriki popote.
 
Naomba nijibu haya maswali ....

Kwanini CHADEMA ipo na CCM ipo ?,

Nini faida kubwa ya Vyama zaidi ya kuunganisha watu wenye mawazo sawa ili sauti zao na mitizamo yao kuwa na nguvu na kupigania kile wanachokiamini ? Kama kuna tofauti ya Kiitikadi / Mitizamo baina ya hivi vyama watakapounda Serikali moja itasimamia itikadi zipi ? Kama hakuna tofauti baina yao ni nini faida ya kuwa navyo hivi vyama in the first place; kwanini wote wasiwe wamoja from the get go ?

Kwahio baada ya kuungana Chadema itasaidia kutekeleza Ilani ya CCM hata kama wanaona CCM maono yao ni ndivyo sivyo, (ukizingatia kama nchi hatuma Master Plan na kila anayeingia anatekeleza anavyoona yeye au wanavyoona wao na genge lao....)
 
Labda kama hujui maana ya maendeleo sawa. Maendeleo ni pa.ona ni kupigwa siasa kila Kona ili mzunguko wa pesa uwe mzuri. Kumbu kwa mfano kama chadema wakienda kufanya mikutano let say Mwanza, watalala hoteli na huko lazima wale, walale, wanywe nk hivyo mwenye hotel atapata pesa na ataajiri watu wengi ili hiduma iwepo masaa yote, kumbuka ambao hawana ajira wakiingia kwenye siasa tayari wamepata ajira, mfano mbowe bila siasa haajiriki popote.
Unajua pesa za kuajiri hao kama hawana Tija ni nani anazilipa ? Kwa logic yako kwanini na wewe kwako usiajiri wafanyakazi hata mia moja ili ulete maendeleo nyumbani kwako.... Hizi ndio fallacy za Keynes katika mfano wake kwamba unaweza kuamua tu kuchimba mashimo kwenye barabara alafu ukaajiri watu wayazibe na kwa kufanya hivyo umeongeza ajira hence uchumi (The Broken Window Fallacy)
 
Tukumbushane tu...,

Sisemi kwamba hili linatokea Sasa lakini Kutumika kwa Rasilimali Fedha na Muda kwenye Maigizo ya Demokrasia au Kutumia Pesa kwa Propaganda, ni bora Muda na Pesa hizo zikatumika kuleta maendeleo kwa Wananchi wanaojua Demokrasia haipo (Maigizo yana Gharama isiyo na Tija, Hususan pale yule unayemuigizia anajua ni Maigizo)

He is not deceived who knows himself to be deceived.​
Umejizima data, unataka uishi kama mfugo kwenye zizi. Kama Mtanzania unaweza kweli kutamani udikteta wa mtu mmoja kama Museveni au Kagame basi wewe ni maiti inayotembea.

Siifagilii CCM kihivyo lakini hata kama inaiba kura za wapinzani lakini angalao tumeona marais 5 wakibadilika toka 1986 wakati Uganda bado ina Museveni peke yake.

Imagine Tanzania ingekuwaje na UDIKTETA wa Magufuli leo hii? Ile miaka 5 tu ya uhai wake tulikuwa hatuongei, hatutoi maoni kumuogopa yeye. Magufuli aliamua achukue hela ya mtu yeyote na afanyeqnachotaka yeye. Magufuli alikuwa anaua yeyote anayemkosoa. Na Mungu aligundua kuwa UDIKTEA wa Magufuli siyo mzuri kwa Tamzania ndiyo maana akamtoa mapema mwaka 2021 kabla hajaharibu nchi yetu.

Hii demokrasia yetu hata kama CCM iko peke yake kwa miaka 62 sasa lakini wanachukua sana maoni na ukosoaji wa upinzani hata kama hawawezi kukiri kwa mdomo
 
Nadhani ni Makosa yangu ku-over-estimate uelewa wa watu kama wewe lakini ni tabia yangu kutumia maneno machache as possible sina kipaji kama cha Pascal Mayalla Kutumia maneno Ishirini iwapo neno moja litatosha kuelezea (ninajali muda wa watu kusoma magazeti) Thus let me break it down really slow...., Hakuna mtu ambaye hapendi Demokrasia (Really Power to the People) lakini kinachotokea ni Maigizo hata Museveni na Kagame aliyekwambia kwao hawana Demokrasia ni nani (by their defition) ? On paper watakwambia wao ni a Democracy ila ukweli ni kwamba ni maigizo ya Demokrasia..., Sasa kwa akili yako ni bora waendeleze gharama na kupoteza muda kuleta ulaghai huo au ni Heri hizo gharama waache kupoteza na ku-call a Spade a Spade...
Siifagilii CCM kihivyo lakini hata kama inaiba kura za wapinzani lakini angalao tumeona marais 5 wakibadilika toka 1986 wakati Uganda bado ina Museveni peke yake.
Hivi kwanza aliyekwambia hata kwa wale ambao Kura kweli zinahesabiwa na haziibiwi Mwananchi ndio anachagua Rais ni nani ? Hata kule America ni kwamba Those who nominate are the one who chooses..., unachaguliwa baina ya A na B ndio uchague hata kama ulikuwa unapenda C wewe hauna choice hio, unaweza kuletewa wabaya wawili na uchague kati ya hao..., Mfano hata sasa hivi Wabunge wa CCM ambao eventually ndio wanachukua jimbo (wengi) ni wewe ndio unachagua au wajumbe ndio wanakuchagulia ... (Those who Nominates are the ones who Chooses)
Imagine Tanzania ingekuwaje na UDIKTETA wa Magufuli leo hii? Ile miaka 5 tu ya uhai wake tulikuwa hatuongei, hatutoi maoni kumuogopa yeye. Magufuli aliamua achukue hela ya mtu yeyote na afanyeqnachotaka yeye. Magufuli alikuwa anaua yeyote anayemkosoa. Na Mungu aligundua kuwa UDIKTEA wa Magufuli siyo mzuri kwa Tamzania ndiyo maana akamtoa mapema mwaka 2021 kabla hajaharibu nchi yetu.
Aliyekwambia Dikteta lazima aue ni nani na aliyekwambia kwenye Maigizo ya Demokrasia watu hawaui ni nani, Theoretically hata Uganda, Rwanda na JPM ilikuwa Demokrasia..., lakini ukweli yalikuwa maigizo sasa swali linakuja gharama za hayo maigizo (hata Bongo movie zina bajeti tofauti tofauti, je sasa hii movie Bajeti, yake ipo vipi)....;

Unajua uzuri wa Demokrasia hata kama ikiwa ni illusion kama wale ambao wanadanganywa wanaamini basi wanaridhika kwamba ni wao ndio wana maamuzi hence hawawezi kufanya fujo (peace) sasa iwapo uongo huo hata wanaodanganywa wanajua kwamba ni uongo it does not serve the purpose....
Hii demokrasia yetu hata kama CCM iko peke yake kwa miaka 62 sasa lakini wanachukua sana maoni na ukosoaji wa upinzani hata kama hawawezi kukiri kwa mdomo
Kwahio kwa unachosema hata kama ni Dikteta ambaye ni Benevolent na anachukua maoni ya watu na kuwasikiliza basi ni safi ? Sasa kuliko CCM kuwa na hayo Maigizo kwamba yoyote anaweza kufanya chochote / kushiriki uongozi alafu hawafanyi ni nini faida ya haya maigizo ambayo yanatumia pesa (kwanini wasiseme ukweli tu ambao unajulikana au wapunguze bajeti ya hizi movies)

Unaweza kuniuliza if what is available is not fit for purpose what is ? Is it Practically possible to have a Democracy which people are Really in Power ? Theoretically and with Current Technology my answer is Yes...

Nadhani ni Makosa yangu ku-over-estimate uelewa wa watu kama wewe lakini ni tabia yangu kutumia maneno machache as possible sina kipaji kama cha Pascal Mayalla Kutumia maneno Ishirini iwapo neno moja litatosha kuelezea (ninajali muda wa watu kusoma magazeti) Thus let me break it down really slow...., Hakuna mtu ambaye hapendi Demokrasia (Really Power to the People) lakini kinachotokea ni Maigizo hata Museveni na Kagame aliyekwambia Uganda sio Demokrasia ni nini ? On paper watakwambia wao ni a Democracy ila ukweli ni kwamba ni maigizo ya Demokrasia..., Sasa kwa akili yako ni bora waendeleze gharama na kupoteza muda kuleta ulaghai huo au ni Heri hizo gharama waache kupoteza na ku-call a Spade a Spade...

Hivi kwanza aliyekwambia hata kwa wale ambao Kura kweli zinahesabiwa na haziibiwi Mwananchi ndio anachagua Rais ni nani ? Hata kule America ni kwamba Those who nominate are the one who chooses..., unachaguliwa baina ya A na B ndio uchague hata kama ulikuwa unapenda C wewe hauna choice hio, unaweza kuletewa wabaya wawili na uchague kati ya hao..., Mfano hata sasa hivi Wabunge wa CCM ambao eventually ndio wanachukua jimbo (wengi) ni wewe ndio unachagua au wajumbe ndio wanakuchagulia ... (Those who Nominates are the ones who Chooses)

Aliyekwambia Dikteta lazima aue ni nani na aliyekwambia kwenye Maigizo ya Demokrasia watu hawaui ni nani, Theoretically hata Uganda, Rwanda na JPM ilikuwa Demokrasia..., lakini ukweli yalikuwa maigizo sasa swali linakuja gharama za hayo maigizo (hata Bongo movie zina bajeti tofauti tofauti, je sasa hii movie Bajeti, yake ipo vipi)....;

Unajua uzuri wa Demokrasia hata kama ikiwa ni illusion kama wale ambao wanadanganywa wanaamini basi wanaridhika kwamba ni wao ndio wana maamuzi hence hawawezi kufanya fujo (peace) sasa iwapo uongo huo hata wanaodanganywa wanajua kwamba ni uongo it does not serve the purpose....

Kwahio kwa unachosema hata kama ni Dikteta ambaye ni Benevolent na anachukua maoni ya watu na kuwasikiliza basi ni safi ? Sasa kuliko CCM kuwa na hayo Maigizo kwamba yoyote anaweza kufanya chochote / kushiriki uongozi alafu hawafanyi ni nini faida ya haya maigizo ambayo yanatumia pesa (kwanini wasiseme ukweli tu ambao unajulikana au wapunguze bajeti ya hizi movies)

Unaweza kuniuliza if what is available is not fit for purpose what is ? Is it Practically possible to have a Democracy which people are Really in Power ? Theoretically and with Current Technology my answer is Yes...

Umenijibu vizuri sana bila mhemuko wala jazba, asante. Ila point yangu ni moja tu kuwa na sisi hii demokrasia ya kubadili Rais kila baada ya miaka 10 ni bora kuliko hao waliokaa miaka 40.

Pili hata kama upinzani hawajapata fursa ya kuingia madarakani lakini wanayo FORUM ya kukosoa through uwakilishi bungeni na mikutano ya hadhara.

Kuhusu gharama ni kwamba hakuna mfumo wa siasa usio na gharama. Hata hao ambao ni MADIKTETA kama walivyokuwa akina Muammar Gaddafi au Mobutu Seseseko walikuwa na gharama za kuziweka tawala zao madarakani. Gharama haziepukiki
 
Unajua pesa za kuajiri hao kama hawana Tija ni nani anazilipa ? Kwa logic yako kwanini na wewe kwako usiajiri wafanyakazi hata mia moja ili ulete maendeleo nyumbani kwako.... Hizi ndio fallacy za Keynes katika mfano wake kwamba unaweza kuamua tu kuchimba mashimo kwenye barabara alafu ukaajiri watu wayazibe na kwa kufanya hivyo umeongeza ajira hence uchumi (The Broken Window Fallacy)
Uchumi ni purchasing power na huwezi kuwa na purchasing power kama hakuna Aggregate demand ambayo inapatika kwa kukuza ajira kwa njia yoyote. Ukiona rais ambaye anabana pesa kama kipindi Cha jpm wanaoumia ni wanachi. Ikifanya siasa ishamili ni ajira hiyo kuliko kuanzisha vimiradi ambavyo unasababisha Capital draining mana wanaofanya kazi ni wachina au wengine ambao wanapeleka pesa kwao kama remitancies
 
Siasa, Wanasiasa, utitiri wa vyama wanazalisha nini, zaidi ya ku-drain our coffers kwa ruzuku ? Unaweza kusema ni a necessary cost.., lakini huwezi kuanzisha vyama vya Siasa kama njia ya mapato unaanzisha kama Matumizi ambayo ni ya lazima....

Kwa logic yako unaweza kuambiwa uanzishe kiwanda au Chama kingine cha Siasa ili vijana wengi zaidi waingie kwenye haya malumbano ukasema uanzishe Chama ili watu wapate Ujira ? Hii ndio huwa naita kujiibia mfuko wa Suruali ili uweke kwenye mfuko wa Shati (Cutting your Nose to Spite your Face)...., Kwa Hitimisho.., huu mtizamo wako wa vyama vya Siasa kama chanzo cha ajira hence kukuza Uchumi nadhani haujalifikiria vema na unahitaji kurudi kwenye drawing board...
 
Back
Top Bottom