Hifadhi ya Taifa Kigosi yafutwa rasmi na kuwa msitu wa hifadhi ya Kigosi

Hifadhi ya Taifa Kigosi yafutwa rasmi na kuwa msitu wa hifadhi ya Kigosi

Death-of-President-Magufuli-likely-to-result-in-fraught-transition-process-renewal-of-power-st...png

Nimeanza kukumbuka Mzee lala unono.
 
Kampuni ilipewa kibali 2005,jakaya anahusika vipi!?..Tena 2009 akatunga sheria ya kuibana kampuni hiyo shughuli zake zisiwe halali,kwa nini hukusema kampuni ililetwa na mkapa ukamrukia jakaya!?
Nineza kuwa nimekosea kidogo tena kwa bahati mbaya ila wewe unaepotosha makusudi bila ushahidi WOWOTE nakushangaa sana au na wewe umeoa kwa Mchengerwa?
 

CCM wametumia mikakati (draft) ya kisingizio wananchi watanufaika hivyo kuiondoa Hifadhi ya Taifa ya Kigosi iwe chini ya Wakala wa Misitu na hivyo ni rahisi kufanya dili la dhahabu sababu kufanya uchimbaji katika Hifadhi ya Taifa (National Park) kisheria wanazuiwa.


July 10, 2023, 11:35 pm

WAHESHIMIWA WABUNGE WAKIONESHA SURA ZA MATUMAINI SUALA LA KIGOSI

img-20230710-wa0002-1024x768.jpg
Mbunge wa Jimbo la Ushetu (kushoto) Emmanuel Cherehani na mjumbe wa Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi Taifa Livingstone Lusinde (kulia). Picha na Sebastian Mnakaya
Serikali imegawa hifadhi ya Kigosi iliyopo katika halmashauri ya Ushetu takriban kilometa 7,000 kwa ajili ya wananchi kufanya shughuli mbalimbali

Na Sebastian Mnakaya

Wananchi wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga watanufaika na hifadhi ya Kigosi baada ya serikali kumega kilometa 7,000 ya eneo hilo kuwa chini ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ambapo wananchi wataruhusiwa kufanya shughuli za kimaendeleo.

Akizungumza katika sherehe za kumpomgeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Hassan katika kata ya Ulowa mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Livingstone Lusinde amesema jambo hilo limekuwa likizungumzwa mara kwa mara na mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani juu ya changamato la pori hilo hali iliyosababisha kubadilishiwa matumizi.

Sauti ya mjumbe wa halmashauri kuu chama cha mapinduzi Taifa Livingstone Lusinde
Kwa upande wake, mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani, amesema kabla ya serikali kumega eneo hilo kwa wananchi walikuwa hawaruhusiwi kufanya shughuli zozote za kimaendeleo, ambapo kwa sasa wataendelea na shughuli hizo bila ya kuwa na vikwazo vyovyote.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani
img-20230710-wa0020-1024x768.jpg
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akiwa na wananchi wa kijiji Cha Ulowa
Naye, makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Doa Limbo ameishukuru serikali kwa kutatua mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi, ambapo kwa sasa wananchi watanufaika na eneo hilo kwa shughuli za kimaendeleo.

Sauti ya makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Doa Limbo
Aidha diwani wa kata ya Ulowa Gabrela Kimaro amesema kuwa kwa kurudishwa pori hilo chini ya usimamizi wa TFS itasaidia wananchi wengi kujipatia kipato kwa kufanya shughuli za ufugaji na uvuvi.

Sauti ya Diwani wa kata ya Ulowa Gabrela Kimaro
Awali pori hilo lilikuwa chini ya Wakala wa Misitu Tanzania {TFS}, na mwaka 2019 likapandishwa hadhi kuwa chini ya usimamizi wa Hifadhi za Taifa Tanzania [TANAPA] ambapo hifadhi hiyo ilikuwa inazuia shughuli za kiuchumi kufanyika ndani ya pori hilo hali iliyosababisha mgogoro na wananchi wa eneo hilo.
Source : Wananchi halmashauri ya Ushetu kunufaika na hifadhi ya Kigosi – Kahama FM

 
Ecological suicide. TANAPA walikuwa wanaweza kudhibiti hawa wa Misitu ni walarushwa wakubwa
 
Kampuni ilipewa kibali 2005,jakaya anahusika vipi!?..Tena 2009 akatunga sheria ya kuibana kampuni hiyo shughuli zake zisiwe halali,kwa nini hukusema kampuni ililetwa na mkapa ukamrukia jakaya!?
Ilipewa leseni ya uchimbaji mwaka 2013.

Kuwa objective, usikae hapa kumtetea mtu.

Soma habari kwa utulivu.

Pia usiwaze kwamba watu wapo hapa kusingizia wengine.

Unapewa evidence unazidi kubadilisha hoja tu.
 
Nineza kuwa nimekosea kidogo tena kwa bahati mbaya ila wewe unaepotosha makusudi bila ushahidi WOWOTE nakushangaa sana au na wewe umeoa kwa Mchengerwa?
Hujakosea kidogo,umekosea pakubwa kumsingizia mtu wizi,Sasa Kama Hilo pori limefutwa kuwa hifadhi na kurudisha TFS..ndiyo tayari kauziwa mwarabu!?
 
huu uongo mwingine wa 21% hebu muwe na jicho la pili la kufanya analysis. Hebu piga hesabu ya idadi ya wafanyakazi 21% ya wanaoajiriwa, halafu upige na hesabu ya wazanzibari wanaotoka vyuo ulete mrejesho hapa kama vinawiana.​


bitimkongwe, nashindwa kabisa kuwaelewa baadhi yenu nyie Watanzania wenzetu...je ni kitu gani hasa kinachowasukuma kutetea hata yale yasiyohitaji utetezi.

Kwenye fursa za ajira mtu na akili zako timamu unaanzia wapi kutetea hata lile wazo tu la Wazanzibari kupewa asilimia 21% ya idadi ya watumishi ndani ya Muunganno?

Zanzibar ina idadi ya wakaazi wasiofikia hata milioni mbili sawa na asilimia 3% ya Watanzania wote...sasa hiyo asilimia 21% ni kwa misingi ipi? Unaanzia wapi?
 
Ilipewa leseni ya uchimbaji mwaka 2013.

Kuwa objective, usikae hapa kumtetea mtu.

Soma habari kwa utulivu.

Pia usiwaze kwamba watu wapo hapa kusingizia wengine.

Unapewa evidence unazidi kubadilisha hoja tu.
Hiyo kampuni ipo humo tangu 2005 kabla ya sheria ya 2009 kutungwa,2005 nani alikua rais!?..maana uchaguzi ulipelekwa mbele baada ya kido Cha mgombea mwenzao wa chadema,usitake kuuruka mwaka 2005 na hiyo kampuni!
 
Ccm Na Sarakasi Zao Na Ukweli Waarabu Watatupa Shida Sana Mno
 
08 May 2022

FILAMU YA ROYAL TOUR YAANZA KULETA MATUNDA HIFADHI YA KIGOSI



View: https://m.youtube.com/watch?v=LsVvmEj8-_I

GEITA Uzinduzi wa Filamu ya Royal tour umeanza kuzaa matunda hapa nchini baada ya kundi la watalii wa ndani kutoka katika taasisi za elimu kuhamasika na kutembelea hifadhi ya taifa ya Kigosi kwa mara ya kwanza tangu ianzishwe ili kujionea vivutio mbalimbali na malikale zilizopo katika eneo hilo ikiwemo kanisa la kwanza la wamisionari lilijengwa mwaka 1891.

Hifadhi ya taifa ya Kigosi ilianzishwa mwaka 2019 ambapo awali ilikuwa inajulikana kama ni pori la akiba kigosi Moyowosi ambayo inaukubwa wa kilomita za mraba 7000 ambayo inapakana na mikoa ya Kigoma,Tabora na Shinyanga na Geita.

Uzinduzi wa filamu ya Royal Tour uliofanyika hivi karibuni hapa nchini umetajwa kuhamasisha baadhi ya watalii wa ndani kutembelea hifadhi hii mpya ili kujifunza historia za malikale na vivutio vinavyopatikana ndani ya hifadhi kama anavyosimulia James Nahonyo mhifadhi mkuu wa hifadhi hiyo.

Scolastika Divai na Samwel Mwarabu ni watalii wa ndani kutoka shule ya sekondari Nyihongo ya wilayani Kahama wanaelezea dhima ya kuunga mkono Rais Samia katika Filamu ya Royal Tour huku Mkoba Kihata akielezea aina ya vivutio vinavyopatika katika eneo hilo
 
Na Mkwe anasema "Online Republics" tuache kuongea na kuitomasatomasa Serikali ndio huku?
 
Duuh!!!
Huu uzi ni noma.
Watu mnashusha habari nyeti mkiombwa source mnatupia papo kwa papo.
Nadhani mwenye dhamana anajilaumu sasa kwa kumtumbua mkurugenzi wa kitengo nyeti.
 
TFS haina uwezo wa kudhibiti kama TAWA na TANAPA. hilo pori ni bye bye kwasababu ya Rushwa.
 
Back
Top Bottom