Hata mimi niliisoma asubuhi hii ndiyo nikaona Zelensky regime akili zao fyatu sana wala mtu husije ukadanganyika kirahisi kwamba wanajeshi wa Ukraine wamejitolea kumwaga damu yao ili kuilinda Continetal Europe
na possibly USA dhidi ya
jeshi la Russia,ukweli wa mambo lengo la Zelensky na wapambe wenzake wanatafuta njia mbadala ya kujiunga na NATO on a fast track~wataizuga NATO/US kwa kusema kwamba kuwa jeshi la Ukraine linamwaga damu nyingi sana kutimiza malengo/kwa niaba ya NATO dhidi ya Urusi.
Hivyo kwa akilï za Senselessky na wapambe wake wanajiona wana haki ya kujiunga na NATO
Kwa kuwa WAUkraine wanakufa kwa wïngikwa niaba ya malengo ya NATO yenyewe dhidi ya Urusi
Ulichoandika hapa ni wendawazimu.
Russia na Ukraine miaka ya 1990s ilisaini mkataba uliosimamiwa na kufadhiliwa na Marekani. Ukraine ikakubali kuharibu silaha zake za nyuklia, silos, warheads, bunkers na missiles. Russia ikakubali haitoivamia Ukraine ila Ukraine isiingie NATO.
Mwaka 2014 Russia ikavamia Ukraine kinyume na makubaliano na Ukraine ikaacha kupambana. Mwaka huohuo Russia ikadhamini makundi ya Donetsk na Luhansk kujitenga, Ukraine ikaacha. After that Ukraine ikachukua mafunzo na silaha kutoka Ulaya.
February 2022 Russia ikavamia Ukraine. Ukraine ikapambana mpaka leo. Bado anatokea muuza mitumba mmoja kutoka kwenye vibanda uko anakwambia "ninaona Zelensky regime akili zao fyatu"
Sasa ni hivi, akili zao fyatu au sio fyatu Ukrainians wameamua kupigana. Hawakudai, hawajakuita ni kiherehere chako mwenyewe, hujaombwa msaada wala kuhitajika kwenda vitani, hukatwi kodi kuwasaidia vita. Na wala hujaombwa maoni kwenye mapigano yao. Wao ndio wanajua wanachotaka, sio wewe. Wewe sio chochote wala sio lolote kwao, kwanza hawajui kama upo. Wanachojua ni bunge lao, serikali, mahakama, jeshi, taasisi zao na washirika wao.
Jina lako la Kihaya, Nyerere aliyepambana na Iddi Amin alipovamia Kagera salient ni mwendawazimu? Mfano nikivamia nyumbani kwako nikawashambulia wanao utajitahidi "usiwe na akili fyatu" yani uniache nikimaliza niondoke?
Na issue ya Ukraine kujiunga NATO si ni ya 2022 baada ya Urusi kuvamia. Kwahiyo utetezi wako ni Urusi ilivamia February 2022, ili Ukraine isiombe kujiunga na NATO somewhere in May 2022 baada ya Urusi kuvamia? Sasa Urusi ilipovamia February justification ilikuwa ni nini.
Yani tuiweke hivi, Tanzanian ikianzisha sheria ya kuua wezi, nikaja nikakuua. Nikienda mahakamani nikajitetea kwamba nimekuua 2023 kwa sababu nina mpango wa kuacha mlango wazi mwaka 2024 na wewe utavamia na kuiba nakuwa sahihi? Justification ya mimi kukuua 2023 ni nini.
BTW Ukraine imeomba kujiunga NATO baada ya Russia kuvunja makubaliano ya mkataba walipovamia Crimea mwaka 2014, bado wakashiriki Donetsk na Luhansk, bado wakavamia 2022. Sasa hayo makubaliano ya nini kuheshimiwa wakati Russia kayavunja mara nne?