Hii chapati niliyotengeneza, usipokua makini utajing'ata Vidole

Na kingine napenda mwanaume anaejua kupika. Nikae ye anipikie siku moja moja.
 
Hii ilikuwa chapati yangu ya kwanza kutengeneza...



Hii ni baada ya kufundishwa....



Na bado nina imani nina a lot of room for development. Sikuwahi kudhani kama ningeweza kupika chapati, nilikuwa nachukulia ni mapishi magumu balaa....ila....
 
Sema ukipata mwanaume asiejua kupika raha hata umpikie nini ye anajionea sawa tuu. [emoji23][emoji23][emoji23]
Au asiejua kufua[emoji23] [emoji23] mi yan hiv vitu viwili naviangalia kwa makini sana.

Mwanaume nae anaeng'arisha nguo ukimfulia anaona kama hujatakatisha,atakwambia mbona hii kola hujasugua vizur,na humu kwapani hujatakatisha,utafubaisha shati langu.mamaaaae unataman umwambie fua mwenyww mbwa ww
 
Hiyo ya kwanza I bet ilitoka kama kaukau [emoji23][emoji23][emoji23]. Wewe unapenda kupika inaonekana
 
Mi natakaga kujua recipes na steps basi.

Sometimes ka video kanasaidia. Unakuta anakuambia kaanga vitunguu hadi viwe 'golden brown' sasa hapo golden brown labda kwenu wadada..mimi golden brown ni rangi nyingi mno.

Wakati mwingine recipe za kizungu zinasema;
- add a pinch of sugar
- add a dash of salt
- add a smidgen of cinnamon
- add a tad of cardamom

Hapo unaahirisha kupika, unapika zako ugali na tembele unalala.
 
Hapo kwenye kufua kwa kweli sina kazi napo sanaaa maana mi mwenyewe kufua siwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…