Hii collabo kati ya mtu mzima Jigga (Jay-Z) na Slim Shady (Eminem) Renegade nani aliua (verses kali)?

Eminem saluti mule ndani, katembea hatari japo Jigga naye kajitahidi sana sanaa...

Kimsingi usipoambiwa hiyo ngoma ni ya nani?! Utajua ni ya Eminem.
Mtu mzima jigga alifanywa kama mtoto
 
Mi naona monster ya em ft Rihanna ndo Kali zaidi aisee 🔥🔥
Zote kwangu ni kali as long as Rihanna yupo kunogesha ngoma ya hip hop ngoma hio ina asilimia kubwa mimi kuikubali ukianza hizo alizo shirikishwa na Eminem, Jay-Z, Kanye West, T.I ........ Rihanna yupo vizuri kwenye kuipa vibe ngoma ya Hip hop ni kama Commando hapa bongo
 
Ngoma kali nenda kaskilize wimbo wa Rosa ree ft Fid Q unaitwa (Trust) wamesampo bit ya hii Ngoma.

Na hiyo ngoma trust ya rosa ree Fidq kapita floo ya Eminem kwenye wimbo wa 50Cent (Dont push me) nenda kaskilize utaleta mrejesho hapa.

Renegade ni wimbo mkali na Eminame kafunika.
 
Niliwahi kuandika mahala, mtu pekee anaeweza kupiga collabo na eminem na asifunikwe vibaya ni Lil Wayne!

Lil Wayne ndio anajua namna ya kuhandle collabo za Slim Shaddy. Na siri pekee, ni kumuacha Shaddy afanye fujo zake, na wewe utulie, ufanye vile unafanyaga siku zote. Ila ukitaka kufunikana, basi Eminem atakufunika, then atakufunua mchana kweupe!

Sikiliza No love ya Eminem na Lil Wayne, kisha sikiliza Drop the world ya Lil Wayne ft Eminem. Utakubalina na mimi. Pia sikiliza Mr. Carter ya Lil Wayne na Jay Z, utakubali vile Lil Wayne anajua kucheza na hawa watabe!

Back to the topic, hata Jay Z mwenyewe anajua kwamba alifunikwa kwenye Renegade!
 
Kwenye Mr Carter Weezy ana verses 3 na Jay ana 1, so it's not fair kulinganisha. By the way Jay's verse was fire, in my opinion.
 
Kwenye Mr Carter Weezy ana verses 3 na Jay ana 1, so it's not fair kulinganisha. By the way Jay's verse was fire, in my opinion.
Ni verse mbili Chief, sio tatu. Labda kama umehesabu na intro. Verse ya Jay Z ilikua poa, ila kwa upande wangu naona Wayne alifanya poa zaidi.

By the way, hoja yangu ni ilikua kwamba Wayne anafanya poa sana kwenye collabo za wakubwa. Hata kama anafunikwa inakua sio kivile, inabaki kua debatable. Ni tofauti na collabo nyingine anazofanya Eminem, huwa anawaacha mbali sana wengine.

Kwenye Forever remix ya Drake, Kanye West alirudi kuandika upya verse yake baada ya kuisikia verse ya Eminem. Unyama ulikua mwingi mno!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Wayne ana verse tatu Mkuu. Cheki.
 
Kwa iyo no luv slim alifunikwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…