Hii daladala iliyotaka kuleta ajali msafara wa CDF iadhibiwe, haina adabu

kumbe kuandika vzur unajua mbona siku nyingne hua una tuchanganyia mambo
 
Kuna uwezekano gari ilifeli breki...halafu hii tabia ya kujichukulia sheria kwa wanajeshi nadhani ifikie kipindi ikomeshwe huyo derevan na konda walipaswa kupelekwa kwa mamlaka husika ili hatua za kisheria zifuate
 

..haya mambo ya misafara ni upumbavu ulioanza miaka ya karibuni.

..Ma-Cdf watangulizi kama Twalipo, Musuguri, Kiaro, walikuwa hawana misafara na bugudha kwa walipakodi wa Tz.

..Na Watanzania ni kama tumezoea kunyanyaswa na kudhalilishwa na viongozi wetu.

..kwa hiki ulichoandika ni kana kwamba dereva wa daladala kupokea kipigo ni jambo halali na stahiki yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…