Hii daladala iliyotaka kuleta ajali msafara wa CDF iadhibiwe, haina adabu

Hii daladala iliyotaka kuleta ajali msafara wa CDF iadhibiwe, haina adabu

..haya mambo ya misafara ni upumbavu ulioanza miaka ya karibuni.

..Ma-Cdf watangulizi kama Twalipo, Musuguri, Kiaro, walikuwa hawana misafara na bugudha kwa walipakodi wa Tz.

..Na Watanzania ni kama tumezoea kunyanyaswa na kudhalilishwa na viongozi wetu.

..kwa hiki ulichoandika ni kana kwamba dereva wa daladala kupokea kipigo ni jambo halali na stahiki yake.
Kumbuka enzi hizo barabara zilikuwa nyeupe! Sasa hivi bodaboda maelfu njoo daladala nazo ni hatari tupu. Sasa tukiachiwa tujiamlie tutapoteza viongozi kwa uzembe!
 
Kumbuka enzi hizo barabara zilikuwa nyeupe! Sasa hivi bodaboda maelfu njoo daladala nazo ni hatari tupu. Sasa tukiachiwa tujiamlie tutapoteza viongozi kwa uzembe!

..jiulize wewe unayetumia usafiri wa umma unawahi ktk majukumu na miadi yako, hawa vigogo wanaotumia vyombo vya serikali wanashindwaje mpaka iwalazimu kusumbua raia wema?

..enzi zetu waliokuwa na misafara ni Raisi, Makamu, Waziri Mkuu, na baadae waliongeza Katibu Mkuu wa Ccm.
 
Watu wanachoka jamani mtu mnasimamishwa saa nzima kumngojea mtu apite hii si haki.
Mbaya zaidi unaweza kuta msafara wa mkuu ulikuwa wrong side ya bara bara.. hawa viongozi saa nyingine wanaleta kero sana bara barabarani, wao ndio wenye haraka sisi raia hatuna haraka.
 
Kila nikimkumbuka CDF Francis Ogolla wa KDF naumia sana. Sasa huyu dereva asije akatupa huzuni nyingine hapa East Africa. Mungu amuepushe CDF Jacob Mkunda na mabalaa.
 
Aiseeee kuna mambo ambayo yakifanyika mpaka unaogopa, nipo maeneo ya Mbezi na askari wa MP wamewapigisha kwata dereva na konda wake. Kilichotokea inasikitisha sana na mpaka tumeshauri wakampime dereva kilevi.

Msafara wa CDF ulikuwa unapita lakini kabla ya kupita walisimama ma MP kadhaa kuzuia magari na kusafisha njia.

Sasa ndugu yetu huyu wa daladala ametokea Goba na speed anaenda Mbeza, Askari wa MP wakamsimamisha jamaa akahisi utani akawa anampelekea MP gari.

Jamaa kulinda pumzi akasogea pembeni huku anamsimamisha, yaani gari ya mwisho inapita kaipelekea juhudi za dereva wa msafara kuikwepa ilikuwa ajali ya kiajabu kabisa.

Naamini wameleekea mahali stahili baada ya kushusha abiria na adhabu watakayopata aisee iwe fundisho kwa magari yote kuheshimu misafara ya viongozi na hasa pale wanapopewa alama ya kusimama kupisha msafara.

Polen sana wote mliohusika Mungu azidi kulinda misafara yenu

Amen.

So far imepigwa simu dreva na MP wameelekea kurudi njia ya Goba bado na googlre wanapoelekea ila nawatakia pole huko waendako naamini MP watamfikiria zaidi konda ambae kihualisia ahusiki na yaliyotokea

Mungu endelea kuwatunza viongozi wetu wape heri na uhai wako kututumikia daima amen
Mbona una akili za kikondoo kondoo za kupenda watu kupigwa na umwamba? Dunia ya leo imestaarabika na tunategemea mtu kama ana makosa achukuliwe hatua stahiki na siyo kufanyiwa unyama. Umeathirika na akili za kitumwa na huenda umekulia kwenye mazingira ya kijima sana.
 
Huyo jamaa leo atapigwa sana...

Lakini tujiulize, kipigo ni njia sahihi ya kurekebisha maadili ya mtu?

Kama jibu ni ndio, kwanini tusitumie njia hii kwa viongozi wetu wasio na maadili!

Mfano mtu amefanya ufisadi anapelekwa jeshini, anapigwa sana.
Naunga mkono hoja.
 
Siku moja natokea Kinyerezi kwenda Mbezi nikashangaa pale Malamba mawili tunasimamishwa na mMP saa 12 asubuhi.
Kuuliza kuna nini, ndo nikaarifiwa CDF anatoka Nyumbani kwake kwenda kwenye majukumu.

Ni muhimu sana kuheshimu mamlaka
Kwan CDF anaishi Mbezi?
 
Back
Top Bottom