Hii daladala iliyotaka kuleta ajali msafara wa CDF iadhibiwe, haina adabu

Kumbuka enzi hizo barabara zilikuwa nyeupe! Sasa hivi bodaboda maelfu njoo daladala nazo ni hatari tupu. Sasa tukiachiwa tujiamlie tutapoteza viongozi kwa uzembe!
 
Kumbuka enzi hizo barabara zilikuwa nyeupe! Sasa hivi bodaboda maelfu njoo daladala nazo ni hatari tupu. Sasa tukiachiwa tujiamlie tutapoteza viongozi kwa uzembe!

..jiulize wewe unayetumia usafiri wa umma unawahi ktk majukumu na miadi yako, hawa vigogo wanaotumia vyombo vya serikali wanashindwaje mpaka iwalazimu kusumbua raia wema?

..enzi zetu waliokuwa na misafara ni Raisi, Makamu, Waziri Mkuu, na baadae waliongeza Katibu Mkuu wa Ccm.
 
Watu wanachoka jamani mtu mnasimamishwa saa nzima kumngojea mtu apite hii si haki.
Mbaya zaidi unaweza kuta msafara wa mkuu ulikuwa wrong side ya bara bara.. hawa viongozi saa nyingine wanaleta kero sana bara barabarani, wao ndio wenye haraka sisi raia hatuna haraka.
 
Kila nikimkumbuka CDF Francis Ogolla wa KDF naumia sana. Sasa huyu dereva asije akatupa huzuni nyingine hapa East Africa. Mungu amuepushe CDF Jacob Mkunda na mabalaa.
 
Mbona una akili za kikondoo kondoo za kupenda watu kupigwa na umwamba? Dunia ya leo imestaarabika na tunategemea mtu kama ana makosa achukuliwe hatua stahiki na siyo kufanyiwa unyama. Umeathirika na akili za kitumwa na huenda umekulia kwenye mazingira ya kijima sana.
 
Huyo jamaa leo atapigwa sana...

Lakini tujiulize, kipigo ni njia sahihi ya kurekebisha maadili ya mtu?

Kama jibu ni ndio, kwanini tusitumie njia hii kwa viongozi wetu wasio na maadili!

Mfano mtu amefanya ufisadi anapelekwa jeshini, anapigwa sana.
Naunga mkono hoja.
 
Siku moja natokea Kinyerezi kwenda Mbezi nikashangaa pale Malamba mawili tunasimamishwa na mMP saa 12 asubuhi.
Kuuliza kuna nini, ndo nikaarifiwa CDF anatoka Nyumbani kwake kwenda kwenye majukumu.

Ni muhimu sana kuheshimu mamlaka
Kwan CDF anaishi Mbezi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…