Mkuu nina utaratibu wakutembelea watoto yatima kila baada ya miezi 3 japo kuna wakati naenda kwa mwaka mara moja,nina makundi ya whatssap huwa natoa michango kwenye matatizo ama furava,nina dispensary natenga kiasi kuhudumia wanaohitaji matibabu lakini hawanafedha kila mwezi hii haitoshi?
Mkuu hakuna mtu ambaye kaumbwa awe pekeake pekeake tuu,kila mmoja anahitaji watu wa kuzunghmza nao,kutaniana na kucheka nao kila siku.
ukijaribu kuikimbia hii nature ndio utaangukia kwenye depression,stress,upweke,na kujiona uko bored na maisha.
ULaya watu wanaishi kipweke sana ndio maana wanasaiokolojia wanafanya kazi vizuri kwa sababu wateja wanao wa kutosha.
Na wateja hawa wanapatikana kupitia life style yao ya kuishi kivyaovyao,mtu katoka kazini,kajifungia ndani kabisa kutoka mpaka kesho,wengine hudhani kwamba kuwa hivi ndio ugenious ama sifa,wanajiumiza wenyewe.
Unahitaji muda fulani kukaa peke yako,lakini hiyo haina maana unahitaji muda wooote uwe peke yako.
Unahitaji muda fulani kulala,hiyo haina maana unahitaji muda wote ili ulale tuu.
Unahitaji muda fulani ili ule,hiyo naina maana unahitaji muda wote ili ule tuuu.
Unahitaji muda fulani kuongea na watu,hiyo haina maana kwamba unahitaji muda wooote kuongea na watu.
Utaona kwamba maisha ni mkusanyiko wa mambo madogo madogo ambayo utayafanya kila siku.
MUda huu utautumia kula,muda huu utautumia kulala,muda huu utautumia kuwa peke yako,muda huu utautumia kuongea na kukutana na watu.
Hayo ndio maisha,sasa utakapoamua kuyatafsiri maisha kwa kutumia jambo moja ukalifanya kwa muda mrefu jambo hilo basi lazima utajihisi tofauti.
Mfano ukaamua kwamba maisha yako wewe muda wote uwe peke yako,basi hapo utajiharibis mwenyewe maana hakuna unayemtesa na utajipunja kwani afya yako ya akili inahitaji watu wengine na mambo mengine ili uenjoy ile ladha ya maisha.
HApo mtaani tafuta kijiwe chenye heshima wanachoongea mambo ya maana japo kwa uchache kisha jiunge nao.
Au kama unaona kwamba mtaa huo umeshachelewa kujichanganya na ukahisi kwamba ukijichanganya na watu basi utawapa majungu ya kusema kwamba kiko wapi mbona alijifanya anakaa peke yake sasa anajichanganya? Basi hama mtaa tafuta mtaa mwingine ambao utakuwa rahisi kuanza maisha ya kujichanyanya na watu wengine.
Ndio maana watu wa uswahilini hawana stress wala upweke maana wanajichanganya na watu,wanajifunza mambo mbalimbali wanashirikiana vitu mbalimbali na hatimae maisha yanakuwa mazuri tu.
Ila ukiishi kiulayaulaya basi jua upweke utakuandama sana mkuu,na jambo hilo ni jepesi,usitafute mwanasaikolojia bila kutibu chanzo cha tatizo.
Ni sawa na mtu anayelala bila neti(mfano) akiumwa malaria anatafuta dokta anatibiwa then anarudi kulala bila neti anaumwa tena hivo hivo.
Mbona watu wengine hawahitaji wanasaikolojia wanaishi maisha yao vyema tu hawana mashaka yoyote ?
BAdili mfumo wako wa maisha,usijione special saana kwamba watu wengine hawana akili ya kuchanganyika na wewe hapana,unahitaji sana kuchanganyika na watu na bado una mambo mengi sana ya kujifunza na wengine.
Usitafute mchawi,mchawi ni life style yako haina afya.
NA watu aina yako husumbuliwa sana na kukosa usingizi maana muda wote huwa wako ndani,hawapati mwanga wa kutosha machoni,na hiyo inaleta tatizo la kutokulala mapema na kupata usingizi wa kutosha.
Tiba ya haya yote ni kujichanyanya na watu,sahau kuhusu introvert na maujinga mengine,just focus on what make and gives you peace.