Hii hali kwenye biashara siyo ya kawaida

Hii hali kwenye biashara siyo ya kawaida

Mnamo mwezi wa nane mwishoni nilifungua biashara ya kuuza kuku Wa kukaanga pamoja na viungo vyake.

Wakati nimeanza mauzo yalikuwa hafifu ikawa hata elfu 5 haifiki ya mauzo, ndo nikaja na Uzi wa kuomba ushauri
Wakajitokeza waungwana wakanipa msaada wa mawazo
Miongoni mwao ni dada angu kutoka kigamboni (jina namhifadhi).

Alinipatia msaada mkubwa niliwahi kuelezea kwenye Uzi
Baada ya hapo mambo yakawa mazuri nikawa nauza sana yani kwa siku nakaanga kama awamu 3 nauza wanaisha
Hali imeanza kubadilika wiki 3 zilizopita siuzi, unakuta nauza elfu 3 au sita.

Biashara yote inabaki kesho yake ukisema ni kuku Wa Jana watu hawanunui Sasa hivi mtaji naona unakata maana hakuna nnachoingiza

Nimeenda kwa mganga akanipa dawa za kuchoma na nyingine za kufukia ila wapi Hali inazidi kuwa mbaya

Nachanganyikiwa yani
Ungeshugulikia kwanza kujua sababu ya biashara yako kuyumba ingekuwa vyema zaidi ya kwenda kwa waganga utapoteza zaidi.
 
Hapo kwa mganga ndiyo umechemka. Ambacho ungefanya ni kucheza na upepo kuna kipindi raia mshiko unakata inabidi warudi kwenye tembele. Hivyo kwenye kipindi cha mpito ungepunguza mzigo ili kulinda mtaji. Then hali ikiimalika unaendelea kama kawaida
Nilifanya hivo mkuu ila Bado, mfano Leo Toka asubuhi mpaka muda huu nimeuza elfu nne na 200 tu!
 
Back
Top Bottom