Hii hali kwenye biashara siyo ya kawaida

Mnamo mwezi wa nane mwishoni nilifungua biashara ya kuuza kuku Wa kukaanga pamoja na viungo vyake.

Wakati nimeanza mauzo yalikuwa hafifu ikawa hata elfu 5 haifiki ya mauzo, ndo nikaja na Uzi wa kuomba ushauri
Wakajitokeza waungwana wakanipa msaada wa mawazo
Miongoni mwao ni dada angu kutoka kigamboni (jina namhifadhi).

Alinipatia msaada mkubwa niliwahi kuelezea kwenye Uzi
Baada ya hapo mambo yakawa mazuri nikawa nauza sana yani kwa siku nakaanga kama awamu 3 nauza wanaisha
Hali imeanza kubadilika wiki 3 zilizopita siuzi, unakuta nauza elfu 3 au sita.

Biashara yote inabaki kesho yake ukisema ni kuku Wa Jana watu hawanunui Sasa hivi mtaji naona unakata maana hakuna nnachoingiza

Nimeenda kwa mganga akanipa dawa za kuchoma na nyingine za kufukia ila wapi Hali inazidi kuwa mbaya

Nachanganyikiwa yani
Pole sana.
 
Nahis nimerogwa
😂😂😂 Tukianza kuwapa msasa juu ya mambo ya kibiashara kiroho mnasema tunaenda kuliwa Hela zetu kwa Watumishi, Ona sasa umerudi unalia😂 kama umeamua kwenda kwa mganga Nenda deep zaidi Nenda kachinje haswaaaaaa Fanya juu chini ukutane na Shetani mwenyewe au Kajisalimishe kwa wakuu wa soko wa hapo kiroho.
Lakini Ningekua Mimi nisingeanza biashara bila kuingilia mifumo ya hapo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Tukianza kuwapa msasa juu ya mambo ya kibiashara kiroho mnasema tunaenda kuliwa Hela zetu kwa Watumishi, Ona sasa umerudi unalia[emoji23] kama umeamua kwenda kwa mganga Nenda deep zaidi Nenda kachinje haswaaaaaa Fanya juu chini ukutane na Shetani mwenyewe au Kajisalimishe kwa wakuu wa soko wa hapo kiroho.
Lakini Ningekua Mimi nisingeanza biashara bila kuingilia mifumo ya hapo.
Connection upande wa giza mkuuu
 
😂😂😂 Tukianza kuwapa msasa juu ya mambo ya kibiashara kiroho mnasema tunaenda kuliwa Hela zetu kwa Watumishi, Ona sasa umerudi unalia😂 kama umeamua kwenda kwa mganga Nenda deep zaidi Nenda kachinje haswaaaaaa Fanya juu chini ukutane na Shetani mwenyewe au Kajisalimishe kwa wakuu wa soko wa hapo kiroho.
Lakini Ningekua Mimi nisingeanza biashara bila kuingilia mifumo ya hapo.
Mkuu we acha tu naona kumikumi hapa
 
Kwanza, mtegemee Mungu ktk mambo yako, usiende kwa waganga utapoteza muda na pesa

la pili, ktk biashara yapo mambo ya kuzingatia
1. Heshima kwa wateja, kuwa na nidhamu ya kazi, lugha nzuri kwa wote
2. Toa nyongeza kwa wale wateja wako wazuri
3. Usiuze ndaza, vyakula vilivyo lala
4. Jitahidi uwe na maboresho ktk biashara kwa ubunifu, ili iwe mpya kila uchao
5. Usikopeshe, maana utafukuza wateja
6. Weka na vingne vya ziada kama inawezekana
 
Mnamo mwezi wa nane mwishoni nilifungua biashara ya kuuza kuku Wa kukaanga pamoja na viungo vyake.

Wakati nimeanza mauzo yalikuwa hafifu ikawa hata elfu 5 haifiki ya mauzo, ndo nikaja na Uzi wa kuomba ushauri
Wakajitokeza waungwana wakanipa msaada wa mawazo
Miongoni mwao ni dada angu kutoka kigamboni (jina namhifadhi).

Alinipatia msaada mkubwa niliwahi kuelezea kwenye Uzi
Baada ya hapo mambo yakawa mazuri nikawa nauza sana yani kwa siku nakaanga kama awamu 3 nauza wanaisha
Hali imeanza kubadilika wiki 3 zilizopita siuzi, unakuta nauza elfu 3 au sita.

Biashara yote inabaki kesho yake ukisema ni kuku Wa Jana watu hawanunui Sasa hivi mtaji naona unakata maana hakuna nnachoingiza

Nimeenda kwa mganga akanipa dawa za kuchoma na nyingine za kufukia ila wapi Hali inazidi kuwa mbaya

Nachanganyikiwa yani
Mganga, eti mganga. Kwani huo wakati unauza ulienda kwa mganga? Au huyo dada wa Kigamboni nae alikuwa mganga! Si ulipata ushauri tu wa jinsi ya kutengeneza kachumbari au nimekosea!
Acheni kuwapa waganga/matapeli/wachawi promo.
 
😂😂😂 Tukianza kuwapa msasa juu ya mambo ya kibiashara kiroho mnasema tunaenda kuliwa Hela zetu kwa Watumishi, Ona sasa umerudi unalia😂 kama umeamua kwenda kwa mganga Nenda deep zaidi Nenda kachinje haswaaaaaa Fanya juu chini ukutane na Shetani mwenyewe au Kajisalimishe kwa wakuu wa soko wa hapo kiroho.
Lakini Ningekua Mimi nisingeanza biashara bila kuingilia mifumo ya hapo.
HaHaHa.....sasa mkuu ndio utoe Laki tano kumwona Kiboko ya Wachawi?
 
Ukizifatilia utagundua sauti za watu ni wale wale wanabadilisha location tu.

Leo anasema tuko Mwanza kesho anajitaja ni wa Songea.
Wale washenzi sana. Nilikua nawarekodi ili niwe nacheka mke analia mtoto wake kafa anaambiwa mkwe wake mchawi bibi anapewa simu anasema Mimi sitaki mambo yenu😂😂😂😂 mume mtu anajifanya kuwanyamazisha waache kulia waendelee kumsikiliza mtumishi😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom