Hii hapa mikoa 12 inayoendesha uchumi wa nchi, inamiliki na kushikilia asilimia 70% ya uchumi wa Tanzania

Kazi ya Mwl ni kelewesha. Tiririka mpaka nikuelewe.
GDP=C+I+G+Net Exports where by
Gross Domestic Product=Pato la Shughuli zote za uzalishaji, uwekezaji na matumizi ndani ya Mkoa husika zikithamanishwa Kwa hela.

C=Consumption,Jumla ya manunuzi/matumizi yote ndani ya Mkoa ya watu, Serikali, taasisi nk

I=Investments, Uwekezaji wa private au Serikali

G=Government Spending/Expenditures,Jumla ya Matumizi ya Serikali Kwa mwaka husika kwenye miradi na Huduma za jamii.

Net Exports (Exports less Imports) kinachobakia ndio kinajumlishwa kama pato na inaweza kuwa positive or negative.

Kiufupi Sasa hiyo 8.8T ya Arusha ndio Kila uzalishaji au service industry kama Utalii nk vilivyozalishwa ndani ya Mkoa Kwa mwaka husika ndio vina thamani hiyo.

Sasa kwenye hiyo serikali imechukua chake Kwa njia ya Kodi ,tozo nk Sasa unaweza Kuta Sasa kwenye kutoa let taarifa za Mapato ukakuta Arusha imechangia Mapato mengi lbda ya TRA sababu ni kwamba Kuna Baadhi ya sekta ziko taxable zaidi au Kwa nature yake Zina attract Kodi mfano Utalii ,lakini kuna Baadhi ya sekta Sina Kodi kiduchu au Hazina mfano Uzalishaji wa Kilimo,mambo hayo ndio huleta utofauti wa Wingi wa Kodi baina ya Mkoa na Mkoa.
 
Mkuu nina mpango nije nioe binti wa kihangaza huko ngara
 
Ukiulizwa jibu vizuri sitaki kukuvunjia heshima kuna baadhi ya watu humu JF uwa nawaheshimu na wewe ukiwemo
Ndio imezidiwa Kwa Pato la Mkoa maana Dom Wana 6T vs 6.7T ya Tabora ila tukija kwenye swala Zima la wapi Kuna concentration ya GDP utakuja Dodoma Mjini ndio imeendelea kushinda Tabora ambayo uchumi wake (GDP) umesambaa na pengine una uwiano kutoka Wilaya Moja Hadi nyingi eg Tofauti ya Nzega,Igunga sio kubwa sana na Tabora mjini.

Lakini Kwa Dodoma,GDP yake haina uwiano baina ya Wilaya yaani hapo Mjini ndio Kila kitu huko Kongww ,Bahi sijui Vijiji gani ni hovyo tuu.
 
Mbeya inabeba uchumi wa mikoa minne...Rukwa,katavi,Songwe etc .
Takwimu sometimes zinadanganya
 
Uwekezaji wa Miundombinu ya Barabara una mchango mkubwa kwenye Uchumi na kuondoa umaskini na sio huo mwingine wa SGR.

Takwimu hizo zinaonesha ushahidi huo huko Mikoani ambako Barabara zimeanza kufungua Uchumi
Ni mapema sana ku judge return ya sgr, ipe next 10 years
 
Sawa.
1. Uko wapi?
2. Kwa nini Muhangaza?
3. Kuna ninachoweza kukusaidia?
Nipo mtwara,nimeambiwa wengi wao ni wife material ni wavumilivu wengi wanafanya rejea kwa mabinti wa kazi wanaotoka huko...vipi na wewe unawafahamu kiundani? Nimeamua nipumzike huku pwani unaoa mwanamke ambae mguu mmoja ndani mwingine nje
 
Nipo mtwara,nimeambiwa wengi wao ni wife material ni wavumilivu wengi wanafanya rejea kwa mabinti wa kazi wanaotoka huko...vipi na wewe unawafahamu kiundani? Nimeamua nipumzike huku pwani unaoa mwanamke ambae mguu mmoja ndani mwingine nje
Nitakujibu endapo utanijibu yafuatayo:
1. Wewe ni mwenyeji wa Mtwara au umehamia?
2. Maelezo yako yanaonesha ulishaoa. Mwangaza atakuwa mke wa ngapi? Uliotangulia kuwao/ kumwoa mngali pamoja?
 
Nitakujibu endapo utanijibu yafuatayo:
1. Wewe ni mwenyeji wa Mtwara au umehamia?
2. Maelezo yako yanaonesha ulishaoa. Mwangaza atakuwa mke wa ngapi? Uliotangulia kuwao/ kumwoa mngali pamoja?
Mimi kwetu ni mtwara ila nimekulia Mozambique ...na ni kweli niliwahi kuoa huku huku pwani ila baadae tukaja kutengana
 
Wale Wana list Yao wa Mikoa maskini zaidi,nitakuja nayo hivi punde 😁😁
Unaongelea maendeleo ya wakazi wa eneo husika au unaongelea mali zinazovunwa katika eneo husika?? Mikoa mingi hapo unaiona juu lakini Maisha yao duni kulika Kagera kwa Sababu ya maliasili zilizopo na zinavunwa kwenda Kuleta maendeleo kwingine. Bora ungekuja na mapato ya halmashauri yanayogusa direct shughuli za wananchi ungeeleweka otherwise hizi porojo unajipigia tu
 
Nipo mtwara,nimeambiwa wengi wao ni wife material ni wavumilivu wengi wanafanya rejea kwa mabinti wa kazi wanaotoka huko...vipi na wewe unawafahamu kiundani? Nimeamua nipumzike huku pwani unaoa mwanamke ambae mguu mmoja ndani mwingine nje
1. Siwafahamu sana Wahangaza, lakini nimeshawahi kuishi na baadhi yao kwa muda mfupi. Ni watu wazuri kama ilivyo kwa Jamii kubwa ya Watanzania.

2. Kama unataka kwenda kuoa Ngara, nenda kwa amani. Lakini si lazima umwoe Muangaza. Kuna na makabila mengine pia huko, hata Wasukuma wapo. Lenga kumwoa mtu utakayeamini mtaweza kushare kila kitu katika maisha yenu. Huoi kabila, unamwoa mtu

3. Kikubwa ni wewe kuthibiti mitazamo yako kiusahihi!

Unajua hata raia wa Mataifa ya kigeni, kama Wanigeria na Wakenya wanaamini mabinti wa Kitanzania ndiyo wanawake bora wa kuwaoa? Wanaposema hivyo, wanawamaanisha Wachaga, Wameru, Wasukuma, Wamakonde, Wamwera, Wamasai, Wasambaa, Wahaya, Wahangaza, Waha, Wafipa, Wakurya, n.k.

4. Ingawa watu wa mikoa mingine wanaamini kuwa Waha na Wahangaza ni wife material, wanaume wengi wa Kiha na Kihangaza, hasa wanaoishi jirani na Burundi, hupendelea kuoa mabinti wa Kirundi. Leo nilipomwuliza kijana mmoja wa Kihangaza sababu inayowapelekea baadhi yao kuamua kuwao Warundi alinipa sababu mbili. Ya kwanza ni kwamba wanawake wa Kirundi ni wachapa kazi sana, na ya pili ni mahari wanayotozwa Burundi ni kidogo sana ukilinganisha na ya kwa Wahangaza.

Kwa hiyo, kama unataka kumwoa Muhangaza wewe fanya hivyo, lakini usitarajie mwujiza katika ndoa yako. Mwanamke haolewe akiwa "amekamilika", ni kazi ya mwanaume "kukamilisha".

Ndoa bora ni matokeo ya "uwekezaji" bora.
 
Umelalamika sana mkuu!!πŸ™„πŸ™„
Hivi mkoa wa Kagera hauna wawakilishi kwenye vikao vya maamuzi?
Shirikianeni na wabunge wenu, zalisheni mahindi, maharage na matunda kwa wingi mrudishe heshima yenu.
 
Naunga mkono
 
My Take
Mikoa ya Ruvuma, Shinyanga, Mara, Geita na Tabora ni game changer kwenye Uchumi wa Nchi, kutoka kusikojulikana hadi kuwa Mikoa muhimu ni jambo la kupongezwa na kuonesha kwamba kumbe ukifungua Nchi Kwa miundombinu Uchumi unafufuka.
Mnapoambiwa Bashe kaeleweka sana mikoa ya Ruvuma na Mbeya na ile yenye kutegemea kilimo nyie hamuelewi. Ila hapa namba zinajieleza zenyewe. Kifupi kama mvua zingekuwa za kawaida mikoa hiyo mwaka huu wangevunja rekodi.

Bashe mpeni maua yake, nyie wa makelele endeleeni tu lakini unafuu wa maisha ndio jibu.
 
Safi sana... Sisi wazaramo hamtuwezi... Dar on top 😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…