Hii hapa orodha ya wanahiphop bora wa muda wote Tanzania

Hii hapa orodha ya wanahiphop bora wa muda wote Tanzania

Nimeanza kufatilia hip-hop mwanzoni mwa miaka ya 2000 tangu nikiwa chekea Hadi Leo ni zaidi ya miaka 20 huyo msanii namba tatu sijawahi msikia kabisa hebu nipe Ngoma yake moja nimsikilize....

Halafu inaonekana unapenda hip-hop lakini hujui chochote kuhusu hip-hop
Kama humjui Mikiller basi wewe sio mwanafamilia wa Hiphop nchini Tanzania. Ingia hata Insta u-search
 
Ni
NimeomeimKwa sisi tusiojua muziki, hip hop inatofauti na nyimbo za akina Blue, FA, Afande Sele, Prof J n.k?

Huwa nachanganyikiwa kutofautisha, Eminem na Jay Z, wanafanya muziki wa aina moja? Yaani Tupac na Pdiddy(sijui ndo hivyo?) wanaimba au wana rap? Tofauti ya kuimba na ku-rap hasa ni ipi?

AY alisema yeye style yake ni commercial, Fid Q akakataa kuwa yeye hafanyi Bongofleva, nikasikia sijui kuna wabana pua; Marlaw na akina Bia tamu, Jux wanafanya aina gani?

Mpoto je?

Kughani ni kufanyaje?
Nimeongeza namba 11 hadi 20. Labda msanii wako yupo.
 
HipHop au Rap?

Dogo janja......[emoji6]
 
Kijenge Juu - Watengwa.

Uhasama wa Taifa - Bamia TV - Zimaaaaaa
 
Hivi JCB yuko wapi kwa sasa!!??
Kuna dude lake nililisikia mwaka 2000 pale "Via Via", nilikoshwa sana japo silikumbuki linaitwaje.
 
Wakuu pamoja na kupenda siasa za CCM ila pia mimi ni mnazi mkubwa wa muziki wa Hiphop. Tangu utotoni nimekua nikipenda Hiphop. Nimekuwa nikisikiliza nyimbo za GWM, Mr II, Dollar Soul, JCB & Watengwa, Nako2Nako, Juakali, hadi hawa waliopo kwenye chati kina PMawenge.

Nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana kwenda pale Uwanja wa basketball Soweto, Arusha kutazama matamasha ya hiphop yaliyokuwa yakifadhiliwa na Sprite. Kiufupi mimi ni mwanafamilia wa Hiphop.

Hii hapa orodha tukufu ya wanahiphop bora kuwahi kutokea nchini, inaanza na bora zaidi hadi namba 10:

1. Mr II (Sugu) - haihitaji kubishana kwamba huyu Joseph Mbilinyi ambaye pia ni mbunge mstaafu wa CHADEMA na mnufaika wa michango ya join The chain kuwa ni mwanahiphop bora zaidi wa muda wote nchini. Ana alama nyingi sana kwenye hiphop Tanzania.

2. Profesa Jay - huyu ni binadamu anayependwa na kila mtu bila kujali itikadi. Kwenye hiphop ya Tanzania ana alama zake zisizofutika.

3. Mikiller Gego - ni mwanahiphop ambaye pia ni mhandisi kitaaluma. He is a scientist & artist. Nyimbo na makala zake zimewagusa hadi wapenzi wa muziki wa Taarabu.

4. Lord Eyes - member wa N2N na sasa Weusi. Kwakweli kwa zile flow alizo nazo Lord Eyes angeweza hata kuwa namba moja sema ana matatizo binafsi ya nje ya Hiphop yanayomfanya ubora wake mara nyingi ushuke.

5. Joh Makini - mwamba wa kaskazini haina haja ya kumzungumzia sana kwa sababu anaeleweka balaa lake.

6. Chid Benz - pamoja na kuwa teja lakini Chid Benz ni mwanahiphop bora wa muda wote. Haihitaji ubishi.

7. Nikki wa II - Ubora wake kwenye Hiphop ulifanya hadi ikulu imtambue na kumteua aisaidie nchi kwenye uongozi ngazi ya ukuu wa wilaya. Ni mwanahiphop anayetajwa kumiliki mtoto mkali hatari yaani MASHINE MNATO.

8. Fid Q - Ngosha the Don hana mambo mengi yanayomfanya awepo kwenye hii orodha tukufu zaidi ya kipaji chake.

9. Nikki Mbishi - ubishi wake ni talent.

10. Dogojanja - hakuna dogo anayeweza kuchana kama yeye.

UPDATE; Kutokana na maombi ya wengi wenu ninaongeza majina namba 11 hadi 20.

11. Zay B - yupo gado. Alibamba miaka ya 2000 mwanzoni na kisha kupotea kabisa.

12. MwanaFA - binamu.

13. Witness - huyu alikuwa na kundi lao na kina Marehemu Langa.

14. Chindo Man (Umbwax)

15. JCB - ukisikia Paah ujue imekukosa.

16. Azma Mponda (Aznas)

17. KR - muziki mnene CD 700.

18. Mansu Li

19. Kala Jeremia

20. Jay Moe.
Bila rosa lee na chemical sioni kam ni kweli.
 
Back
Top Bottom