Hii imekaaje, kosa la mume polisi kumpiga mke ili aonyeshe mumewe alipo?

Hii imekaaje, kosa la mume polisi kumpiga mke ili aonyeshe mumewe alipo?

Kumficha mtuhumiwa au muhalifu ni kosa kisheria, Raia yoyote yule anatakiwa atowe ushirikiano kwa vyombo vyetu vya kisheria, hata police wapo kisheria, bora kapewa kofi as worning kuliko angefunguliwa kesi ya kuficha muhalifu, na kuficha muhalifu inaonekana na wwe unafaidika na uhalifu huo!!
Kwanini kupigwa makofi ni bora kuliko kufuata sheria inavyotaka? Hiyo sheria ina kazi gani sasa iwapo kuna mbadala wenye ubora? Tuifute tu tuweke hii unayosema ni bora watu wakihisiwa wanaficha mhalifu badala ya kumpeleka kituoni kumhoji wazibuliwe makofi.
 
Afya ya Akili ni Janga,wanaangalia upande Mmoja!,Yeye akifyatuliwa Kofi anajisikiaje sijui!
 
Habari wanajamii,imetokea Leo polisi,wakiwa kwenye gari Binafsi,wamekuja kwa jamaa bila balozi wa mtaa na kugonga geti na kumkuta mke awaonyeshe alipo mumewe .Cha kushangaza mwanamke akawa kama anasita kueleza alipo mumewe, Askari wa kike akatoka kwenye gari na kumnasa makofi huyo mke wa jamaa!Na kumtishia kumpeleka kituoni,Ni hapa Kisasa_Dodoma.
Hata kama Huyo mama angekuwa mtuhumiwa hapaswi kupigiwa Wala kutwezwa utu wake.

Si jukumu lake kutoa taarifa kwa polisi hao bila kuambiwa mumewe anatuhumiwa kwa kosa Gani, RB namba yake, lakini pia polisi wangeweza TU kutoa notice afike kituoni na si ajabu mtuhumiwa angeenda yaani Kuna wakati polisi wanatumia nguvu pasipo na sababu yeyote
 
Wanatafuta uadui usiokuwa na ulazima,ndio maana wakistaafu wanaishia kuishi kwa shida uraiani!
 
Maana uwe na pesa za kumpata huyo mwanasheria. This is a 'Police State'.
Daah...! Mtu unaonewa bila sababu na unakuwa huna cha kufanya. Haya mambo yanatokea kwa nchi hii tu. Mnigeria wamefindishwa sheria wale watu. Tena sio waoga kama sisi. Tumekuwa kama ndezi ndani ya mabanda
 
Nitajuaje kuwa wewe ni mhalifu kabla ya kuambiwa wewe ni mhalifu! Yaani nikiulizwa na askari wewe uko wapi basi nijue wewe ni mhalifu! Haiwezekani.
Ulikuwepo mwanzo mwisho wa tukio au unakisia yaliyoendelea!!?
 
Back
Top Bottom