Uchaguzi 2020 Hii inakatisha tamaa kwa Dkt. Magufuli

Uchaguzi 2020 Hii inakatisha tamaa kwa Dkt. Magufuli

Alitegemea kukubarika zaidi, kwa jinsi alivyokuwa akitumia vyombo vya Habari, shirika la utangazaj nchini TBC, vyombo vya Habari vya CCM.

Yawezekana watu hawavifuatilii sana ama ugumu wa maisha kwa watanzania a.k.a vyuma vimekaza vina wafanya watu wabeze juhudi zake, ama visasi kwa wanaompinga na kumkosoa, wabunge wa CCM kusifu kila linalofanywa na serikali hata kama baya ama kuna usaliti ndani ya CCM, ama amekosa watu makini wenye uzoefu na kampeni ama mgombea wa CHADEMA ana Sera nzito zinazosikika na kueleweka na kugusa maisha ya Watanzania.

Kiukweli kama ulifanya vitu vingi vya kujitoa hata kuhatarisha maisha Lakin watu hawaoni hii inaweza kumkatisha tamaa JPM.

Ni Kweli awamu ya tano Iko kwenye ujenzi wa miundombinu, maendeleo ya nchi na vitu Lakin Wananchi Wana hali ngumu.
Kwa moyo wa kibinadamu tu kwa jinsi watanzania walivyoonesha kumkataa lazima akate tamaa.

Alianza vibaya atamaliza vibaya. Mwache avune alichopanda. Pk alimpoteza.
 
Umefanya vizuri kutojipendekeza, lakini watanzania hatutaki sifa ya kabila iwe kigezo cha kuchagua kiongozi. Ni muhimu Watanzania wajue Una elimu gani, uzoefu uliotukuka na mabadiliko ulio yafanya au mchango wako kwako wewe binafsi na kwa jamii kwa wakati huu.

Sifa ya kuteuliwa ni kwa wanyonge tuu kwenye siasa (mediocrity) , tunatakiwa tuamini uwezo wetu na uwe kwa mfumo wa Meritocracy.
Hayo kwa jiwe hayana nafasi! Hivi kwa ajili yako unaweza kuamini wale watu walioteuliwa kuchukua nafasi za DEDs, DAS, n.k?
 
..tatizo la Magufuli siyo mjenga hoja mzuri.
Na ukishindwa kujenga hoja unakosa sifa ya kuwa kiongozi. Kiongozi hapimwi kwa uwezo wa kulima matuta ya viazi au kubeba mizigo mizito bali hoja zake za kujenga nchi na kuongoza timu yake.
 
Ni humu kwenu jf tuu ndo hakubaliki
Siku aliyopanga kurudi ilipotangazwa watu wa aina yako walidai hivyo hivyo kwamba watu wa Mh. Tundu Antiphas Lissu wako mtandaoni tu hawapo Tanzania. Lakini siku ndege yake ilipotua, umati uliojitokeza kumpokea uliwashangaza wabaya wake...endeleeni kujifariji hivyo hivyo, mtakapozinduka mtakuta mkazi mpya keshatinga Magogoni. Nawahurumia kweli kweli!
 
Alitegemea kukubarika zaidi, kwa jinsi alivyokuwa akitumia vyombo vya Habari, shirika la utangazaj nchini TBC, vyombo vya Habari vya CCM.

Yawezekana watu hawavifuatilii sana ama ugumu wa maisha kwa watanzania a.k.a vyuma vimekaza vina wafanya watu wabeze juhudi zake, ama visasi kwa wanaompinga na kumkosoa, wabunge wa CCM kusifu kila linalofanywa na serikali hata kama baya ama kuna usaliti ndani ya CCM, ama amekosa watu makini wenye uzoefu na kampeni ama mgombea wa CHADEMA ana Sera nzito zinazosikika na kueleweka na kugusa maisha ya Watanzania.

Kiukweli kama ulifanya vitu vingi vya kujitoa hata kuhatarisha maisha Lakin watu hawaoni hii inaweza kumkatisha tamaa JPM.

Ni Kweli awamu ya tano Iko kwenye ujenzi wa miundombinu, maendeleo ya nchi na vitu Lakin Wananchi Wana hali ngumu.
Haya maelezo ilitakiwa uyatoe baada ya tarehe 28 Oktoba. Mnayatoa mapema kwasabbu mnajua baada ya uchaguzi mtalikimbia hili jukwaa.
 
  • kibaya zaidi amekutana na mgombea ambaye ni saizi yake kihoja na kiutu
  • kibaya zaidi huwezi kumchafua lissu kwa sababu CV yake ya kuwapigania walalahoi inafahamika tofauti na ilivyokua kwa lowassa.
  • unapaswa uwe na roho ya kikatili kumchagua kiongozi ambaye ameshindwa kuwakamata watesaji wa Tundu Lissu
Kilichonisikitisha kumfukuza ubunge mtu unayejua kuwa ni mgonjwa tena ukamnyima na mshahara na matibabu. Hii dhambi inatutafuna

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli aliwekeza zaidi kwenye propoganda,barabara nyingi bado zipo pale pale alipoishia kikwete,na ujenzi wa reli ndo kwanza umeanza,kwa kifupi he has done nothing
Duh.. Ujenzi wa reli ndo umeanza, mabarabara yote mapya mikoani na kwenye mitaa unasema zimejengwa enzi za kikwete. kweli wewe hujijui, Mungu akusamehe
 
Kilichonisikitisha kumfukuza ubunge mtu unayejua kuwa ni mgonjwa tena ukamnyima na mshahara na matibabu. Hii dhambi inatutafuna

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
swadakta,
na tendo lile ndio lilizidi kuchochea khofu na maswali ya kwamba serikali huenda ina chembe ya uhusika wa tukio la kushambuliwa kwake.
bunge halikupaswa kuchukua hatua kama ile.
 
Ingekuwa enzi za mwalimubangefaulu, nakubali amefanya mengi mazuri lakini HANA KIASI, Bible inasema iweni na KIASI kwa kila jambo, gusa kila sehemu, yeye amewasahau watu.Lakini Bible pia inasema WA KWANGU HAWAPO CHINI YA SHERIA, UONGOZWA NA BUSARA.Yeye kazama kwenye sheria zaidi na kujikuta anayaumiza makundi mengi katika jamii.

Hata hizo sheria nyingi anazitumia kwa kukomoa na anatekeleza sheria kwa double standard ya wazi kabisa. Kibaya zaidi yeye binafsi hana lolote analofanya kwa kuheshimu sheria, ukiona sheria anaifuata ujue haimuumizi yeye. Lakini matokeo yoyote yatakayotokea kwenye uchaguzi huu, atakuwa ameelewa watu wanataka nini, na sio nini anataka kuwapa watu.
 
Alikuwa anadanganywa na wasaidizi wake kwamba anakubalika walimfeed taarifa azipendazo ili wampige pesa, ndo ajue unafiki wa watz.
 
Nitajie nchi ambayo Rais anayetetea nafasi yake huwa anaachana na majukumu yake ya Urais pale inapofikia kipindi cha Uchaguzi mkuu.
Anaagiza vipi wakati sio raisi na October arudi tena kuumiza watu.
 
Kwa moyo wa kibinadamu tu kwa jinsi watanzania walivyoonesha kumkataa lazima akate tamaa.

Alianza vibaya atamaliza vibaya. Mwache avune alichopanda. Pk alimpoteza.
Badala ya kuwasikiliza watz akamsikiliza pk anaeongoza kamkoa tu.
Anga limemkataa Mungu kamuondolea kibali badala ya kuchunga kondoo anawapiga risasi Mungu anataka hesabu sijui atajibu nini.
 
swadakta,
na tendo lile ndio lilizidi kuchochea khofu na maswali ya kwamba serikali huenda ina chembe ya uhusika wa tukio la kushambuliwa kwake.
bunge halikupaswa kuchukua hatua kama ile.
Kwa muujiza ule wa kupona risasi 32 ningekuwa mimi ndo muusika ningetubu kwa Mungu na kuamua kumtumikia Mungu maisha yangu yote yaliyobaki duniani ili angalau nifidie dhambi nilizomkosea Mungu
 
Back
Top Bottom