Hii inawezekana vip?

Hii inawezekana vip?

Hammer11

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2024
Posts
1,518
Reaction score
2,174
Niliwahi kuhudhuria darasa moja, nikastajabu sana. Huyo mwalimu alitufundisha eti kuna sijui nabii au mtume kiongozi wa dini aliwahi kupanda farasi sijui punda akaenda mbinguni. Alipofika huko akakutana na manabii wa kale wakina Musa, Yusuph na wengineo. Ila hakukutana na mtu mweusi wa kale hata mmoja.

Tuache hicho. Sasa mimi nikaondoka na maswali mpaka leo sina jibu. Wakina Musa na mitume wote walizikwa, sasa huyo kiongozi huko mbinguni alikutana nao kwa namna gani? Kama mizimu au ni vipi?

Wenye elimu na hii wajue. Na yeye alipaaje hadi huko mbinguni? Alikuwa mfu au mzima? Asanteni. Kumbukeni mimi sina dini yoyote, naamini mizimu ya uziguani kwa babu zangu.
 
Kila mtu anayekufa mwili huoza nafsi huenda kwa Mungu kama mtu alikuwa mzuri na kama alikuwa mwovu nafsi inakwenda kuchomwa moto.

Maana yake ni hivi nafsi huishi hata baada ya kifo.

Roho zote ni Mali ya Mungu, mtu atende maovu au mema roho yake lazima itakwenda kwa Mungu. Ez 18:4.

Kwahiyo kwakuwa nafsi haifi kuna uwezekano wa kumuona mtu aliyekufa miaka hata elfu 10 iliyopita.

Ila huyo mtume wa kupanda Ibraku alikuwa wa mchongo, muongo mwongo kama baba yake
Screenshot_20241116-231630.jpg
shetani . Yoh 8:44
 
Niliwahi kuhudhuria dalasa moja nikastajabu sana huyoo mwalimu alitufundisha ety kuna sujuii nabii au mtume kiongozi wa din aliwahi kupanda farasi sijui punda ...
Hili darasa liliisha, au wewe ulikatisha masomo njiani?

Nadhan ungefuatilia darasa mpka mwisho ungekuja kusimulia katika ukamilifu zaidi gentleman,

Hata hivyo akili za kuambiwa ni sharti uchanganye na zako, ili kuepuka wa akina Kibwetere na Makenzi wa humu mjini wasikurestishe in peace kwa njaa🐒
 
hili darasa liliisha, au wewe ulikatisha masomo njiani?

nadhan ungefuatilia darasa mpka mwisho ungekuja kusimulia katika ukamilifu zaidi gentleman,

hata hivyo,
akili za kuambiwa ni sharti uchanganye na zako, ili kuepuka wa akina Kibwetere na Makenzi wa humu mjini wasikurestishe in peace kwa njaa🐒
Niliona ujinga nikasepa mtaan kutafuta pesa mtuu anapaaajee na punda kaka
 
Ule uongo Samson aliua simba mimi ndipo huwa sielewi, hivi Israel ilivyo jangwa hao simba walikuwa wanafugwa? Simba anaishi vipi middle east kwenye nchi za jangwa?

Halafu baada ya kumuua baadae anapita kwenye huo mzoga wa simba akakuta asali, eti akaanza kulamba🤣

Huwa nachoka...
 
Niliwahi kuhudhuria dalasa moja nikastajabu sana huyoo mwalimu alitufundisha ety kuna sujuii nabii au mtume kiongozi wa din aliwahi kupanda farasi sijui punda akaenda mbinguni afuu sasa kufika huko akakutana na manabiii wa kale wakina musa yusuph na wengineo ila hakukutan na mtu mweusi wa kale hata mmoja tuache hicho sasa mm nikaondoka na maswali mpaka leo cna jibu wakina musa na mitume wote walizikwa sasa huyoo kiongozi huko mbinguni alikutana nao kwa namna gani kama mizimu au ni vip wenye elimu na hii wajee na yeye alipaaje hadi uko mbinguni alikuwa mfu mzima asanten kumbukeni mm sina dini yoyote naamini mizimu ya uziguani kwa babu zangu

Kuwa na macho ni jambo moja na kuona ni jambo la pili.
 
Yule jamaa alipandwa na mapepo akiwa mapangoni kwenye kuchunga mbuzi wa mke wake .
Hata huo Utume alipewa na mke wake na mjomba wake
Sasa mdau, hayo ni mambo katika ulimwengu wa roho, hujawahi kusikia wahubiri wanakuambia ulimwengu wa roho, katika huo ulimwengu mtu anaweza kusafiri hapa na US ndani ya sekunde... Ni sawa na masuala ya astral projection...

Masuala ya imani yapo complex, majini ni roho, malaika ni roho, ndio maana jini hulioni...

Nahisi hata wachawi wanatumia hayo masuala ya ulimwengu mwingine...
 
Ule uongo Samson aliua simba mimi ndipo huwa sielewi, hivi Israel ilivyo jangwa hao simba walikuwa wanafugwa? Simba anaishi vipi middle east kwenye nchi za jangwa?

Halafu baada ya kumuua baadae anapita kwenye huo mzoga wa simba akakuta asali, eti akaanza kulamba🤣

Huwa nachoka...
Kisa cha Samson kimelenga miaka zaidi ya 350 BCE pale Hebron palikua na misitu na mapori yenye wanyama kabla ya mabadiliko ya kimazingira yaliyopelekea ukame na semi Arid
Ila hapo mbele sijui wewe amini tu hiyo hadithi kama ni kweli au uongo utajua mwenyewe!
😁😁
 
Sasa mdau, hayo ni mambo katika ulimwengu wa roho, hujawahi kusikia wahubiri wanakuambia ulimwengu wa roho, katika huo ulimwengu mtu anaweza kusafiri hapa na US ndani ya sekunde... Ni sawa na masuala ya astral projection...

Masuala ya imani yapo complex, majini ni roho, malaika ni roho, ndio maana jini hulioni...

Nahisi hata wachawi wanatumia hayo masuala ya ulimwengu mwingine...
Sasa huyoo kiongozi Alienda kama jini au mchawi
 
Back
Top Bottom