Mie naona kula na aina ya vyakula kama mazoea, umezoea mihogo kupikwa hivyo ila mie naona mapishi ama chakula ni ubunifu sijui nisemaje, na ndio maana ukitoka ukienda nchi nyingine utajionea mashkolo mageni, mchele ni ule ule ila mapishi tofauti na wenzio wanakula bila tabu, na ww ukiwapelekea mapishi yako unayoona ni sahihi watakuona wa ajabu kabisa..
Kuna mtu alinikuta nakunywa zangu uji na mkate akanishangaa kichizi, eti anaona ajabu nikamwambia tatizo umekremisha vitu ulivyovikuta, nikamwambia katika jamii yetu ungekuta watu wanakula hivi nawe ungekuwa unakula mtu akinywa chai na mkate ungemshamgaa "ungekuta nyama inaitwa kisamvu na kisamvu ni nyama pia ungeita hivyo hivyo"..
Utatuzi wa suala lako mkuu, jitahidi uingie jikoni umpikie kama mara 2 mara 3 hiv ataona utofauti ama mueleze ukweli japo hii si njia nzuri saana kibinadamu, we ingia jikoni pika.. Km una nafasi shiriki katika mlo wenu wa siku kuanzia kuchagua mnakula nini mpaka upishi wake.. Mie sijui kwanini wanaume wenzangu wengi hawaprndi kushiriki hili jambo.