Hii kauli Dotto Magari kuhusu Elimu. Anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa kupotosha na kutukana umma

Hii kauli Dotto Magari kuhusu Elimu. Anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa kupotosha na kutukana umma

Kwangu namuona ni mtu ambaye amejaaliwa kipato lkn ana majivuno pia

Ameshasahau aliyemjalia hayo ni Allah,hivyo anajiona ni ujanja wake

KIburi ni kitu kibaya sana hapa duniani
Neema zinawapumbaza watu wengi. Japo muda wowote mambo yanabadilika,. Aliyejuu anaweza kushuka na wachini akapanda juu. Kwahyo haistahili kumdharau mtu kwasababu yeyote
 
Hii yote imesabanishwa na serikal ya Ccm leo hii msomi anaonekana hana maana yan leo hii Tz msomi anadharauliwa na chawa dalasa la saba kisa tu anaweza kushika pesa
Ni muda wa wasomi kubadilika na kufanya kaz na kutafta haki zao km wasomi
 
Anachosema ni ukweli mtupu.

Mimi nikikutana na mtu ana hela kuliko mimi basi pia atakua na akili kunizidi, maana haiwezekani uwe na akili halafu ukose hela, narudia tena haiwezekani.

Huna hela = Huna akili.
Kwa hiyo Daktari aliyeamua kupata mshahara mdogo ili kuokoa maisha ya watu hana akili. Kwa hiyo mwalimu wa shule ya msingi St Kayumba kwa wito wake akaamua kujitolea kufundisha watoto wa kaya masikini kwa mshahara mdogo hana akili, kwa hiyo hata wale wataalamu wengine waliojitolea kusaidia jamii kwa kutumia elimu zao hawana akili.

Hela sio kipimo cha akili, kuna wengi wasio na hela ila wana utajiri wa nafsi. Tusipende dharau, kila mtu anamtegemea mwingine.
 
Back
Top Bottom