Hii kauli Dotto Magari kuhusu Elimu. Anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa kupotosha na kutukana umma

Hii kauli Dotto Magari kuhusu Elimu. Anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa kupotosha na kutukana umma

Hapo ndo tatizo linapoanzia watu.akili kisoda kabisa. Ivi kwa mfano unafika hospital unaambiwa daktari hayupo kaenda kwenye michongo na hakuna Huduma how will you fill? Hata siku moja elimu/Uvumbuzi haviwezi kuwa replaced na pesa never
Tafuta hela kelele za nini wewe kilaza kama huna hela maana yake huna akili
 
Kwa sababu hajafanya kosa lolote ametumia haki yake ya kikatiba na kibinadamu tu kujieleza.

Na ingawa hajajieleza vizuri sana, hoja yake ya kimsingi ina mantiki.

Ukiondoa maneno ya shombo yote na dharau zake, hoja yake ya kimsingi ni kupingana na logical fallacy ya "argument from authority" ya kuheshimu sana vyeti, elimu rasmi.

Kimsingi anasema yeye ni salesman mzuri kuliko wasomi wengi waliosomea marketing and sales kwenye elimu rasmi.

Na unaweza kupima hilo kwa kuangalia matokeo ya kazi zake, si kwa kuangalia cheti gani anacho.

Ukimsikiliza unaweza kuona hana elimu rasmi, unaweza kuona kuwa pengine elimu rasmi ingeweza kumsaidia kujieleza vizuri zaidi, kuwa na class, kuondoa maneno ya shombo na kujikita kwenye mada.

Lakini, pengine hayo maneno ya shombo ndiyo branding yake, ndiyo marketing strategy yake.

Juzi nilimkuta dogo mmoja anaangalia movie moja, based on real events, "Confessions of a Cam Girl" inamuonesha binti Mmarekani kakataa kwenda chuo kikuu, anataka kuwa influencer online, anasema Kim Kardashian alifanikiwa bila ya kwenda chuo. Wazazi wake walikuwa wanamsisitiza aende chuo, yeye anasema wazazi wamepitwa na wakati ulimwengu huu watu wanafanya wanachotaka na elimu inapatikana popote, si lazima kwenda chuo.

Sasa labda Dotto Magari naye kashajitafuta kajipata anaona chuo hakina umuhimu kwake yeye anatakiwa kufundisha watu aina mpya ya marketing, hizo degrees za marketing zilizopo vyuoni zote zinakwenda kizamani wakati yeye ndiye anakwenda na marketing ya kileo ya kimtandao, ndiyo maana tunamuongelwa yeye na si msomi wa marketing hapa.

Mimi sipendi maneno controversial ya shombo, na Dotto inawezekana anasumbuliwa na saikolojia ya "Sizitaki Mbichi Hizi". Lakini, najua kuwa hayo maneno ni sehemu ya haki ya mtu ya kujieleza, ni haki yake ya kikatiba na kibinadamu.

Kama wewe ni msomi kweli, unatakiwa kujua uhuru huu na kupuuza maneno haya. Zaidi, unatakiwa kuchukua maneno ya Dotto kama changamoto kwamba elimu inatakiwa kupimwa kwa matokeo yake, na kama kweli Dotto kawashinda wasoni katika kutangaza biashara, basi hao wasomi inawezekana kawashinda kweli, wajitafakari.

Of course inawezekana Dotto ni chawa tu kapanda kwa uchawa na si mpiganaji kihivyo, hapo napo inabidi wasomi wamjibu kwa facts.
Jf kennedy aliwah sema
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    47.1 KB · Views: 5
Mpaka wafanyabiashara wanakimbiliia kwa hakina Dotto Magari na wao kujitamba ni kwa sababu hakuna marketing firms za kuweza kutangaza biashara zao.

Sasa kwanini Dotto Magari asiongee ukweli elimu imekusaidia nini kama wafanyabiashara wanaona kumlipa yeye kufanya promotion unalipa kwao kuliko wewe unaejidai umesoma.

Kubwa zaidi hakuna sheria aliyovunja katoa mawazo kwa mtazamo wake (huna ulazima wa kukubalina) nae anao uhuru huo. Unaweza ku-counter argue mtazamo wake.

Mi ndio maana nikipata wasaa nawaendea kule kwenye jukwaa la ‘stories of change! Kuwapa mapande yao wajinga wajinga.

Dotto hana kosa kwa kutoa opinion yake ambayo ni ya msingi kwa upande wangu.

Kuna mtu anaweza tają ‘marketing firm’ hata moja Tanzania. Sasa kwanini asiseme ukweli.
 
Mjumbe hauwawi, wasomi wengi wa bongo(ukimtoa Fernandez wa, Nala, Melo wa JF) hawana akili, huyu jamaa hajasoma kama anavyosema, lakini ana social skills kubwa, kwenye jamii,kuliko kijana mwenye Masters, kwanza waliosoma madegree hawawezi hata kujichanganya na watu wa chini, kuongea lugha ya mtaani, itakayoelekweka kwa mama ntilie, bodaboda, nk, huwa wanajitenga,
Elimu yetu inatukalilisha vitu kibao, ambavyo havina matumizi kwrnye maisha ya wanacnhi wa kawaida, Engineer, inabidi aweze kuwa na kujinyunbylisha kadri atakavyo, awe MC, mchungsji, DJ, mpiga debe nk, kama umesoma vitu vigumu harafu unazidiwa na asiesoma kufanya vitu rahisi,hapo kuna shida!
Miaka hiyo, nimeanza, chuo, mwaka wa pili, nikarudi kwa, anko, likizo,nikakutana na binamu yangu katoka kijijini, yupo hapa dar anauza mitumba, siku moja, akaniambia nimsaidie kuandika business plan, anataka kutafuta mtaji afungue biashara ya sterionery na vibanda vya kupiga simu,
Nilibaki nimetoa macho! Sijuhi kitu!
Akaona akasome English course, akaandika mchanganuo wake, akaomba pesa kwa ndugu, marafiki, akafungua biashara zake, akaacha kuuza mitumba, akawa anasimamia stationery zake,akahama pale hm, akapanga kimara,subuh anafungua ofc zake, anakagua mahesabu, anaacha wadada wanaendelea kufanya kazi, akaenda zake Kulala hm,
Mwaka mmoja tu, alikuwa ameishatengeneza ukwasi wa kutosha, akaagiza container ya computer afungue internet cafe, akapoteza maisha!
Kijana wa std 7,lakini nilikuwa na mpiga vizinga vya pocket money, boom likichelewa!
Wasomi wa bongo, stop winning, and shape up, we are disgrace, alichoongea Doto magari, kina ukweli ndsni yake,
Ni afrika tu unakuta anasema wasomi vbya leo tumeona hata wanasiasa wasiokua wasomi maaamuzi yao yaliyokua yakipumbavu Taifa bila wasomi ni sawa na taifa la mahayawani
 
Sahihi kabisa madaktari popote mlipo akitokea mwambieni akachemshr pesa zake anywe kama dawa msimpe tiba yeyote
***** hii umemaliza kabisa hiz habari za za kutokuheshimu professional za watu naliona hata makazini na uzuri watz tumerogeka instagram basi tunaona waliosoma hopeless hili nakataaa yeye dotto kwa upande wake marketing strategies yake inamlipa tuliona watu wengi wakija km yeye mfano. Mzee mpili,mzee wa liquid strategy yake nzuri ila sio longterm itafika time kila mtu atakua hana habari nae please tusidharau elimu kmyeye anaona haifai mtt wake asimpeleke shule amrisishe makelele
 
Kwa hiyo malaya na mashoga na majambazi yenye pesa yana akili? Kujiuza na ujambazi ni kipimo cha akili kuwa mtu anayo?
Mkuu, Tofautisha akili na elimu. Elimu ni chakula cha akili, inaipa misuli akili. Unaweza kuwa na elimu isiyo na msaada kwako na ukawa jambazi na ukawa na pesa. Ila huwezi kuwa na akili usiwe na pesa. Hakuna mtu mwenye akili ombaomba.
 
Kwa hiyo malaya na mashoga na majambazi yenye pesa yana akili? Kujiuza na ujambazi ni kipimo cha akili kuwa mtu anayo?
Mkuu, Tofautisha akili na elimu. Elimu ni chakula cha akili, inaipa misuli akili. Unaweza kuwa na elimu isiyo na msaada kwako na ukawa jambazi na ukawa na pesa. Ila huwezi kuwa na akili usiwe na pesa. Hakuna mtu mwenye akili ombaomba.
 
Mkuu, Tofautisha akili na elimu. Elimu ni chakula cha akili, inaipa misuli akili. Unaweza kuwa na elimu isiyo na msaada kwako na ukawa jambazi na ukawa na pesa. Ila huwezi kuwa na akili usiwe na pesa. Hakuna mtu mwenye akili ombaomba.

Pesa kiasi gani sasa ndio unakuwa na akili? Mwenye mshahara wa laki 5 na mwenye mshahara wa milioni 5 hapo mwenye akili ni huyo wa mshahara mkubwa?
 
huwezi kuwa na akili usiwe na pesa. Hakuna mtu mwenye akili ombaomba.
Hapa pia unaonyesha una tatizo la kielimu kwenye watu waliosoma pesa haiko katika vigezo vya kupima akili ya mtu

Kipimo cha akili kinaitwa

Intelligence quotient​

Na katika vigezo vya kupima pesa haimo

Lakina wewe kwa kuwa elimu huna endelea kuamini kuwa pesa ndio kipimo cha akili
 
Pesa kiasi gani sasa ndio unakuwa na akili? Mwenye mshahara wa laki 5 na mwenye mshahara wa milioni 5 hapo mwenye akili ni huyo wa mshahara mkubwa?
Hapana. Kuwa na pesa si kipimo cha akili sababu unaweza lipwa mshahara bila kutumia akili, ila hakuna mwenye akili asiye na pesa sababu akili itakuonyesha pa kuipata pesa.
 
Hapa pia unaonyesha una tatizo la kielimu kwenye watu waliosoma pesa haiko katika vigezo vya kupima akili ya mtu

Kipimo cha akili wa kinaitwa

Intelligence quotient​

Na katika vigezo vya kupima pesa haimo

Lakina wewe kwa kuwa elimu huna endelea kuamini kuwa pesa ndio kipimo cha akili
Sijui kwanini hamuwezi kutofautisha elimu na akili? Hakuna mtu asiye na tatizo la elimu. Hata wewe kuna vitu huna elimu navyo.

Huwezi kuwa na akili usiwe na pesa, akili siku zote itakuonyesha ilipo pesa.
 
Anachosema ni ukweli mtupu.

Mimi nikikutana na mtu ana hela kuliko mimi basi pia atakua na akili kunizidi, maana haiwezekani uwe na akili halafu ukose hela, narudia tena haiwezekani.

Huna hela = Huna akili.
Haiwezekani hizo pesa akawa amerithi, ameiba au ameuza dawa za kulevya??
 
Back
Top Bottom