Hii kauli Dotto Magari kuhusu Elimu. Anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa kupotosha na kutukana umma

Hii kauli Dotto Magari kuhusu Elimu. Anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa kupotosha na kutukana umma

Kwa sababu hajafanya kosa lolote ametumia haki yake ya kikatiba na kibinadamu tu kujieleza.

Na ingawa hajajieleza vizuri sana, hoja yake ya kimsingi ina mantiki.

Ukiondoa maneno ya shombo yote na dharau zake, hoja yake ya kimsingi ni kupingana na logical fallacy ya "argument from authority" ya kuheshimu sana vyeti, elimu rasmi.

Kimsingi anasema yeye ni salesman mzuri kuliko wasomi wengi waliosomea marketing and sales kwenye elimu rasmi.

Na unaweza kupima hilo kwa kuangalia matokeo ya kazi zake, si kwa kuangalia cheti gani anacho.

Ukimsikiliza unaweza kuona hana elimu rasmi, unaweza kuona kuwa pengine elimu rasmi ingeweza kumsaidia kujieleza vizuri zaidi, kuwa na class, kuondoa maneno ya shombo na kujikita kwenye mada.

Lakini, pengine hayo maneno ya shombo ndiyo branding yake, ndiyo marketing strategy yake.

Juzi nilimkuta dogo mmoja anaangalia movie moja, based on real events, "Confessions of a Cam Girl" inamuonesha binti Mmarekani kakataa kwenda chuo kikuu, anataka kuwa influencer online, anasema Kim Kardashian alifanikiwa bila ya kwenda chuo. Wazazi wake walikuwa wanamsisitiza aende chuo, yeye anasema wazazi wamepitwa na wakati ulimwengu huu watu wanafanya wanachotaka na elimu inapatikana popote, si lazima kwenda chuo.

Sasa labda Dotto Magari naye kashajitafuta kajipata anaona chuo hakina umuhimu kwake yeye anatakiwa kufundisha watu aina mpya ya marketing, hizo degrees za marketing zilizopo vyuoni zote zinakwenda kizamani wakati yeye ndiye anakwenda na marketing ya kileo ya kimtandao, ndiyo maana tunamuongelwa yeye na si msomi wa marketing hapa.

Mimi sipendi maneno controversial ya shombo, na Dotto inawezekana anasumbuliwa na saikolojia ya "Sizitaki Mbichi Hizi". Lakini, najua kuwa hayo maneno ni sehemu ya haki ya mtu ya kujieleza, ni haki yake ya kikatiba na kibinadamu.

Kama wewe ni msomi kweli, unatakiwa kujua uhuru huu na kupuuza maneno haya. Zaidi, unatakiwa kuchukua maneno ya Dotto kama changamoto kwamba elimu inatakiwa kupimwa kwa matokeo yake, na kama kweli Dotto kawashinda wasoni katika kutangaza biashara, basi hao wasomi inawezekana kawashinda kweli, wajitafakari.

Of course inawezekana Dotto ni chawa tu kapanda kwa uchawa na si mpiganaji kihivyo, hapo napo inabidi wasomi wamjibu kwa facts.
 
Ukizimgatia ya huyo kijana na yakakuingia akilini basi mnafanana akili.

Wewe na yeye wale wale.
 
Anachosema ni ukweli mtupu.

Mimi nikikutana na mtu ana hela kuliko mimi basi pia atakua na akili kunizidi, maana haiwezekani uwe na akili halafu ukose hela, narudia tena haiwezekani.

Huna hela = Huna akili.

This falls in line with "tatizo hii nchi wanawapa uongozi watu wajinga." Huwa sikubaliani na hii kauli. Mtu timamu hawezi kubali kuongozwa na mjinga. Kama unaona anayekuongoza ni mjinga, chances are wewe ni mjinga zaidi yake. Mf. ukiambiwa panda gari ila dereva wa hilo gari ni kichaa utapanda? Kama huwezi kwanini ukubali kuongozwa na mtu mjinga?

As much as hatuwapendi hawa viongozi mpiga mwingi, Mwigulu, Jiwe nk ila hawakufika hapo bahati mbaya. Hawakuokotwa tu barabarani na kupewa uongozi walipambana na kuwashinda wapinzani wao on the way up. They are more than likely kuwa na uwezo kuliko wapinzani wao. Siwatetei hiyo ndo reality.
 
Tatizo hamna ugunduzi wowote nyie wenye elimu kubwa , yaani kifupi hata profesa hana maajabu maana anatafuta pesa kwa kuajiriwa na dili .

Fanyeni ugunduzi wa maana kurahisisha maisha lazima heshima iwepo , leo Mo dewji ana heshima kuliko hata wahadhiri wa vyuo .
 
Imekuuma,sio kwa povu Hilo.
Punguzeni kunata wasomi,unaenda ofisi ya Umma unamkuta ofsa kavimba kama puto la pasaka,unamsalimia hata hajibu anakwambia nikusaidie nini?!
Hivi mkiwa humble mnapungukiwa nini!
Mnanuka madeni,mnapata wapi ubavu wa kudharau watu!
 
😂😂😂😂 wasomi wanatokwa povu.

Tumia elimu yako ikupe pesa sasa.

Ila deep down jamaa anaumia kwa kutosoma ama lah alishawahi kuumia kwa kukosa elimu. Na ninyi wenye elimu mkamkaanga sana kisa hana kitu na elimu hana.

Leo kajipata na yeye anatema nyongo dadeki, kama una elimu kweli huwezi kuumia kwa maneno yake.
Ukiona unaumia kwa maneno ya huyu jamaa basi kweli huna akili kama asemavyo.
 
Mjumbe hauwawi, wasomi wengi wa bongo(ukimtoa Fernandez wa, Nala, Melo wa JF) hawana akili
Ukiumwa unaharisha huko mbona unasumbua madaktari si ujitibu mwenyewe bwege wewe kama kusoma hakuna maana
Daktari asingesoma huyo Doto magari angetibiwa na hayo magari yake takataka toka majalala ya Japan anayouza huyo bwege?

Ndege anazopanda ATCL mfano marubani wasomi wasingesoma angeendesha yeye? Au treni ya SGR yeye angeendesha kama kusingekuwepo na watu walioamua kusoma?

Madaktari huyo bwege Dotto magari akija hosputalini kutibiwa na yeyote anayedharau wasomi hadharani iwe bungeni nk msimtibu na mwambieni kabisa elimu haina maana na kusoma hakuna maana ikiwemo.kusomea udaktari nenda kwa wasiosoma wenzio wakakutibu bwege wewe

Wasomi ifike mahali mchachamae kuleta heshima kwenye elimu

Uzuri wanaoponda elimu wengi popular .madaktari wasubirini hospitalini watakuja tu wafanyizieni
 
Doto Magari ni msanii pia anachoongea ni kweli, wasomi muwe wapole kwa sababu wanaona upigaji wenu kwenye taasisi za serikali, pia anaona woga wenu wa maisha ambapo wasomi kila siku wanalia hawana ajira na wakati wamesoma, wengi na kusoma kote hawawezi kujiajiri , biashara zimewashinda Dotto Magari anawatia hasira ya mafanikio ili wasomi wenye diploma, degree, masters waamke katika kusaka fursa hata za kawaida badala ya kulalia.
 
Back
Top Bottom