Hii kauli Dotto Magari kuhusu Elimu. Anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa kupotosha na kutukana umma

Hii kauli Dotto Magari kuhusu Elimu. Anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria kwa kupotosha na kutukana umma

Kwangu namuona ni mtu ambaye amejaaliwa kipato lkn ana majivuno pia
Ameshasahau aliyemjalia hayo ni Allah,hivyo anajiona ni ujanja wake
Hakuna Allah aliyemjalia chochote, hizo ni porojo tu za watu wenye akili ndogo kujifariji.
 
Sijui kwanini hamuwezi kutofautisha elimu na akili? Hakuna mtu asiye na tatizo la elimu. Hata wewe kuna vitu huna elimu navyo.

Huwezi kuwa na akili usiwe na pesa, akili siku zote itakuonyesha ilipo pesa.
Unaweza kuwa na akili na usiwe na pesa, sio kila mtu mwenye akili anajali kuhusu utajiri.
 
Hapana. Kuwa na pesa si kipimo cha akili sababu unaweza lipwa mshahara bila kutumia akili, ila hakuna mwenye akili asiye na pesa sababu akili itakuonyesha pa kuipata pesa.
Nadhani unaongelea akili ya ujasiriamali. Kuna watu wana akili za uvumbuzi ama teknolojia ila hawana pesa nyingi sababu hawako oriented kwenye akili ya ujasiriamali
 
Neema zinawapumbaza watu wengi. Japo muda wowote mambo yanabadilika,. Aliyejuu anaweza kushuka na wachini akapanda juu. Kwahyo haistahili kumdharau mtu kwasababu yeyote
Ni nani huyu? Kazi yake ni ipi au ni maarufu kwa kitu gani?
 
Maskini akipata bana....huyo ela kazipatia ukubwani ndomana anakua limbukeni mtu aliyekulia kwenye Hela hawezi kuwa Na ulimbukeni wa hivyo Ila waliozipatia ukubwani ndo Hua washamba sana
Ni nani huyu? Kazi yake ni ipi? Umaarufu wake umetokana na nini?
 
sasa unampinga doto wewe una v8 wewe?
akili na elimu nivitu viwili tofauti doto anaakili bali elimu yadarasani ndio amekosa

wasomi wengi hela hawana mwenye hela Labda aingie kwenye siasa akaibe hela zawananchi
😃😃😃😃
 
Unaweza kuwa na akili na usiwe na pesa, sio kila mtu mwenye akili anajali kuhusu utajiri.
Utajiri unapimwaje? Nilicho na uhakika nacho ni huwezi kuwa na akili usiwe na pesa au ukawa ombaomba, ila unaweza kuwa na elimu na usiwe na pesa na ukachakaaa chakari choka mbaya na una degree ya sales and marketing. With exception za magonjwa, ulemavu, uzee n.k ukiwa na akili hutokosa pesa.
 
Haya tuendelee kukaa kwenye foleni isiyotembea inayoenda kuwachoga watoto kufit kwenye mfumo wa CCM.
 
Wasomi wengi wapumbavu wajinga wajinga wasiokuwa na akili Wala maarifa zero chini ya zero hamna kilakitu

Hao wasomi wetu wametusaidia Nini Sasa Hadi Leo? Unapompinga mpinge Kwa hoja sio majungu
 
Nguvu inayofanya kazi hapa ni suala la elimu ya darasani ikihusishwa na namna ilivyo na msaada kwa vijana. Huyo doto ni kama njiti iliyoshika moto kwenye nyasi kavu. Moto utasambaa sio kwa sababu njiti ina nguvu ila sababu nyasi ni kavu.
Hahahahaha ,watu wa hivyo kaa nao mbali mkuu ,unaeza piga kofi mtu ukaonekana umemaindi
 
Mna

Mnamkuza tu bure hana m

Miaka ya nyuma ajira zilikuwa tele watu wasiosoma waliitwa wakimbia umande na wazembe
Na ndo hiki kinachomuumiza huyu jamaa, miaka ya nyuma alisota na waliosoma aliwaona malaika, huyu bwana huenda anatamani kua na hiyo elimu leo kesho ila ndo ivo anajiona kachelewa na hajui asome nini.

Hana kitu kinachontisha msomi anaejitambua na anaejijua anataka nini na afanye nini ili akipate.

Wahanga wakubwa wa maneno yake ni graduates wa miaka ya hivi karibuni na hawajajipata kivyovyote.
 
Back
Top Bottom