ppl0
Askofu Mwanamapinduzi anesema amekamatwa na Polisi kutokana na kauli yake ya uchochezi "Rais amekataliwa na Mungu"
Ametoa ufafanuzi huo Ukurasani kwake X
Namuuliza askofu Mwanamapinduzi; enzi za shujaa Magufuli ungethubutu kutamka maneno hayo?
Jumaa Mubarak.
Wezi walimchafua sana Magufuli kupitia wanaharakati na Wapinzani wakadanganyika wakaingia mkenge. Genge la wapigaji ndani ya CCM lilifanya juu Chini kumchafua Magufuli kwa namna yoyote na kwa gharama yoyote.
Mbona Masudi Kipanya alikua anamchora Magufuli katika picha ya Katuni yenye bichwa kubwa na sura mbaya kila siku lakini Magufuli hajawahi kumtisha wala kukasirika zaidi ya Kucheka na kusema wazi kuwa Kipanya anamchora sana kwenye katuni?
Mtu kusema kuwa Mungu amemkata fulani sio Kosa kwa sababu serikali haifanyi kazi kwa maelekezo ya dini wala imani bali katiba.
Mwacheni JPM apunzike.
System ilifanya kazi yake enzi zote tangu mkoloni mpaka leo lakini wakati wa JPM system ikasingiziwa kuwa inatumwa na JPM. Rais Magufuli enzi zake alitangaza vita dhidi ya wala Rushwa wakubwa ,wezi wa mali za umma, mashoga , Wauza madawa ,magaidi,majambazi ,wazembe n.k.
Sasa rais anapotangaza maadui wa taifa kwenye rasilimali na fedha za umma ni wazi kuwa kinachofuata ni vyombo vyake vya dola kuwadhibiti wanaotaka kukwamisha vita hiyo.
Hua namshangaa sana Hata Lisu japo Sasa namkubali ila linapokuja suala la kusema kuwa JPM aliwatuma watu wakampige risasi ndio naona kuwa anapoteza sana dira na kutafuta huruma kwa wapigaji ambao tayari wapo madarakani na wapo na mama. Na sera yake na msimamo wake uko wazi kuwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake. Na ni wazi kuwa mwenye kamba ndefu atakula zaidi.
Kamba ya Wapinzani ni mikutano ya hadhara ambayo haizuii wenye kamba ndefu kula . Mikutano haijazuia chochote
Kwa sasa ama mtu asimame kama JPM apate kura nyingi za wazalendo au amponde JPM amsaidie mama Kushinda na kundi lake la wapigaji na madalali wa kuiza nchi.
Hakuna Rais aliyepingwa kama JPM tangu uhuru.Tatizo likawa kuwa wananchi wengi walimwelewa sana JPM wakiwemo viongozi wa dini . Wapinzani walikosa sera wenyewe kwa sababu wananchi walimkubali sana ndio maana watu walikua hawataki kushiriki kwenye maandamano .
Na kwa mfano mama leo hawezi kuzuia maandamano tanganyika mana hayana madhara kwake zaidi ya kutumika kumponda JPM tuu na kupinga kuuzwa kwa bandari ambayo imeshauzwa na watu wanasafri na kukopa bila kikomo. Maandamano hajabadili chochote.
Wanyonge leo wanaandamano mana hawaoni mtetezi na sio kwa sababu CCM inataka waandamane ila Jamii iko tayari kufanya lolote .
Upepo umelazimisha walaji wawape wananchi angalau uhuru wa kulia njaa wakati wao wanakula.