Pre GE2025 Hii kauli ya Askofu Mwanamapinduzi 'Rais kukataliwa na Mungu' angeweza kuitoa enzi za Hayati Magufuli?

Pre GE2025 Hii kauli ya Askofu Mwanamapinduzi 'Rais kukataliwa na Mungu' angeweza kuitoa enzi za Hayati Magufuli?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Askofu Mwanamapinduzi anesema amekamatwa na Polisi kutokana na kauli yake ya uchochezi "Rais amekataliwa na Mungu"
Amechochea kwenye jambo alilowasha nani? Ni yeye wa kukamatwa au mwanzilishi
 
Huyo mchungaji sijui askofu ni mpumbavu sana,mungu katujaalia rais mpenda raia wake,msikivu na anayejari maslahi ya watanzania wote.

Mungu atupe nini tena?
Mikumi tena kwa mama Samia
Asingeli wafukuza Wamaasai kutoka Ngorongoro kama anazo hizo sifa unazombebesha.
 
View attachment 3011165

Askofu Mwanamapinduzi anesema amekamatwa na Polisi kutokana na kauli yake ya uchochezi "Rais amekataliwa na Mungu"

Ametoa ufafanuzi huo Ukurasani kwake X

Namuuliza askofu Mwanamapinduzi; enzi za shujaa Magufuli ungethubutu kutamka maneno hayo?

Jumaa Mubarak.
Magu alikuwa shujaa wa nani? Wanasiasa walipotea na wengine kupigwa moto acha waliokimbia nchi, watu waliporwa pesa zao ktk account zao na maduka ya kubadilishia pesa kutekwa, mo alitekwa na hadi leo hakuna watuhumiwa, vijana wa hivyo walipewa madaraka makubwa wakaunda vikisi vya kuteka na kutesa watu na kuwapoteza huo ndio ushujaa? Asante Mungu kwa kutuondolea boriti ktk maisha yetu.
 
Hayoyote yamefanyika kwa maslahi mapana ya.taifa,tumuunge mkono rais wetu
Mapana yapi ilihali gharama za gas,mishahara mifinyu, hospital bila dawa,kadi ya mama mjamzito sasa inalipiwa fedha,uhaba wa watumishi hospitals,shuleni hakuna walimu kulingana na mahitaji au unazungumzia taifa la Zanzibar?
 
ppl0

Askofu Mwanamapinduzi anesema amekamatwa na Polisi kutokana na kauli yake ya uchochezi "Rais amekataliwa na Mungu"

Ametoa ufafanuzi huo Ukurasani kwake X

Namuuliza askofu Mwanamapinduzi; enzi za shujaa Magufuli ungethubutu kutamka maneno hayo?

Jumaa Mubarak.


Wezi walimchafua sana Magufuli kupitia wanaharakati na Wapinzani wakadanganyika wakaingia mkenge. Genge la wapigaji ndani ya CCM lilifanya juu Chini kumchafua Magufuli kwa namna yoyote na kwa gharama yoyote.

Mbona Masudi Kipanya alikua anamchora Magufuli katika picha ya Katuni yenye bichwa kubwa na sura mbaya kila siku lakini Magufuli hajawahi kumtisha wala kukasirika zaidi ya Kucheka na kusema wazi kuwa Kipanya anamchora sana kwenye katuni?

Mtu kusema kuwa Mungu amemkata fulani sio Kosa kwa sababu serikali haifanyi kazi kwa maelekezo ya dini wala imani bali katiba.

Mwacheni JPM apunzike.
System ilifanya kazi yake enzi zote tangu mkoloni mpaka leo lakini wakati wa JPM system ikasingiziwa kuwa inatumwa na JPM. Rais Magufuli enzi zake alitangaza vita dhidi ya wala Rushwa wakubwa ,wezi wa mali za umma, mashoga , Wauza madawa ,magaidi,majambazi ,wazembe n.k.
Sasa rais anapotangaza maadui wa taifa kwenye rasilimali na fedha za umma ni wazi kuwa kinachofuata ni vyombo vyake vya dola kuwadhibiti wanaotaka kukwamisha vita hiyo.

Hua namshangaa sana Hata Lisu japo Sasa namkubali ila linapokuja suala la kusema kuwa JPM aliwatuma watu wakampige risasi ndio naona kuwa anapoteza sana dira na kutafuta huruma kwa wapigaji ambao tayari wapo madarakani na wapo na mama. Na sera yake na msimamo wake uko wazi kuwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake. Na ni wazi kuwa mwenye kamba ndefu atakula zaidi.
Kamba ya Wapinzani ni mikutano ya hadhara ambayo haizuii wenye kamba ndefu kula . Mikutano haijazuia chochote

Kwa sasa ama mtu asimame kama JPM apate kura nyingi za wazalendo au amponde JPM amsaidie mama Kushinda na kundi lake la wapigaji na madalali wa kuiza nchi.


Hakuna Rais aliyepingwa kama JPM tangu uhuru.Tatizo likawa kuwa wananchi wengi walimwelewa sana JPM wakiwemo viongozi wa dini . Wapinzani walikosa sera wenyewe kwa sababu wananchi walimkubali sana ndio maana watu walikua hawataki kushiriki kwenye maandamano .

Na kwa mfano mama leo hawezi kuzuia maandamano tanganyika mana hayana madhara kwake zaidi ya kutumika kumponda JPM tuu na kupinga kuuzwa kwa bandari ambayo imeshauzwa na watu wanasafri na kukopa bila kikomo. Maandamano hajabadili chochote.

Wanyonge leo wanaandamano mana hawaoni mtetezi na sio kwa sababu CCM inataka waandamane ila Jamii iko tayari kufanya lolote .

Upepo umelazimisha walaji wawape wananchi angalau uhuru wa kulia njaa wakati wao wanakula.
 
Mpaka alimwita dikteta uchwara, itakuwa ulikuwa mdogo au ulikuwa bado unasoma chuo cha utumishi wa Umma Tabora


JPM alipingwa na kutukanwa sana ndani ya Chama chake na hata wapinzani .

Wapinzani waliopambania rasilimali za nchi hii kwa muda mrefu waliamua kumuunga mkono na kurudi CCM akiwemo Dr.Slaa.
Huyu mama hajapata upinzani mkubwa mana alishatoa uhuru wa kila mtu kula kwa urefu wa kamba yake . Hata wapinzani sasa wanacheza urefu wa kamba yao.
 
Magu alikuwa shujaa wa nani? Wanasiasa walipotea na wengine kupigwa moto acha waliokimbia nchi, watu waliporwa pesa zao ktk account zao na maduka ya kubadilishia pesa kutekwa, mo alitekwa na hadi leo hakuna watuhumiwa, vijana wa hivyo walipewa madaraka makubwa wakaunda vikisi vya kuteka na kutesa watu na kuwapoteza huo ndio ushujaa? Asante Mungu kwa kutuondolea boriti ktk maisha yetu.
Alikua na huruma sana.

Hivi unafikiri akitokea rais ambaye sio mwanachama wa CCM kwa katiba hii na akaamua kuitumia vizuri kuna Mwizi wa mali za umma atabaki hai ?!!

Hiiii, yaani kuna vichwa kama 2000 hivi vinatakiwa viliwe ili nchi inyooke na iwe na maendeleo kama Ujeruman ndani ya miaka 20.

Unasema JPM kateka watu wakati alikua na huruma sana mpaka wakina Nanilii waliokua wanamtukana mitandaoni bado wapo na wanaendeleza upigaji huku wakiwakejeli watu wanyonge ?
 
1.Mishahara gani umaongelea wewe mkuu,samia kaingia madarakani ndani ya mwezi mmoja wa utawala wake mimi mwalimu nilipanda darajaa ambalo nimelitumikia toka enzi za kikwete hadi magufuli na baadae samia,mwaka huu serikali yake imetangaza kupandisha madaraja watumishi,kwangu mimi ndani ya utawala wa samia wa miaka 3 nitakuwa nimepanda madaja mawili,hakuna rais aliyewahi kufanya jambo hili.

2.kuhusu gasi nadhani hili halihitaji tochi kujua kuwa mama anapambana ili kuhakikisha nchi yetu inatumia nishati safi,hujasikia bajeti ya mwaka huu kuwa kuna punguzo la mitungi ya gasi kwa asilimia nyingi tu?

Watanzania tunataka rais gani kama huyu bado tunamlalamikia,binafsi naona ni wachache tu ndo hawamwelewi,sidhani kma hata asilimia 0.1% wanafika

Mikumi tena kwa mama samia
Mapana yapi ilihali gharama za gas,mishahara mifinyu,
 
Hivi huwa mnazungumzia Mungu gani? Maana utasikia fulani chaguo la Mungu, mara fulani kakataliwa na Mungu mara fulani kafyekelewa na Mungu hata sielewi huyo Mungu wa aina gani.
 
Back
Top Bottom