Hii kazi ya Customer Care inabidi uwe na Uvumilivu wa hali ya juu

Hii kazi ya Customer Care inabidi uwe na Uvumilivu wa hali ya juu

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Nawaonea sana huruma watu wanaofanya kazi kitengo cha customer care.

Hawa watu wanabeba lawama za Mataasisi na Maofisi.

Mteja anapiga simu anaporomosha matusi, kejeli na lawama kibao. Alafu unakuta huyo mteja ndio mwenye kosa.

Mimi nimewai kuona Boyfriend wa mteja alikopa pesa kwenye App moja ya Benki, hizi App za Miamala ya simu ya Benk moja maarufu. Pesa ndefu tu akajitumia. Sasa si unajua tena, pesa ikawa inaingia kwenye account hiyo ikikaaa tu, watu wa Benk wanakata mdogo mdogo deni lao.

Kucheki balance anaona pesa imepungua na hakutoa chochote wala kufanya transactions. Akawapigia Customer Care wa Benki hiyo akawapolomoshea matusi na kuwaita wezi huku kapanic akitishia kuama Benki.

Ikabidi apewe maelekezo ya kucheki Benki Statement ku-track matumizi ya pesa. Kuangalia vizuri anakuta kuna miamala ilifanywa na Boyfriend bila yeye kuwa na taarifa. Ambapo wakati Boyfriend anafanya miamala hakukuwa na salio hivyo akapata mkopo wa dharula, ambao unakatwa pole pole siku pesa ikiingia. Kesi ikarudishwa kwa Boyfriend.

Hapo customer care ashakula matusi, kampuni ishatukanwa na kadharika, alafu kosa ni la mteja, au watu wa Tech ndani ya kampuni. Ila kwa sababu Customer Care ndio mtu wa kwanza kuzungumza na mteja anakula matusi.
 
Kwa hiyo. .. tukusadieje ? Watu wasiajiriwe kama customer care? Kila kazi na changamoto zake
 
Ni kama useme kucheza mpira ni kazi ngumu kuliko zote kwa sababu muda wote unakimbia Uwanjani. Hapana, kila kazi kama ni professional nina imani umeshakuwa trained kwa changamoto tarajiwa. Wakati wewe unamuonea huruma mchezaji, yeye hilo si tatizo kwake, pengine anawaza kwa nini hawanipi pasi.

Lile tabasamu la air hostes wa Emirates au Qatar airways si la kuzaliwa, wamekuwa trained. Changamoto ni kufanya kazi ambayo huna skills nayo. Kuna customer care anakupa majibu kwa utulivu in professional way mpaka unajiona mjinga na utashangaa mteja mkorofi anarudi tena kupata huduma tena akiwa mpole. Jambo lisilovumilika ni kuhatarisha maisha ya mtoa huduma.
 
Kuna kipindi changu Cha ujana nilikuwa napiga maksudi akipokea mwanamke namtongoza tuu.

Utaskia kaka kama unachangamoto nyingine nikusaidie.
 
Kwa hiyo. .. tukusadieje ? Watu wasiajiriwe kama customer care? Kila kazi na changamoto zake
Kuna sehemu nimeomba msaada wako... punguza makasiriko la sivyo utalembwa kama jina lako
 
Mteja anapiga simu anaporomosha matusi, kejeli na lawama kibao. Alafu unakuta huyo mteja ndio mwenye kos
Mteja wana aina hiyo, unamtafute nje ya ofisi ili mshikishane adabu.

Watz wakiwa kwenye vyombo vya mawasiliano wanajifanya wana ujasiri wa kuandika au kuongea chochote kile.
 
Ni kama useme kucheza mpira ni kazi ngumu kuliko zote kwa sababu muda wote unakimbia Uwanjani. Hapana, kila kazi kama ni professional nina imani umeshakuwa trained kwa changamoto tarajiwa. Wakati wewe unamuonea huruma mchezaji, yeye hilo si tatizo kwake, pengine anawaza kwa nini hawanipi pasi.

Lile tabasamu la air hostes wa Emirates au Qatar airways si la kuzaliwa, wamekuwa trained. Changamoto ni kufanya kazi ambayo huna skills nayo. Kuna customer care anakupa majibu kwa utulivu in professional way mpaka unajiona mjinga na utashangaa mteja mkorofi anarudi tena kupata huduma tena akiwa mpole. Jambo lisilovumilika ni kuhatarisha maisha ya mtoa huduma.
Kazi ya kudili na psychology ya mtu ni ngumu kuliko ya mpira, ndio maana timu ikifeli anatimuliwa kocha ambaye kazi yake ni kuweka utimamu wa akili na maarifa

Unazungumzia kazi ya Air hostess ambayo haifanani na ya kupiga simu ya huduma kwa wateja.... ukiona mpaka mfu anapiga simu huduma kwa wateja ujue huyo mtu ana shida au kero inayomsumbua, na mtu mwenye kero inayomsumbua anafatuta ufumbuzi tunajuaga namna wanavyokuwa na kumtuliza kwa kum-solvia shida zake wakati yeye analalamika juu yenu sio poa.... Air Hostess hapokei kero, yeye ni kusaidia tu baadhi ya vitu kwenye ndege na kutoa maelekezo
 
Kazi yangu Ina changamoto mnoo naona bora nitukanwe kama Hao
Kazi hipi hiyo?

Usiombe kazi ambayo hujui ugumu wake, Customer care wana moyo, usipokuwa na skills unaweza tukana wateja ukafukuzwa kazi, maana unakuta siku hiyo wewe nae una hasira zako alafu kuna mteja aelewi maelekezo na anakukashifu
 
Kuna kipindi changu Cha ujana nilikuwa napiga maksudi akipokea mwanamke namtongoza tuu.

Utaskia kaka kama unachangamoto nyingine nikusaidie.
Sasa uoni kuwa kazi ya Customer Care ni ngumu... unakuta huyo dada kasha jam ila miiko ya kazi inamkataza hasikuzingue
 
Mteja wana aina hiyo, unamtafute nje ya ofisi ili mshikishane adabu.

Watz wakiwa kwenye vyombo vya mawasiliano wanajifanya wana ujasiri wa kuandika au kuongea chochote kile.
Hahahah yeah ni changamoto wateja wakiwa kwenye simu wanajiona wako dunia nyingine, wanaporomosha matusi sana

Muda mwingine wanatakiwa wawe wanaomba mapambano na watu wanaowatusi.

Kazi ya kudili na kero na malalamiko ya raia ni ngumu sana kama hauna moyo
 
Acha kudharau kazi, unaweza kukuta unayofanya wewe ndio ya kishoga
Mimi kazi yangu wewe ukija kufanya lazima unye maana inahusisha kunyanyua vitu vizito, kukimbia na kuchimba

Ukikaza misuli tu nya ileee
 
nimefanya kazi miaka 4 pale azam tv ni matatizo tupu fulu kula matusi ya wateja.
 
Back
Top Bottom