Mwafrikaazania
Senior Member
- Aug 6, 2026
- 109
- 211
Hakuna kazi rahisi.Kazi ya kudili na psychology ya mtu ni ngumu kuliko ya mpira, ndio maana timu ikifeli anatimuliwa kocha ambaye kazi yake ni kuweka utimamu wa akili na maarifa
Unazungumzia kazi ya Air hostess ambayo haifanani na ya kupiga simu ya huduma kwa wateja.... ukiona mpaka mfu anapiga simu huduma kwa wateja ujue huyo mtu ana shida au kero inayomsumbua, na mtu mwenye kero inayomsumbua anafatuta ufumbuzi tunajuaga namna wanavyokuwa na kumtuliza kwa kum-solvia shida zake wakati yeye analalamika juu yenu sio poa.... Air Hostess hapokei kero, yeye ni kusaidia tu baadhi ya vitu kwenye ndege na kutoa maelekezo
Ni kila kazi ina changamoto yake. Bottom line, una skills za hiyo kazi? Umekuwa trained, unajua kuwa kazi yeyote inayohusisha kuoanana au ku-deal na mteja moja kwa moja inahitaji maarifa? Unajua kuna kampuni zimeajiri kabisa Mtu mwenye cheo cha customer experience Manager!
Ukilalamika wewe customer care, vipi kwa Mtu mwenye matatizo ya akili aliyepo Mirembe. Au unahisi wanatakiwa wapelekwe kama Ng'ombe. Ukifika hapo ndiyo utaona madaktari wanawahudumia na hawaoni kero na kila siku hawakosi kwenda kazini.
Kwani wakati unapewa kazi ya customer care ulijua watakuja Watu waungwana muda wote. Kuna wateja wagumu pia, ndiyo maana unatakiwa uwe na skills za kuwasikiliza wote. Na kwa taarifa tu, Wateja wagumu huwa baadaye wanakuwa Wateja loyal sana. Heri mteja mlalamishi na mbishi, akielewa atarudi tena, kuliko Mteja wa 'hewala bwana' ambaye akiondoka unaweza usimpate tena.
Shida ya hiyo kada ya 'customer care' imejaa Watu wasiyo na skills, akipata Mteja mropokaji naye anakuwa emotional. Fikiria pia, una mgonjwa hospitali, matibabu huyaelewi na gharama pia huzielewi, unalalamika na kukasirika, jukumu la daktari na cashier au yeyote yule anayekuhudumia anatakiwa akutulize na kukusikiliza. Ndivyo wanavyotakiwa kuwa. Je, akikujibu hovyo unafikiri hali itakuwaje?