Hii kazi ya Customer Care inabidi uwe na Uvumilivu wa hali ya juu

Hakuna kazi rahisi.
Ni kila kazi ina changamoto yake. Bottom line, una skills za hiyo kazi? Umekuwa trained, unajua kuwa kazi yeyote inayohusisha kuoanana au ku-deal na mteja moja kwa moja inahitaji maarifa? Unajua kuna kampuni zimeajiri kabisa Mtu mwenye cheo cha customer experience Manager!

Ukilalamika wewe customer care, vipi kwa Mtu mwenye matatizo ya akili aliyepo Mirembe. Au unahisi wanatakiwa wapelekwe kama Ng'ombe. Ukifika hapo ndiyo utaona madaktari wanawahudumia na hawaoni kero na kila siku hawakosi kwenda kazini.

Kwani wakati unapewa kazi ya customer care ulijua watakuja Watu waungwana muda wote. Kuna wateja wagumu pia, ndiyo maana unatakiwa uwe na skills za kuwasikiliza wote. Na kwa taarifa tu, Wateja wagumu huwa baadaye wanakuwa Wateja loyal sana. Heri mteja mlalamishi na mbishi, akielewa atarudi tena, kuliko Mteja wa 'hewala bwana' ambaye akiondoka unaweza usimpate tena.

Shida ya hiyo kada ya 'customer care' imejaa Watu wasiyo na skills, akipata Mteja mropokaji naye anakuwa emotional. Fikiria pia, una mgonjwa hospitali, matibabu huyaelewi na gharama pia huzielewi, unalalamika na kukasirika, jukumu la daktari na cashier au yeyote yule anayekuhudumia anatakiwa akutulize na kukusikiliza. Ndivyo wanavyotakiwa kuwa. Je, akikujibu hovyo unafikiri hali itakuwaje?
 
Kuna siku nilikuwa nanunua nguo kariakoo.katika ile kuchagua nikawa nimeangalia nyingi narudisha kumbe yule muuzaji akawa anakereka akasema mwishowe utazikagua zote sasa.Nakamwambia kwani kuna tatizo nikiziangalia zote?nilipomuona amenuna nikaacha kununua halafu nikanunua duka la jirani yake.customer care inahitaji uvumilivu
 
Kazi ya kudeal na watu mahali popote kuanzia kwenye familia,kazini n.k inahitaji Emotional and Social Intelligence iliyoshiba haswaa
 
Yeah ni kweli
 
Kazi ya kudeal na watu mahali popote kuanzia kwenye familia,kazini n.k inahitaji Emotional and Social Intelligence iliyoshiba haswaa
Umenena vyema... hakuna kazi ngumu kama kazi ya kuhusika na mtu moja kwa moja hasa ya customer care
 
Of coz hakuna kazi rahisi, ila ugumu unazidiana viwango... kuna kazi nyingine Unaweza kuta mtu kaajiriwa tangu kijana mpaka anazeeka yupo hapo, ila uwezi kukuta customer care hasa hawa wanaopokea kero za wananchi kama wa mitandao ya simu kaajiriwa tangu kijana mpaka uzeeni anafanya kazi hiyo... mtu anafanya kazi ya kupokea matusi tangu asubuhi mpaka jioni 😄

Unaweza ukawa trained vizuri lakini hiyo haiondoi ugumu wa kazi.... mtu anakuja na Negative energy, na unajua hata customer care naye ni binadamu anaweza akawa na vitu vinavyomsibu... mteja analalamika wewe mixture matusi, mfano hawa wa mitandao ya simu wanatukanwa sana 😄. Unaweza kupoteza uvumilivu kama utakutana na watu 10 wa aina hiyo, mwanzo Unaweza ukawa unawajibu vizuri ila kadri muda unavyozidi kwenda au miaka inavyozidi kwenda na wewe unakuwa faded na matusi... Unaweza jikuta siku umetoa kauli ya kukwaza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…