Hii kero ni kwa shule hii Tu au huko kwengine yapo haya?

"Maazimio ya kikao, wazazi walikubaliana kila mzazi kuchangia 80,000/= elfu themanini ili kuwapa motisha waalimu wapate kutimiza majukumu Yao vizuri. Na hii ilipendekezwa itolewe kwa awamu mbili."

👆👆

Sasa kama mlikubaliana, malalamiko ni ya kazi gani?

Halafu elfu 80 inakushindaje mzazi?

Unataka mtoto asome bure bila gharama?
 
Kuna ku-play party kwengine kwa kukwepa majukumu yao.
 
Haya si malalamiko waalimu wengi wanakosa uwajibikaji kichaka kinakuwa hiki. Mwanafunzi unamfundisha, kama mwalimu wewe ni mtu wa Kwanza kufahamu changamoto za mwanafunzi wako. Ikitokea anafanya vibaya na wewe unaona suluhu kumuambia mzazi ajiongeze ili mwanae apambaniwe ina maana mwalimu kashindwa kutekeleza majukumu yake kifupi hatoshi.
 
Kam A wazazi wamekubali wewe inakuuma nini?
 
Kam
A wazazi wamekubali wewe inakuuma nini?
Kama wazazi wangekuwa Wanakaa na watoto wao na kuzungumza nao juu ya utekelezaji wa kile kilichoazimiwa, hakuna mzazi ambaye angekuwa tayari. Sababu kinachotekelezwa hakiakisi na uhalisia. Shule za serikali baadhi ya waalimu si wawajibikaji
 
Sekta zingine mnawapa sana rushwa mkitaka huduma na wanapiga sana pesa za serikali iwe ni kwa wizi wa pesa au vifaa ila ikiwa walimu tu maneno yanakuwa mengi.

Hii ni double standard

Waacheni nao wale kwa urefu wa kamba bimkubwa alisharuhusu
 
Mshahara mdogo
Kama wazazi wangekuwa Wanakaa na watoto wao na kuzungumza nao juu ya utekelezaji wa kile kilichoazimiwa, hakuna mzazi ambaye angekuwa tayari. Sababu kinachotekelezwa hakiakisi na uhalisia. Shule za serikali baadhi ya waalimu si wawajibikaji
Unataka wawajibike kivip? Hata mimi nisingewajibika?
 
Waalimu waliajiliwa kwa kazi ipi?
Dogo mambo mengine kama huyaelewi piga kimya. Au kama toto lako ni kilaza halifundishiki, waache watoto wa wengine wasome. Sie wengine tunalipa zaidi ya laki moja na hatulalamiki, bali tunaamini watoto wetu wanaweza kuwa akina Peof. Kabudi au Prof. Kindiki wa kesho!
 
Kwa vile walikubaliana wazazi na walipanga wao siyo tatizo.
Kinachotakiwa waalimu sasa waitendee haki hiyo 80,000 ya kila mzazi.
Wafanye wajibu wao kwa kuajiri kisha ziada kwa hiyo pesa ya ziada.
 
Walichofanya wazazi na walimu ni sahihi sana elf 80 ni hela ndogo kwa program nzuri kama hiyo
Acha mterezo mtoto ulimzaa Kwa ihari yako mwenyewe usione kama ni mzigo acha kutafuta unafuu penye hakuna toa elf 80 .
 
mbona unasema wazazi walikubaliana wao wenyewe inamaana kuna muhtasari wa kikao.Muwege mnachangia hoja kwenye vikao unaona kitu hukubaliani nacho unakataa sio unavunga badae unaanza kulalama
 
Mkuu shida si wazazi kukubaliana je ilikuwa sahihi kwa waalimu hili Jambo kuli- address kwa wazazi? Kwa nini Kwanza wasingeangalia kwanza weakness Yao ipo wapi?
ulikuwepo kwenye kikao?
 
Asante MKUBWA, tatizo si pesa MKUBWA! Tatizo waalimu kuja na wazo la mzazi ajiongeze ili Mtoto wake apambaniwe. Hii ni wazi kabisa waalimu hawawajibiki ipasavyo katika kutekeleza majukumu Yao bila mzazi kuwa chochote kitu.
 
Sekta zingine mnawapa sana rushwa mkitaka huduma na wanapiga sana pesa za serikali iwe ni kwa wizi wa pesa au vifaa ila ikiwa walimu tu maneno yanakuwa mengi.

Hii ni double standard

Waacheni nao wale kwa urefu wa kamba bimkubwa alisharuhusu
hamna cha urefu sema walimu wanafanya favour tu,mfano mitihani inayotakiwa kufanyika ni midterm,terminal na annual ila unakuta walimu wanatoa test za mara kwa mara na kufundisha mda wa ziada ila malalamiko yako pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…