Hii kero ni kwa shule hii Tu au huko kwengine yapo haya?

Hii kero ni kwa shule hii Tu au huko kwengine yapo haya?

Hilo Mimi sina shida nalo mkuu. Shule nyingi sasa hivi waalimu wengi hawafundishi wanachoangalia wao salio linasoma mwisho wa mwezi basi.
Shule nyingi walimu hawafundishi
UNA UHAKIKA?
LETE USHAHIDI
 
Haya si malalamiko waalimu wengi wanakosa uwajibikaji kichaka kinakuwa hiki. Mwanafunzi unamfundisha, kama mwalimu wewe ni mtu wa Kwanza kufahamu changamoto za mwanafunzi wako. Ikitokea anafanya vibaya na wewe unaona suluhu kumuambia mzazi ajiongeze ili mwanae apambaniwe ina maana mwalimu kashindwa kutekeleza majukumu yake kifupi hatoshi.
Niliwai kuandika humu kuwa walimu wapo kwenye passive aggressive
Ndugu mzazi mwalimu wa sasa hawezi kuacha kwenda kuuza kiduka chake soko la jioni akae anampambania mwanao mwenye kichwa kigumu saaaaaana kama chako
 
Ni shule wasichana mabwepande (Tumaini). Waalimu wamebuni chanzo cha kijiongezea kipato maisha yasonge.

Hii ni shule ya boarding kwa wasichana, kidato cha tano na sita. Mwaka huu baada ya shule kufunguliwa mwezi August, wale wanafunzi waliotoka kidato cha tano na kuingia kidato cha sita, walifanyiwa mitihani ya majaribio.

Matokeo ya majaribio hayo hayakuwa mazuri Sana,ndipo waalimu walipoona fursa ya kuwashirikisha wazazi kwa kuita kikao cha wazazi ili wazazi waone ni namna gani kwa kushirikiana na waalimu wapate ufumbuzi wake.

Baada ya waalimu kuiwasilisha hoja kwa wazazi,waalimu waliondoka na kuacha wazazi wajadili namna gani mzuri watakayoona inafaa ya kuwawezesha waalimu WAWAPAMBANIE WATOTO WAO.

Maazimio ya kikao, wazazi walikubaliana kila mzazi kuchangia 80,000/= elfu themanini ili kuwapa motisha waalimu wapate kutimiza majukumu Yao vizuri. Na hii ilipendekezwa itolewe kwa awamu mbili.

Nirudi kwenu wadau wa jamiiforums,
Je ni sahihi kweli kwa hiki walichokifanya hawa waalimu? Inakuwaje jukukumu linalohusiana na wao mzigo anakuja kubebeshwa mzazi? Utendaji kazi wa mwalimu kwa mwamafunzi wake unaonekana kwenye matokeo.

Upowapi uwajibikaji na uchapakazi wao waalimu hawa? Hivi wakaguzi wa hizi shule mpo? Mishahara wanayolipwa waalimu hawa inatokana na Kodi za hawa wazazi ambao leo wamegeuzwa ng'ombe wa maziwa. Hebu naomba waalimu timizeni wajibu wenu. Tupo kwenye maisha ya kupita tu kama unaona kipato hakitoshi tafuta kwengine tuwahurumie hawa wazazi wanapambana na mengi.
kama tabia zako ndio hiz je hao wanafnz watakuaje , kwann usingemalz malalamiko yako kweny kikao unaleta umbea hku, na ukachange zaid
 
Huwaliza sana hili swala la tuition kwa wanafunzi, sijawahi kupata majibu sahihi. Hivi ni kwa nini hao walimu wasitie nguvu ya tuition kwenye vipindi vya kawaida?
UMESHAWAI KUJIULIZA

Kwanini huo muda wa tuition mwalimu pia asiende kufanya kazi nyingine ya kumuingizia kipato ?

au kwanini huo muda wa tuition mwalimu Asipumzike zake na mke/ Mme Wake ?
 
UMESHAWAI KUJIULIZA

Kwanini huo muda wa tuition mwalimu pia asiende kufanya kazi nyingine ya kumuingizia kipato ?

au kwanini huo muda wa tuition mwalimu Asipumzike zake na mke/ Mme Wake ?
Jibu ni moja tu, umewahi kuishi na watu wenye mfumo wa akili iliyojifunga?(closed mind system)
 
Gharama ya tsh 80000/- ni gharama ya topic mbili tu za advance kwa tuition mtoto anayesoma advance,kwahiyo Kama mmetajiwa sh 80000/- remedial( extra time) Kwa masomo yote 3 na civics advance kwa mwaka,maana hujasema ni muda gani,hayo ni malipo madogo Sana ,ndugu mzazi lipa,kazi ya ualimu ,set up ya vipindi mada haziishi ,Ila extra Kama hizo madam zinatembea
 
Mkuu,elewa kuwa sipingi maamuzi ya wazazi. Ninachokiongelea ni kitendo cha waalimu kuona wao si sehemu ya tatizo na kuja na hoja kuwa mzazi ajiongeze ili Mtoto wako apambaniwe. Kama mwalimu umefikia hatuwa hii ni wazi kabisa majukumu yako ya uwalimu yamekushinda na hutoshi kwa hiyo nafasi.
hayo ungeyaongea kwenye kikao
 
Back
Top Bottom