Hii kero ni kwa shule hii Tu au huko kwengine yapo haya?

Huu utaratibu upo kwenye shule nying za advance,pia wazaz huchanga pesa za kuiba mtihani wa taifa
 
Ungekuepo kwenye Kikao Cha Wazazi, hoja Yako hii ingejibiwa huko huko.

Siku ingine Mkiitwa kwenye vikao vya Wazazi shuleni, muwe mnaenda.
 
Hao wazazi wangeongeza kidogo hata iwe laki mbili na elfu tisini na tisa hivi ili walimu waweze kusema mpe mruke katikati ya mwezi.
 
Mkuu unajipa uhakika gani kwa kutoa hiyo 80 Mtoto atafanya vizuri? Suala sio pesa. Ni utayari waalimu wetu wa kujitoa kwa ajili ya majukumu yao.
Wewe una uhakika gani mwanao ana utayari wa kusoma?
 
Mkuu shida si wazazi kukubaliana je ilikuwa sahihi kwa waalimu hili Jambo kuli- address kwa wazazi? Kwa nini Kwanza wasingeangalia kwanza weakness Yao ipo wapi?
Umesema jaribio lilitolewa baada ya shule kufunguliwa (form five hawakuwa wamesoma lolote). Je walipewa mtihani wa level ipi? Kama ni level ya advance, walimu wahojiwe inakuwaje umpime mtu kwa kitu ambacho hakifahamu? Kama walipewa mtihani wa olevel, walimu wako sahihi
 
Hilo Mimi sina shida nalo mkuu. Shule nyingi sasa hivi waalimu wengi hawafundishi wanachoangalia wao salio linasoma mwisho wa mwezi basi.
Orodhesha hizo Shule peleka kwa Mkuu wa Mkoa.
 
Njaa njaa na janja janja tu, majukumu yao yatatimizwa kwa kuongezewa 80,000?

Hapa ndo mimi na mtoa mada tunajiuliza, vinginevyo wawe waalimu wa ziada.
 
Dah! Ndugu Mzazi unazingua aisee...!
Na hiyo ni A level ...
Hiyo michango ishazoeleka kabisa O level...kwa minajili ya kuwasaidia watoto wenu.
Hili ndo tatizo la kupenda vya bure.

Siasa ndo zimetufikisha hapa. Shule zinafunguliwa mpya nyingi hizi za Advanced girls lakini hazina Walimu.

Walimu wako mtaani, wanapokuja jitolea wazazi mnaitwa ili mchangie walimu wapate pesa ya dagaa na unga hutaki...

Ewe mzazi vipii!??🤷🤷😞😞😞
Mbona unashangaza.

Alafu upande wa pili huoni huo ni mtego wa kuwawajibisha walimu. Nyie andikeni muhtasari, gongeni sahihi, pelekeni kopi bodi ya shule kwa DEO na Mkurugenzi alafu msubiri matokeo ya wenenu. Yasipobadilika huo muhtasari utawawajibisha walimu. Toeni hela.
 
1. Baadhi ya Watoto siku hizi wanaoenda advance Wana uwezo mdogo Sana tofauti na zamani, bila kutumia nguvu ya ziada, muda wa ziada hawawez kufauli

2. Sylubus ya Advance ktk mosomo mengi ni ndefu, bila walimu kujiongeza kufundisha jioni na usiku ni ngumu Sana kumaliza topics.

3. Wapo walimu wa kujitolea, Wana moyo wa kufundisha ila wanaitaji hela watatue changamoto za maisha yao .

4. Mitihani ya mara kwa mara, ya ndani na nje (Joint) ina mchango mkubwa ktk kuongeza ufaulu WA mtoto.

Ili kufaulisha watoto lazima shule iwe na mikakati binafsi, nje ya ratiba ya serikali na ili shule iweze kutekeleza mipango hiyo lazima kuwe na FEDHA. Kama hakuna chochote cha ziada kinafanyika kuongeza ufaulu basi shule imefanya utapeli maana walimu wanaopata mishahara kwa Kazi hiyo.
 
If you think education is expensive try ignorance
 
Sasa wewe jamaa...wazazi si wamekubaliana shida Iko wapi ? Kwani wameshurutishwa? Tena wenyewe bila kushinikizwa.... brother hapo hakuna shida.....walipe tu
 
Mkuu shida si wazazi kukubaliana je ilikuwa sahihi kwa waalimu hili Jambo kuli- address kwa wazazi? Kwa nini Kwanza wasingeangalia kwanza weakness Yao ipo wapi?
Usitoe Mkuu ..kaaa tulia ...mwanao utamfundisha mwenyewe masomo ya ziada na kiada.
 
80k unaona nyingi ngoja mwanao afeli arudi mkae nae apo nyumbani sasa.
Na sio mwalimu unamuona anakuwa kaajiriwa
 
Ni ya serikali mkuu
""Maazimio ya kikao, wazazi walikubaliana kila mzazi kuchangia 80,000/= elfu themanini ili kuwapa motisha waalimu wapate kutimiza majukumu Yao vizuri. Na hii ilipendekezwa itolewe kwa awamu mbili.""

Umeielewa hii aya???

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Maazimio ya kikao, wazazi walikubaliana kila mzazi kuchangia 80,000/= elfu themanini ili kuwapa motisha waalimu wapate kutimiza majukumu Yao vizuri. Na hii ilipendekezwa itolewe kwa awamu mbili.


Wazazi waombe mitihani ya wanao kama wamefeli kweli au ni gemu, kila mwanafunzi anajua uandishi wake.

Upigajiiiiiiiiiiii huu kibokoooooo 🤣🤣🤣🙌🏽 na inasikitisha pia
 
Mtoa mada Mimi naona umeshajibiwa ni haki wazazi kuwajibika na sio tatizo kabisa kwa wazazi kuchangia 80

Hoja ya walimu kutotimiza majukumu yao Haina mashiko: unajua jinsi walimu wanavyofanya kazi?

Unajua mwisho wa kazi ni saa ngap? Mimi ninaona huku mtaani wanafunzi wengi wanataka saa 11 jioni alafu mwisho wa kazi ni saa tisa na nusu, je huo muda wa ziada analipwa na nani?

Umesema kuna wanafunzi walifanyishwa mtihani wakafeli japo naamini kuna walio faulu, je huyo aliyefaulu amefundishwa na walimu tofauti ? Na darasa tofauti?

Kumbuka kuna wanafunzi wanatumia muda mchache wa kuelewa na wengine wanatumia muda mwingi kuelewa


Mzazi , usiwalalamikie walimu hawatimizi majukumu yao wewe hapa ndo unataka kukwepa kutimiza majukumu yako kwenye kikao halali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…