Bachelor ll
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 4,106
- 6,678
Shule nyingi walimu hawafundishiHilo Mimi sina shida nalo mkuu. Shule nyingi sasa hivi waalimu wengi hawafundishi wanachoangalia wao salio linasoma mwisho wa mwezi basi.
Niliwai kuandika humu kuwa walimu wapo kwenye passive aggressiveHaya si malalamiko waalimu wengi wanakosa uwajibikaji kichaka kinakuwa hiki. Mwanafunzi unamfundisha, kama mwalimu wewe ni mtu wa Kwanza kufahamu changamoto za mwanafunzi wako. Ikitokea anafanya vibaya na wewe unaona suluhu kumuambia mzazi ajiongeze ili mwanae apambaniwe ina maana mwalimu kashindwa kutekeleza majukumu yake kifupi hatoshi.
wew ulitoa wazo ganMkuu shida si wazazi kukubaliana je ilikuwa sahihi kwa waalimu hili Jambo kuli- address kwa wazazi? Kwa nini Kwanza wasingeangalia kwanza weakness Yao ipo wapi?
kama tabia zako ndio hiz je hao wanafnz watakuaje , kwann usingemalz malalamiko yako kweny kikao unaleta umbea hku, na ukachange zaidNi shule wasichana mabwepande (Tumaini). Waalimu wamebuni chanzo cha kijiongezea kipato maisha yasonge.
Hii ni shule ya boarding kwa wasichana, kidato cha tano na sita. Mwaka huu baada ya shule kufunguliwa mwezi August, wale wanafunzi waliotoka kidato cha tano na kuingia kidato cha sita, walifanyiwa mitihani ya majaribio.
Matokeo ya majaribio hayo hayakuwa mazuri Sana,ndipo waalimu walipoona fursa ya kuwashirikisha wazazi kwa kuita kikao cha wazazi ili wazazi waone ni namna gani kwa kushirikiana na waalimu wapate ufumbuzi wake.
Baada ya waalimu kuiwasilisha hoja kwa wazazi,waalimu waliondoka na kuacha wazazi wajadili namna gani mzuri watakayoona inafaa ya kuwawezesha waalimu WAWAPAMBANIE WATOTO WAO.
Maazimio ya kikao, wazazi walikubaliana kila mzazi kuchangia 80,000/= elfu themanini ili kuwapa motisha waalimu wapate kutimiza majukumu Yao vizuri. Na hii ilipendekezwa itolewe kwa awamu mbili.
Nirudi kwenu wadau wa jamiiforums,
Je ni sahihi kweli kwa hiki walichokifanya hawa waalimu? Inakuwaje jukukumu linalohusiana na wao mzigo anakuja kubebeshwa mzazi? Utendaji kazi wa mwalimu kwa mwamafunzi wake unaonekana kwenye matokeo.
Upowapi uwajibikaji na uchapakazi wao waalimu hawa? Hivi wakaguzi wa hizi shule mpo? Mishahara wanayolipwa waalimu hawa inatokana na Kodi za hawa wazazi ambao leo wamegeuzwa ng'ombe wa maziwa. Hebu naomba waalimu timizeni wajibu wenu. Tupo kwenye maisha ya kupita tu kama unaona kipato hakitoshi tafuta kwengine tuwahurumie hawa wazazi wanapambana na mengi.
UMESHAWAI KUJIULIZAHuwaliza sana hili swala la tuition kwa wanafunzi, sijawahi kupata majibu sahihi. Hivi ni kwa nini hao walimu wasitie nguvu ya tuition kwenye vipindi vya kawaida?
Jibu ni moja tu, umewahi kuishi na watu wenye mfumo wa akili iliyojifunga?(closed mind system)UMESHAWAI KUJIULIZA
Kwanini huo muda wa tuition mwalimu pia asiende kufanya kazi nyingine ya kumuingizia kipato ?
au kwanini huo muda wa tuition mwalimu Asipumzike zake na mke/ Mme Wake ?
hayo ungeyaongea kwenye kikaoMkuu,elewa kuwa sipingi maamuzi ya wazazi. Ninachokiongelea ni kitendo cha waalimu kuona wao si sehemu ya tatizo na kuja na hoja kuwa mzazi ajiongeze ili Mtoto wako apambaniwe. Kama mwalimu umefikia hatuwa hii ni wazi kabisa majukumu yako ya uwalimu yamekushinda na hutoshi kwa hiyo nafasi.