Hii kiitifaki imekaaje?

Hii kiitifaki imekaaje?

Rais inabidi asindikizwe na Vigogo wa ngazi za juu, sio Waziri
View attachment 2008034
Everything in protocol process is properly arranged, well taken care of and documented, nothing is bad luck or oversight. Kiongozi yeyote wa chini ya Rais anapoagizwa na Rais kumsaidia kwenye jambo fulani/kumuwakilisha basi ujuwe haendi kama kiongozi tu wa kawaida bali anaenda na delegated power ya Rais. Kwahiyo hapo President wetu haagwi na Waziri tu bali anaagwa na Waziri aliyekasimiwa sehemu ya mamlaka ya Rais kufanya shughuli hiyo ya kumuaga mgeni. Uki-mess na huyo Waziri ume-mess na power ya Rais mwenyewe.

Mwaka 2009 wakati Mhe. Raila amewaburuza The Hague Rais Uhuru, DP Ruto and sundries, Mhe. Raila ali-lobby kwamba ili haki kutendeka kwa wahanga wa vita ya uchaguzi ya 2008, Uhuru na Ruto wasiende The Hague kama viongozi wa kitaifa wakati wao ni washukiwa wakuu. GoK ikaelemewa na kuridhia hoja ya Mhe. Raila ambayo ilibadili asilani sura ya itifaki ya viongozi hao wa kitaifa, hivyo washukiwa hao walisindikizwa na motorcade ya top brass toka Ikulu hadi JKIA na walipofika tu pale walinyang'anywa bendera zao, walinyang'anywa wapambe wao (wakapewa ulinzi wa kawaida) na kule The Hague hawakupokelewa kama Rais na kama Makamu Rais bali kama watu wa kawaida washukiwa wa mauaji ya halaiki, hivyo hawakukagua gwaride kule ughaibuni. Ila walipokanyanga tu ardhi ya Kenya pale JKIA walipokelewa kama viongozi wa kitaifa na kurudishiwa itifaki zote. Kwahiyo walipoenda The Hague walienda kama raia watuhumiwa hawakuenda kama viongozi (rais na makamu Rais), walilazimishwa na hoja ya Mhe. Raila (iliyopitishwa) kubakisha Urais wao na Umakamu Rais wao Kenya wanapoenda The Hague.

Wakati Mhe. Raila ameteuliwa na Katibu Mkuu wa UN kwenda kumshawishi Laurent Gbagbo (aliyeshindwa uchaguzi) aondoke Ikulu kumpisha Rais halali aliyeshinda uchaguzi Alassane Ouattara, Gbagbo alimtishia Raila kwamba ole wake akanyage nchi yake, atahakikisha ndege aliyopanda Raila inachakazwa vipande vipande na akitua salama ataishia jela ugenini, hivyo akamtaka Raila achague maisha au mauti, UN ilipopata habari hizo ika-cancel mpango huo, Raila akailaumu UN na kusema ANAENDA KIVYAKEVYAKE BILA KUTUMWA NA JUMUIYA YOYOTE YA KIMATAIFA NA AKAMWAMBIA GBAGBO MUDA ATAOTUA, FLIGHT No., HOTELI ATAYOLALA, MUDA ATAOINGIA IKULU, NA KUMTAKA GBAGBO KUANDAA MABEGI YAKE KUONDOKA IKULU, Gbagbo akashangaa ujasiri wa ina hii, kama mchezo, Raila akatua kama alivyopanga na akanyimwa kuingia Ikulu akasema hatoki nchi hiyo hadi Gbagbo ameondoka Ikulu, Gbagbo akalegea na kumruhusu Raila kuonana naye, message binafsi ya Raila haikubadilika mbele ya Gbagbo, akamwambia anazo siku 7 tu za kuondoka Ikulu kwa heshima kinyume chake mapinduzi na jela vinamhusu, akamwabia anaenda kumshawishi Alassane Ouattara aunde serikali akiwa ukimbizini na iendeshe Ivory Coast tokea ukimbizini. Ndani ya siku nne Gbagbo akatangaza jeshi kuondoka mitaani kurudi kambini na yeye anaondoka Ikulu. Raila alitangaza kwamba sasa yatosha Madespots kuendesha Afrika.

Mhe. Raila hana mfano duniani.
 
Misri ni chimbuko la Uislamu, ni mwanachama wa OIC, ni mwanachama wa Arab League. Kwa 90% ni Islamic Nation. (Ingawa hata Mozambique ni mwanachama wa OIC, pia Israel ni mwanachama wa OIC japo Wayahudi wako 75%, ila Israel imejiunga OIC kwa maslahi ya Kiulinzi na Usalama (kufanya ujasusi kwa nchi za Kiarabu ili iweze kukaa salama))
Maneno mengi pointi zero.....misri sio nchi ya kiislam(Islamic republic),kama Iran na Saudi Arabia
 
There's obviously a significant age difference here which kind of explains everything. Relatively speaking, the older woman would be more likely to die from COVID-19, thus the face mask. However, and sans COVID-19, the older woman is sure as hell expected to use the hijab to cover her feminine body parts because the hijab gets to hide a lot of her physical shortcomings under guise of religious tradition.
 
Labda wamechungulia ratiba yake inaonesha atarudi tena, hivyo kusindikizwa next round[emoji23]
 
Kuhusu ushungi na hizo kanzu kwa Misri na Tunisia siyo sehemu ya vazi la dini ya kiislamu bali ni nguo kama nguo zingine! Miaka kabla ya ukoloni wamisri walipata mavazi hayo kutoka Maka, Tehran na Baghdad hivyo dini ilipokuja huku kwenu Waarabu weusi ndiyo mnaweza kuua asiyevaa!

Ni kama vile nchi za baridi wanavyovaa warm jackets 🧥 ili kuepuka baridi kali AU wakati wa theluji!

Halafu na waanzilishi wa mavazi hayo ni kwa ajili ya joto jangwani na upepo wenye mchanga!

Kuhusu, usindikizwaji na Waziri wa uhamiaji ina sababu nyingi majukumu kwa viongozi waandamizi.


Kuona kuwa Mgeni hana lolote la maana bali wamepoteza muda na pesa za kumlisha kwa siku 3 zote!

Wamempuuzia kama wamisri daima walivyo na tabia ya kupuuzia wageni wengine wengi.
 
Maneno mengi pointi zero.....misri sio nchi ya kiislam(Islamic republic),kama Iran na Saudi Arabia
Nimesema kwa 90%. Sijasema ni taifa kamili la Kiislam kwa 100%. Mkristo anaweza kuwa Rais Misri? Mkristo anaweza kuwa Rais Zanzibar? Dhiang' gi jamb iye!
 
Kuona kuwa Mgeni hana lolote la maana bali wamepoteza muda na pesa za kumlisha kwa siku 3 zote!
mj-spits.gif
 
Nimesema kwa 90%. Sijasema ni taifa kamili la Kiislam kwa 100%. Mkristo anaweza kuwa Rais Misri? Mkristo anaweza kuwa Rais Zanzibar? Dhiang' gi jamb iye!
Acha kuchanganya jifunze hiki kitu........Indonesia ndio nchi yenye waislam wengi ila sio nchi ya kiislam.
Iran,Saudi Arabia,ni nchi za kiislam.
Jifunze.
Mkristo gani ameshawahi kugombea urais/umakamo wa urais Zanzibar?,umewahi soma hata basic ya hesabu za probability?
Zanzibar kuna waislam wengi ila sio nchi ya kiislam.
Kuna nchi za kiislam duniani,ila hakuna nchi ya kikristo hata moja,hata Vatican
 
Acha kuchanganya jifunze hiki kitu........Indonesia ndio nchi yenye waislam wengi ila sio nchi ya kiislam.
Iran,Saudi Arabia,ni nchi za kiislam.
Jifunze.
Mkristo gani ameshawahi kugombea urais/umakamo wa urais Zanzibar?,umewahi soma hata basic ya hesabu za probability?
Zanzibar kuna waislam wengi ila sio nchi ya kiislam.
Kuna nchi za kiislam duniani,ila hakuna nchi ya kikristo hata moja,hata Vatican
Zambia ni taifa la Kikristo. Australia inatambua Ukristo zaidi. Uingereza Waziri Mkuu lazima awe Anglican. Malkia (ukoo wa kifalme) mwenyewe ni Anglican. Aidha, nikufundishe kwa kukusahihisha kwamba Vatican ni ya Kikristo siyo ya Kiislam.
 
Back
Top Bottom