Everything in protocol process is properly arranged, well taken care of and documented, nothing is bad luck or oversight. Kiongozi yeyote wa chini ya Rais anapoagizwa na Rais kumsaidia kwenye jambo fulani/kumuwakilisha basi ujuwe haendi kama kiongozi tu wa kawaida bali anaenda na delegated power ya Rais. Kwahiyo hapo President wetu haagwi na Waziri tu bali anaagwa na Waziri aliyekasimiwa sehemu ya mamlaka ya Rais kufanya shughuli hiyo ya kumuaga mgeni. Uki-mess na huyo Waziri ume-mess na power ya Rais mwenyewe.
Mwaka 2009 wakati Mhe. Raila amewaburuza The Hague Rais Uhuru, DP Ruto and sundries, Mhe. Raila ali-lobby kwamba ili haki kutendeka kwa wahanga wa vita ya uchaguzi ya 2008, Uhuru na Ruto wasiende The Hague kama viongozi wa kitaifa wakati wao ni washukiwa wakuu. GoK ikaelemewa na kuridhia hoja ya Mhe. Raila ambayo ilibadili asilani sura ya itifaki ya viongozi hao wa kitaifa, hivyo washukiwa hao walisindikizwa na motorcade ya top brass toka Ikulu hadi JKIA na walipofika tu pale walinyang'anywa bendera zao, walinyang'anywa wapambe wao (wakapewa ulinzi wa kawaida) na kule The Hague hawakupokelewa kama Rais na kama Makamu Rais bali kama watu wa kawaida washukiwa wa mauaji ya halaiki, hivyo hawakukagua gwaride kule ughaibuni. Ila walipokanyanga tu ardhi ya Kenya pale JKIA walipokelewa kama viongozi wa kitaifa na kurudishiwa itifaki zote. Kwahiyo walipoenda The Hague walienda kama raia watuhumiwa hawakuenda kama viongozi (rais na makamu Rais), walilazimishwa na hoja ya Mhe. Raila (iliyopitishwa) kubakisha Urais wao na Umakamu Rais wao Kenya wanapoenda The Hague.
Wakati Mhe. Raila ameteuliwa na Katibu Mkuu wa UN kwenda kumshawishi Laurent Gbagbo (aliyeshindwa uchaguzi) aondoke Ikulu kumpisha Rais halali aliyeshinda uchaguzi Alassane Ouattara, Gbagbo alimtishia Raila kwamba ole wake akanyage nchi yake, atahakikisha ndege aliyopanda Raila inachakazwa vipande vipande na akitua salama ataishia jela ugenini, hivyo akamtaka Raila achague maisha au mauti, UN ilipopata habari hizo ika-cancel mpango huo, Raila akailaumu UN na kusema ANAENDA KIVYAKEVYAKE BILA KUTUMWA NA JUMUIYA YOYOTE YA KIMATAIFA NA AKAMWABIA GBAGBO MUDA ATAOTUA, FLIGHT No., HOTELI ATAYOLALA, MUDA ATAOINGIA IKULU, NA KUMTAKA GBAGBO KUANDAA MABEGI YAKE KUONDOKA IKULU, Gbagbo akashangaa ujasiri wa ina hii, kama mchezo, Raila akatua kama alivyopanga na akanyimwa kuingia Ikulu akasema hatoki nchi hiyo hadi Gbagbo ameondoka Ikulu, Gbagbo akalegea na kumruhusu Raila kuonana naye, message binafsi ya Raila haikubadilika mbele ya Gbagbo, akamwambia anazo siku 7 tu za kuondoka Ikulu kwa heshima kinyume chake mapinduzi na jela vinamhusu, akamwabia anaenda kumshawishi Alassane Ouattara aunde serikali akiwa ukimbizini na iendeshe Ivory Coast tokea ukimbizini. Ndani ya siku nne Gbagbo akatangaza majeshi kuondoka mitaani kurudi kambini na yeye anaondoka Ikulu. Raila alitangaza kwamba sasa yatosha Madespots kuendesha Afrika.
Mhe. Raila hana mfano duniani.