Hii kolablo ya Mpina na Gwajima ni kitisho kwa CCM maslahi

"Kizungumkuti cha mgombea.. Huyu wa sasa kwa jinsi alivyochafuka ndani na nje ya nchi je atafaa? Au watafute mbadala"? Nani
Kwa maslahi ya nchi atafutwe mbadala tu
Hilo pekee ni jambo zito sana kwa chama hicho.
Huyu aliye chafuka anashikiliwa na Genge, lililokinyakuwa chama cha CCM kuwa chombo cha kufanyia uchafu.

Hili Genge ni la waimba "AMANI" (kwa upana wake wote - nataka unielewe kwa maana hiyo).

Wengine tayari wamejiapiza, wapo tayari "kupoteza maisha yao kulinda AMANI". AMANI isiyo ambatana na HAKI!.

Kwa hiyo usifikiri kuna kazi ndogo hapa ya "kumtafuta mbadala".

Watu wanapo amua kuuwa wenzao kwa sababu tu ya mtu mmoja abaki madarakani; usifikiri hapo kuna kazi rahisi.

Naomba usinielewe vibaya. Sisemi kamwe kwamba Kundi "AMANI na HAKI", ndani ya chama hicho ni wepesi wepesi tu. Lakini inatakiwa na wao wajizatiti kikwelikweli kukiokoa chama chao toka kwenye makucha ya hawa watekaji na wauaji wa waTanzania.
 
IMG-20250528-WA0082.jpg
 
Mkutano mkuu wa ccm unaendelea mjini Dodoma yaliko makao makuu ya Taifa la Tanganyika
Ni mkutano wenye agenda nyingi.. Nyingine ni tete na pengine zinaweza kuzimwa ama kujadiliwa kwa tahadhari kubwa sana... Kwasababu huu ni mwaka wa uchaguzi na ccm iko kwenye shaka kubwa kutokana na mambo matatu makubwa

1. Mkakati na kampeni ya CHADEMA kuzuia uchaguzi mkuu kupitia NO REFORMS NO ELECTION
2. Kushinda uchaguzi kama utafanyika kwa uwazi, kwa uhuru na kwa haki
3. Kizungumkuti cha mgombea.. Huyu wa sasa kwa jinsi alivyochafuka ndani na nje ya nchi je atafaa? Au watafute mbadala? Nani?

Katikati ya agenda hizi na mtanziko wa namna ya kwenda nazo.. Siku chache kabisa kabla ya huu mkutano ukatiwa doa kubwa na makemeo ya mmoja wa makada wake kuhusu utekaji nchini na tenguatengua ya wakuu wa vyombo vya ulinzi

Kada huyu maarufu si mwingine bali ni mchungaji Gwajima na mbunge ambaye alipata upinzani mkubwa toka kwa makada wengine wakubwa na wadogo isipokuwa mmoja tuu ambaye aliungana naye.

Aliyeungana naye si mwingine bali ni Luhaga Mpina mbunge pia na aliyewahi kushika nyazifa mbalimbali ndani ya chama na serikalini
Hawa wawili wanachukuliwa kama makada watukutu na wakorofi ndani ya chama wasioogopa kusema chochote kwenye kukosoa utendani ndani ya chama na serikali kwa ujumla

Kolabo yao kwenye hili ni mtanziko mpya ndani ya mkutano mkuu, ambapo sasa inabidi iwepo agenda ya dharura kuwahusu.. Mbaya zaidi wana nguvu kanda yq ziwa na wanahesabiwa kama sehemu ya SKMG
If no reform no economic developments
 
Dua zetu ni kwa kila Mtanzania Mzalendo!!

May almighty protects them
 
Mie naamini usalama wa taifa nako kuna shida. Kama mtu anaweza kupanga mpango na JOHN MREMA NA KIGAILA ambao hata kujieleza hawawezi? Basi kazi ipo
Mazungumzo ya JOHN MREMA na clouds ni aibu kwakweli
Kwani mrema ana uwezo basi mkuu yule alikua anabebwa sana pale ila uwezo wake upo chini niliwahi kumsikia akizungumzia sakata la Dr Slaa tukiwa sehemu nilishangaa kwa kuwa yeye ndio alikua msemaji pale nikawaacha tu ila jamaa hamna kitu kabisaa..
 
Back
Top Bottom