Hii kolablo ya Mpina na Gwajima ni kitisho kwa CCM maslahi

Mbunge wa CCM kupitia jimbo la Kisesa nchini Tanzania, Luhaga Mpina ameonya kwamba taifa hilo halitaweza kuzimaliza changamoto zinazolikabili kwa kuongea kwa lele mama na kutokuambizana ukweli. Amesema hakuna kiongozi mwenye kinga ya kutokukosolewa.

"Hata mahala palipoharibika, mnapongezana. Watu wanatekwa, nyinyi mnapongezana. wananchi wanatekwa.. anatekwa mwananchi wa kwanza, anatekwa wa pili, wa tatu, anatekwa mwananchi wa 80, bado waziri wa mambo ya ndani yuko ofisini!!" alihoji Mpina

Amesema taifa linawezaje kuwa na waziri anayejulikana, halafu anayeleta madhara hajulikani? "Inawezekanaje kuwa na wizara ya mambo ya ndani ambayo kazi yake ni kushughulika na wahalifu, halafu wahalifu hao wakavalishwa jina "wasiojulikana Ni lazima kama taifa tuwe na hasira na mambo yasiyo ya kawaida."

"Waliompiga Fr. Kitima tena kwenye makaazi ya maaskofu hadi leo hawajulikani.. halafu waziri yule bado yupo.. IGP bado yupo, vyombo vya dola vyote vipo na wananchi wengine wanaolia kwa ndugu zao kutekwa na kuumizwa nao wanaendelea kulia. Halafu inafika mahala tunaanza kuzungumza kwa kubembelezana kwa kuhofia watu kupoteza ajira au kutekwa."

Amesema haiwekani kuwa na taifa la namna hiyo na kwamba ni lazima viongozi wanaohusika wajirekebishe au waachie ngazi kama wameshindwa kusimamia mustakabali wa amani ndani ya nchi, huku akionya tabia ya kushabikia mambo mabaya huku lawama zikiwaangukia wanaolaani visa vye utekaji na watekaji wakiendelea kupongezwa.
 
Mimi ni mwana CCM japokuwa si mjumbe wa mkutano unaoendelea ila nachukizwa sana na yanayoendelea na nina imani hata miongoni mwa wajumbe wanaojielewa wanachukia pia. Kumetengenezwa CCM ya ajabu sijawahi kuiona toka izaliwe, isiyosikiliza wananchi, isiyolia na shida za wananchi, isiyojishughulisha na matatizo ya wananchi. CCM ninayoijua inatabia ya kujisafisha hasa nyakati hizi ila hii sioni dalili za kufanya hivyo. Kusemakweli tuna CCM kiziwi kuwahi kutokea, na hiki kiziwi kina sababu yake. Nyakati hizi tutegemee maazimio ya kujisafisha kama kawaida. Binafsi nisipoona mpango madhubuti wa chama kushughulikia utekaji najiondoa rasmi CCM.
 
Sitakujibu wakati huu kwa haraka haraka, kwa sababu mchango wako huu unahitaji kuchangiwa kwa utulivu kabisa. Hili ni swala la nchi yetu, siyo swala la nyinyi wanaCCM peke yenu.
Tutaungana kwa pamoja kama waTanzania kuirekebisha nchi yetu inayo elekea kusiko kuzuri..

Naahidi, nitakusoma tena, na nitachangia zaidi nitakayo kuwa nayo baada ya kutafakari vizuri mchango wako huu muhimu kwetu sote.
 
"Hata mahala palipoharibika, mnapongezana. Watu wanatekwa, nyinyi mnapongezana. wananchi wanatekwa.. anatekwa mwananchi wa kwanza, anatekwa wa pili, wa tatu, anatekwa mwananchi wa 80, bado waziri wa mambo ya ndani yuko ofisini!!" alihoji Mpina
Haya maneno Luhaga Mpina kayaongelea wapi, Bungeni?

Ni wakati wa kuwatambua na kuwaunga mkono hawa wachache wanaojitokeza mbele kuwasemea wengine bila kujali ya huko nyuma walifanya nini.
Hii siyo kazi nyepesi wanayoifanya sasa hivi katika mazingira haya tuliyomo.
 
Mama akamatwe tu na kulazimishwa kuachana na urais maana anajihaibisha mno. Watu wanatekwa na kuuliwa huku yeye akiwa kimya tu kana kwamba anafuiahia. Pia wane na suluhisho la katibi mpya kwani tunataka kuwashikisha adabu marais waliopita pamoja na viongozi wapuuzi walio wezi.
 
"Kizungumkuti cha mgombea.. Huyu wa sasa kwa jinsi alivyochafuka ndani na nje ya nchi je atafaa? Au watafute mbadala"? Nani
Kwa maslahi ya nchi atafutwe mbadala tu
Kwa bahati mbaya sana CCM huwa wanafanya mambo kwa kuangalia zaidi maslahi binafsi na ya chama.

Masuala ya kuangalia maslahi mapana ya taifa waliacha miaka mingi iliyopita.
 
Mie naamini usalama wa taifa nako kuna shida. Kama mtu anaweza kupanga mpango na JOHN MREMA NA KIGAILA ambao hata kujieleza hawawezi? Basi kazi ipo
Mazungumzo ya JOHN MREMA na clouds ni aibu kwakweli
Anajua kujieleza,

Asilojua ni kuongea uongo unaofanana na kweli
 
Mfano ccm wako tayari kumnunua hata boni yai wa chadema na siyo tu kumnunua bali na kumpa nafasi mahali
Je unafikiri watakuwa tayari kumtimua mtu kama mpina ambaye hata akihamia chauma ana uhakika wa kurudi bungeni ? Mtu kama gwajima ukimtimua chama ndiyo umepa kasi sasa umaarufu utaongezeka zaidi ya
Kwa hiyo ccm sidhani kama wana mpango wa kuwaondoa hawa labda kama wana mbinu mbadala
 
https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/share/v/12Krhd5p7fg/?mibextid=D5vuiz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…