Mpira wetu wa Bongo,tukiendeleza Ujinga Ujinga huu watu kuwa ba matokeo nje ya uwanja,Ligi yetu itakuja kukosa Mvuto ....Ukiangalia Rwanda na nchi nyingine za jirani leo tunaona Kenya pia mwamko wa mpira umekuwa mkubwa,huku Kwetu tuache Janja janja,mara Timu moja ina timu zake kwenye Ligi,eti matokeo tayari watu wanaenda kucheza unajua kabisa Yanga anashinda,hili jambo sio la Afya kabisa kwenye mpira.Nadhani Simba na Azam kama vilabu vikubwa ndio vinacheza mpira wa ushindani na matokeo yao ya uwanjani ni Halisi kabisa hayana kipengele.
Ila tuseme ukweli Yanga wanatuharibia ligi ya NBC,mwishoe ligi yetu mvuto utakosekana.Natamani turudi miaka ya nyuma ile kweli kinapigwa unaona Simba inaenda Mbeya haitoki,hapa unasema ligi Kuu kweli...
Kama hivi Tabora vs Yanga unaona kabisa jamaa washafanya mambo nje ya uwanja na kutaka kushinda.Yani vurugu vurugu tu halafu wasimamizi wa Soka wapo Kimya kukemea hili...
Ubora wa Ligi yetu ya NBC unaenda kuisha yasipokemewa haya.
Sitaki kusema mengi...
Ila mmemsikia Mhe.RC wa Tabora,ya kuwa wachezaji wanatumiwa jumbe na miamala kuahidiwa ili wacheze chini ya kiwango na kuwaachia Yanga...
Soka la kivyetu vyetu,pale mpira badala ya kugeuka kuwa mchezo wa Ushindani unageuka kuwa mchezo wa Rushwa...Huu ni upumbavu halafu na sisi mashabiki wa Soka badala ya kupiga kelele kukemea haya tunakaa kushadadia ujinga na upuuzi huu.Tunaua soka letu kila siku.
GENTAMYCINE
@