Hii 'Mashemeji derby' inaenda kufuta ule upuuzi wa Kariakoo

Kumbe ndo mvivu wa kufuatilia hiv? Ndo maana unaandika nyuzi kama hiz za kujidharau

Derby yao imeahirishwa mara mbili kwa ukosefu wa uwanja.
Uwanja kuwa kwenye matengenezo na sio kususia .mechi kwa kukosa mazoezi ya uongo na kweli sababu Yao ilikuwa genuine na ilijulikana mapema sio ya kariakoo ambayo watu waliingia hasara za Kila aina
 
Kamwe hiyo Derby ya wajaluo na wakikuyu haitaizidi Kkoo derby. Acheni masikhara aisee. Wapinzani wa Derby ya Simba na Yanga wako South Afrika tu kwa ukanda wa SADC na EAC.
Uwanja umeongea Leo ni suala la mda wakianza kusajili ma pro tayari wataanza kutoa changamoto kwa Simba na Yanga
 
Watanganyika wanasifia kila kitu cha Kenya na Rwanda hata kama cha hovyo. Inferiority complex.
Hii nchi tatizo ina raia wa hizo nchi na wamepewa uhuru wa raia wa kawaida.
Sasa unaposema inferiority complex kwa sababu unatoa maoni ya hisia tu hayana ukweli.
Hii ni tabia ya watu wasio na elimu
 
Uwanja kuwa kwenye matengenezo na sio kususia .mechi kwa kukosa mazoezi ya uongo na kweli sababu Yao ilikuwa genuine na ilijulikana mapema sio ya kariakoo ambayo watu waliingia hasara za Kila aina
Nakushauri utafute habari. Acha kukoment mihemuko.
Juzi kati hapa. Wamehairisha mechi siku moja kabla eti kisa AFC leopard hana uwanja
 
Acha tff waendelee kulala usingizi na kujidanganya ila fkf inarejea kwa Kasi sana
Tena Kasi ya kimbunga Katrina, Kwanza Kenya Wana makampuni makubwa, wanajua kujitangaza, wanajua ushindani, hii ligi yenu ya kutumia kanuni ya Busara itabaki historia
 
Matokeo ya ubaya wote ufanyikao sirini matokeo yake huonekana hadharani,angalia mwaka huu timu ya Yanga imeishia Makundi,mwenzao yupo kimataifa,Yanga hana ushindani wa Uwanjani kuanzia ndani ndio maana hata kocha wao aliyetimkia Algeria aliyaona haya akawakimbia.

Na kuna uwezekano hata mwakani Yanga wasifanye vyema kimataifa,waache ujinga wa kuzicheza mechi nje ya Uwanja.Mpira wetu utazidi kukosa Radha kwa upuuzi huu.
Mimi binafsi nishaacha kuangalia mechi zao, naangalia mechi za Azam na Simba tu.Kuona watu wanavyopambana kweli kutafuta matokeo uwanjani.
 
Punguza chuki na ushabiki, naona mahaba yamekuzidi mpaka hujui nini ulichoandika, mwisho wa siku ndo mnakuwa wa chawi kwa ajili ya chuki
 
🚮
 
Kujikubali kwa lipi!?
Mpira mechi inaihirishwa sababu ya birthday mechi inaihirishwa sababu ya mabaunsa viwanjani maamuzi yana dosari za kutosha useme tujikubali kivipi!?
Yes kwa Sasa tuko mbele Yao ila hatua wanayopiga inatishia usalama wa huo utawa
Kutamba kwa kununua Mechi???
Una risiti ya mauzo hata ya mechi Moja!?
Unajua misimu minne ya Simba kuchukua ubingwa alikuwa analalamikiwa hivyo hivyo kwa coastal,namungo,n.k!?
 
Uliangalia mechi ya Azam na pamba!?je Simba na JKt au Simba na fountain gate!?unazungumziaje mechi na tabora
Ukitaka kurekebisha angalia pote ukiangalia upande mmoja hakuna kitu utasaidia utakuwa sawa na bodi ya ligi
 
Derby ya kikabila.
Gor(luo) Vs AFC(luhya) makabila ya ukanda mmoja Nyanza na western na Wana mwigiliano wa kuoana. Maana halisi ya neno shemeji.
Safi sana umefafanua kirahisi zaidi na ndio maana Leo ilikuwa na mvuto mkubwa sana
 
Tena Kasi ya kimbunga Katrina, Kwanza Kenya Wana makampuni makubwa, wanajua kujitangaza, wanajua ushindani, hii ligi yenu ya kutumia kanuni ya Busara itabaki historia
Tukisema haya tunaambiwa ni inferiority complex ila Kenya hata mechi ya Shabana na police unaliona joto kweli sisi joto litakuja baadae kwa team kugombea zisishuke daraja
Narudia tena "tusipokuwa makini tutapoteza bidhaa muhimu ya kimichezo"
 
Azam akiwekeza kama alivyofanya hapa bongolala ligi ya Kenya itatupita in 10yrs time.
Kenyans are monsters when it comes to opportunity.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…