Suala la kuwa ni serekali ya majizi ya kura, wala sihitaji ww udhibitishe hilo, maana hivyo ndivyo ilivyo regdless unakubali hukubali.
Tuje kwenye hayo maelezo yako ya kutaka kusifia mtu na sio mifumo. Tuanze na reli ya SGR, hiyo reli kipande cha Dar-Moro alisema itakamilika Nov 2019, je mpaka anafariki hicho kipande kilikuwa kimekamilika ambapo ni ni mwaka na zaidi? Unatarajia muujiza gani kwa wale ambao walikuwa sio sehemu ya maamuzi yake. Mgao wa maji, yeye angekuwepo angefanyaje iwapo hakuna mvua, na hakuna water reserve yoyote kukabiliana na hali hii? Alipoingia madarakani 2016 kulikuwa na ukame mkali na mgao wa maji ulikuwepo pia, yeye alifanya miujiza gani?
Unapotosha kuwa malori yalikuwa yamefichwa sasa yamerejea kwa kasi, ni kwamba hiyo SGR ilikuwa inafanya kazi hayo malori yakaaondoka, na sasa hayupo treni imesimama ndio malori yamerudi ama? Unasema hujui kama SGR itaisha, yeye alikopa zaidi ya 15y+, mbona hakumaliza hiyo SGR & SG respectively?
Unasema Tony Blair alikuja hapa nchini kutushauri, kwahiyo alikuja kutushauri tuwe na mgao wa maji na umeme!? Toka lini ushauri ukawa shuruti kwa viongozi wetu? Au unadhani wote ni hamnazo kwa kuchomekea sababu zisizo na kichwa wala miguu?
Arrogance kwenye taasisi za serikali imerudi tena, kwani iliwahi kuondoka au uhuru wa vyombo vya habari tu uliminywa kuripoti habari hizo negative? Kama kuna tofauti, basi ni ndogo sana kwa yeye kutokuwepo. Kwani hatukuona watu wakitekwa na kuuwawa, bila kupata majibu ya mambo hayo? Tulishuhudia chaguzi za kishenzi na kihayawani chini ya tume ya uchaguzi, au hiyo tume ya uchaguzi sio taasisi ya umma? Huenda unachanganya ufanisi na hofu+ maigizo. Bei ya mafuta ya kula na petroli yalipanda maradufu wakati wake, ajira kulikuwa hakuna nk. Au ni ubora gani unaongelea?
Gazeti la financial times limeanza kutusifu tena, kwani likitusifu sasa kuna ubaya gani kama wanaona utawala wa kishenzi umeondoka? Isitoshe gazeti la Financial Times lina madhara gani hapa nchini wakati halina hata wasomaji? Mbona magazeti ya uhuru, habari leo nk yanayochwapwa hapa nchini na kusomwa hadi sasa, yanasifia kwamba mambo ni mazuri toka utawala huu uingie? Je tukuamini ww na sio hayo magazeti ya serikali yanayosema mambo ni mazuri? Kama kweli unasema mambo ni mabaya hadi unashangaa financial times kuisifia nchi yetu, mbona kinachoandikwa na magazeti ya ccm na serikali kusifia hali ni nzuri hakikushangazi?
Wakati anapora na kunajisi chaguzi, huku akiharibu mifumo ya kuhoji mliona anafanya kitu cha maana. Hatimaye amefariki akiwa ameua mifumo ya kuhoji,mambo yanazidi kuharibika kwa kasi na hakuna mwenye uwezo tena wa kuhoji, badala ya kujiuliza tumefikaje hapa, mnaanza kuchomekea sababu za uongo ili kumsafisha mtu muovu! Unashangaa rais muovu kusemwa, kwani alikuwa mtu muadilifu, Nape si alitolewa bastola hadharani akiwa waziri, alichukua hatua gani kama alikuwa kiongozi mzuri? Je ni kiongozi au binadamu gani asiyesemwa? Au kwako yeye alikuwa Mungu? Kama alikuwa hataki kuambiwa ukweli, ulitegemea watu wasimsungumze huko pembeni? Huu ujinga wa kutotaja kuambiwa ukweli naona kauacha kwa wengine, Ndugai naye kaambiwa ukweli anaanza vitisho vya ulevi wa madaraka.
Tunaposema tunataka katiba mpya tunamaanisha, bila kuwa na mifumo bora. Kama kungekuwa na katiba bora yale mazuri yake yangebaki, na uchafu wake asingepata nafasi ya kuufanya. Lakini badala yake, mazuri yake yametoweka, na uchafu aliopandikiza ndio umechukua nafasi. Amka dai katiba mpya itakayolinda mifumo, na sio kuamini mtu anayeweza kufanya mazuri machache na maovu mengi.