Hii nchi haina usawa: Mbunge miaka mitano, mafao zaidi ya Tshs. 200M, mwalimu miaka 32 kazini, mafao Tshs. 70M, miezi sita hajalipwa

Dhana ya "Rais wa wanyonge" ina maana nyingi. Kwa namna wanavyolitumia hawa wenzetu inaonekana wanamaanisha Rais anayetengeneza taifa la watu wanyonge ili awatawale wakiwa katika hali hiyo ya unyonge.
 
Maneno ya Ndugai alipopokea mic kutoka kwa Rais mliyasikia? Akaanza kusema "nimetumwa na wabunge kukwambia Mhe. Rais kuhusu utaratibu...kuhusu utaratibu" huku anacheka cheka... Wabunge nao wanashangilia... halafu akasema "nimeambiwa imeshapita..."

That was beyond reprehensible.

The last thing out of your mouth mbele ya Watanzania milioni 60 wasio na viinua mgongo, pensheni, ajira, savings account, bima, mitaji, nothing, kwenye kufunga bunge ni kuongelea maslahi yenu binafsi, kupigia chapuo mabilioni yenu? Ubinadamu gani huo?

Tena unajifanya kama bado hazijatoka au zinaweza kukwama vile, ili ujipigie kampeni ya kurudi kwenye U-Spika kwamba we ndo ulizipigania wakati unajua zimeshalipwa kwenye benki zenu!

Bado hatuna watu wanaojua ku balance maslahi yao na ya Umma.
 
Ndg yangu mtoa post! Nimeisoma post yako kidogo tu nikajua unakoelekea! Jibu la hoja yako ni dogo tu " Acha kazi hizo unazofanya zenye ujira mdogo" sheria yetu ipo wazi inaruhusu tu na wewe kuzamia humo mjengoni! Vinginevyo utaendelea kushangaa na kulalamika!
 
Sheria ungekuwa unatunga wewe ?
vilaz.a wale watatunga sheria gani ya maana, si bora hizo sheria kukawa na kakikundi kadoogo ka watanzania WATAALAM wakatusaidi kuzitunga hizo sheria.
Bunge la tz uwepo wake hauna tija yoyote...ni bahati mbaya wananchi wa kawaida hatuna namna yoyote ya kupinga hali hiyo...labda kizazi kijacho kitapata "namna" ya kuukataa ujinga huu!!!.
 
Kwahio akizamia mjengoni yeye matatizo ya mafao kwa walimu wote nchini yataisha?
 
Wengine mafao yetu hayazidi laki Saba lakini mpaka leo hatujapata tunazidi kufuatilia tu .
 
Inahuzunisha sana Tanzania siasa imesha kuwa the big business, tuombe Mungu huko mbele abadili kila kitu siasa iwe ni kazi ya kujitolea ili kuwasaidia wananchi,. Ni Nyerere peke yake ndio alikuwa mwanasiasa mzalendo Tanzania. Wabunge walikuwa wanasafiri kwa mabasi kwenda bungeni.
 
Hakuna mwanasiasa anayeweza kuleta usawa wa kipato,ni porojo tu.
 

Vipi kuhusu madiwani wanapata mafao kiasi gani?
Aisee watu wanauana kwenye nafasi za kisiasa
 
Na mfano hai aliekuwa mbunge wa Kilombero kabla ya huyu alieomba kaz ya kupiga deki na kufagia Lumumba, mpk sasa ni marehemu.
uko sahihi kabisa, zile pesa ni DHULUMA hauwezi kufanikiwa maishani.
Wengi wao wakitoswa ubunge hufa masikini!!.
Ogopa sana kudhulumu masikini.
cc Job Ndugai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…