Hii nchi haina usawa: Mbunge miaka mitano, mafao zaidi ya Tshs. 200M, mwalimu miaka 32 kazini, mafao Tshs. 70M, miezi sita hajalipwa

Siku tukilinganisha mambo mengine na nchi zingine usikimbie


Kwa nini nikimbie? Kwa hiyo ulitaka Mwalimu na Mbunge wawe na kipato sawa? Ni wapi hilo linafanyika labda?
 
Kwahiyo bila bunge kwahiyo bunge likifutwa zitakuwa zinapitishwa na nani ?
Mkuu.

Bunge likifutwa hapo inamaanisha aliyelifuta ndiye anakua inchaji. Kwa nchi yetu Rais ana uwezo huo.

So yeye ndiye atapitisha.
 
Mkuu Mimi huwa mnanikosea hapo tu ukiachana na CCM tatizo siyo chama sisi ndo tupo hivyo kama waafrika mi nipo tayari kuona kiongozi yoyote akae madarakani najua ni yale yale yataendelea. Swala kuu ni kutengeneza FIKRA ya huyu mwafrika achana kabisa na mambo za CCM CDM futa.
 
Hilo GENGE LA WAHUNI hata siku moja haliwezi kuona tofauti hii kubwa sana kati ya mapato ya Wabunge wa Bunge FAKE na madaktari, walimu, manesi n.k. Hakuna haki hata chembe.


 
NDIOMAANA SIPOTEZI MUDA KUWAPIGIA KURA CCM
 
Kwa taarifa yenu zile hela anazogawa barabarani na kwenye makanisa ya katoliki ni michango ya wastaafu kutoka psssf. Mfuko upo hoi.

Mlivyo wanafiki, wazushi na wachonganishi, eti: "Magufuli uchangia makanisa ya Kikatoliki!!" Mara ngapi tumeshuhudia akichangia ujenzi wa Misikiti Nchini, juzi hapa kachangia ujenzi wa Msikiti pale Chato - wakati mwingine mjifunze kubakiza akiba ya maneno.

Nisieleweke vibaya, hata mini uaikitishwa sana nionapo wastaafu wakipigwa danadana, kucheleweshwa mafao yao, wengine kutolipwa kabisa kutokana na visingizio vya kutunga tu na dhuluma za mwajili bahati mbaya Serikali hii hii ambayo tunaiita ni mtetezi mkubwa wa wanyonge inakuwa na kigugumizi cha kuwachukulia hatua kali/wajibisha waajili wakorofi ,wadhulumaji na mafisadi wanao endedha mashirika ya UMMA kama mali ya UKOO!! Mfano ahi TAZARA, wastaafu wameangahikia kiinua mgongo chao miaka nenda rudi bila mafanikio, Wizara ikufikia hatua ya kuwambia wastaafu jqamba hawastahili kulipwa kiinua mgongo, hivi kuna sheria gani hapa kwetu Tanzania ambayo inasema baadhi ya mashirika ya UMMA haya wajibiki kulipa wastaafu kiinua mgongo, inakuwaje Serikali ya Zambia imewajibika kuwalipa wastaafu wa TAZARA upande wa ZAMBIA lakini Serikali yetu tunayo fikiri ni mtetezi mkubwa wa wanyonge haioni umuhimu wa kuiga mfano mzuri wa Zambia wa kuwalipa kiinua mgongo wastaafu wa TAZARA upande wa Tanzania ambao wengi wao walihusika katika ujenzi wa reli, robo ya wastaafu wamekwisha fariki Dunia, inaelekea tatizo la wastaafu wa East Africa Community linataka kujirudia TAZARA.

Kinacho shangaza zaidi katika suala zima la wastaafu wa TAZARA, atakuta wanao fikisha suala hili mahakamani kwa kutumia mawakili, Serikali inakubali kuwalipa kiinua mgongo chao! Hii inamaanisha wale wasio kuwa na uwezo wa kuwalipa mawakili watakosa haki zao, now a million dollar question is: kwa nini Serikali moja inakuwa na double standard linapo kuja suala la kuwalipa wastaafu wa TAZARA mafao yao.
 
Badala ya kutumia pesa nyingi hivyo kuwalipa wagonga meza, ni bora kuwapa wataalamu angalau wafanye tafiti mbali mbali ikiwemo kutafuta chanjo na dawa za magonjwa kama korona...
 
Nitajie nchi iliyo na usawa kati ya Wanasiasa na watu wa kawaida, ...

Usiniulize swali badala yake lieleze jukwaa kwanini unadhani kusiwe na usawa kati yao?

Sera na ilani ya CCM toka mwaka 1961 mpaka 2020 inasemaje kuhusu hili...?
 

Aisee, It's very sad....

Inaumiza sana ndugu yangu. Mungu amsaidie huyo mama kwanza apate afya na alipwe mafao yake haraka...

Na sisi wengine tusichoke kupiga kelele....

Lazima kila tupatapo nafasi tu - shout against this injustice....

Kelele zetu hizi za msaada zinamfikia Mungu na anasikia...

Ukombozi wetu u karibu, msikate tamaa
 
Usiniulize swali badala yake lieleze jukwaa kwanini unadhani kusiwe na usawa kati yao?

Sera na ilani ya CCM toka mwaka 1961 mpaka 2020 inasemaje kuhusu hili...?


Kwani nimekulazimisha kunijibu? Ondoa jazba kama mtoto, ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…