Hii nchi haina usawa: Mbunge miaka mitano, mafao zaidi ya Tshs. 200M, mwalimu miaka 32 kazini, mafao Tshs. 70M, miezi sita hajalipwa

Mleta mada yeye kaona katika hili wa kulaumiwa ni Magufuli na ccm tu,ila mie naona hawa wanasiasa wa upinzani ndio wanatakiwa kulaumiwa kwa unafki wa kutopigia kelele masuala yenye kugusa masilahi yao.
 
Kuna matatizo mengi kama na yapo kwa muda mrefu tu ili sasa muda wote tunajadili udikteta wa Magufuli na utawala wake kana kwamba kabla yake mambo yalikuwa shwari.
 
Unaongea sababu si mnufaika
Mtu yupo bungeni vipindi 4-6 na kila kipindi analipwa pension, hii haki kweli? Ndiyo maana wataalamu wanaacha kazi zao wanaenda kupasha mikono na kusinzia hovyo hovyo
 
hata wabunge wetu wameshindwa kabisa kuwa watetezi wa wapiga kura wao! ni vyema wafanyakazi wote wakaungana na kutowapa ubunge wanaogombea kwa awamu ingine. tuwape wapya na tuwape jukumu la kwenda kupigania haki za wafanyakazi wanaoteseka.
Wewe si muamuzi wa nani awe mbunge na nani asiwe
 
Ndo maana ya madaraja. Wale ndio maana ya serikali. Bila Serikali ni mjumuishi wa hayo
 
Mambo Kama haya ndo uwafanya wataalamu wetu kutafuta ajira nje ya afrika,then wanasiasa uwatumia kina Walter Rodney kuandika chuki za how Europe underdevelope afrika.Hali sisi wenyewe ndo atuwathamini wasomi.Leo cv ni uwezo wako binafsi wa kuimba kwaya,kuwatukana wapinzani,kuwadhalilisha na sio ya utaalaamu au usomi wako.
 
Pole nyingi kwa wale wenye pesa za kuchezea kuchangia hao mabwanyenye.
 
Inasikitisha sana.siyo tuu hata mafao.watumishi wengi wa uma wana madai halali mengi sana lakini hawalipwi hata kudai wanaogo eti watatumbuliwa wanaonekana siyo wazalendo kuidai dai serikali.wanatumwa na mabeberu
 
yupo mwalimu aliyefanya kazi miaka 32 (1988 - 2020) kwa taabu na shida nyingi. Amestaafu tangu mwezi Januari, 2020. Baada ya kukokotolewa kwa mafao yake ya mkupuo atapata kama Tshs. 75,000,0000 hivi.

Tena hiyo milioni 75 ya mwalimu kwa mahesabu yangu mimi wala haifiki !

Kwa mujimu wa takwimu za utafiti wa shirika la TWAWEZA wastani wa mshahara wa Mwalimu ni 637,790/=

Kwa sheria ya PSSSF ya kanuni na vikokotoo vya mafao ya pensheni ya mkupuo, hela hiyo haikaribii hata robo ya milioni 75.

APE = Shilingi 637,790 kwa mwezi mara miezi 12 = Shilingi 7,653,480 kwa mwaka
PS = miaka 32 mara miezi 12 kwa mwaka = miezi 384
CF = 12.5
PF = 1/580
CR = 1/4

Hizo namba tano (APE, PS, CF, PF, CR) ukizizidisha unapata milioni 16 tu!

Haya, basi tuseme ni Mwalimu Mkuu labda anapata milioni 1 kwa mwezi, which is a pipe dream estimate, bado mkupuo wake ni 24.8 milion

Sasa hiyo milioni 75 ya mwalimu mnaipata wapi ????
 
Inasikitisha sana, yeye mwenyewe MTUKUFU MFALME anajilipa 1.2 Bilioni kila mwezi (NJE YA MSHAHARA NA MARUPURUPU YAKE), kwaajili ya kufanyia STAREHE NA ANASA TU.
Nchi hii inaliwa na wenye meno, wajinga ndio waliwao. Ndio sababu haya ma CCM yapo tayari KUCHAPA RISASI MPINZANI YEYOTE MCHANA KWEUPE..
 
Daa, ukweli mchungu sana
 
Hii ilipaswa iwe SAUTI KUU YA WATANZANIA
Wabunge wanafaidi wao wakirudi majimboni story nyingiiiii hawana lolote

WABUNGE KWA NINI MAISHA YENU YAWE YA UHAKIKA ZAIDI KULIKO MTANZANIA
BUNGENI HUWA HAMUONGELEI POSHO MISHAHARA MIKOPO YENU??!
TUANZIE HAPA
HAMSTAHILI MEMA YA NCHI KULIKO MTANZANIA WA KAWAIDA
KWENYE MIKUTANO YENU TUNAOMBA MTUJIBU HILI
WABUNGE WA KUTEULIWA NI KICHAKA CHA UHUNI HAWANA WANALOFANYA BUNGENI

ALL THIS CRAP HAS TO STOP !
 

Exactly, tukianzisha movement ya namna hii kwa umoja wetu, tunaweza KUBADILI MAMBO....
 

Kwa mujibu wa Salary Scheme ya kada ya ualimu "TANZANIA GOVERNMENT TEACHERS SALARY SCALES (TGTS)", wengine hufikisha kiwango hicho especially kama kiwango cha elimu cha mwalimu huyo ni ingalau stashahada ama shahada....

Ukianza kazi kama mwalimu mwennye shahada (university degree), utaanza na Salary Scale ya TGTS. D1 ambayo mshahara kwa sasa ni Tshs. 730,000 (kama sijakosea kidogo)...

Mwalimu mwenye Stashahada (Diploma in Education) akianza kazi leo, ataanza na Salary Scale TGTS. C1 ambayo nadhani kwa sasa ni kama Tshs. 575,000 hivi (kama sijakosea kidogo)....

Hawa wote wakipata neema ya Mungu kwa sababu mtu kuwa kwenye utumishi wa umma nyakati hizi kwa miaka 32 ama zaidi siyo mchezo, ni neema ya Mungu pekee itakufikisha hapo, basi uwezekano wa kufikia Salary Scale ya TGTS H (Tshs. 2,300,000) ama TGTS. I (Tshs. zaidi ya 2,800,000) ni Mkubwa....

Hawa wakifika hapo uwezekano wa kupata mafao ya kiinua mgongo kizuri ni Mkubwa....

Huyu wa Sengerema - Mwanza niliyemtolea reference hapa, ni halisi na ni ndugu yangu, mwalimu wa shule ya msingi. Kastaafu akiwa ngazi ya mshahara wa TGTS. G ambao kwa sasa ni kama Tshs. 1,600,000+ hivi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…