Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye maslahi yao huwa wanaungana , pesa kitu kingineMleta mada yeye kaona katika hili wa kulaumiwa ni Magufuli na ccm tu,ila mie naona hawa wanasiasa wa upinzani ndio wanatakiwa kulaumiwa kwa unafki wa kutopigia kelele masuala yenye kugusa masilahi yao.
Ni wakati sasa na sisi kuungana na sio kukubali kutenganishwa na hawa wanasiasa hali ya kuwa wao huungana kwenye masilahi yao.Kwenye maslahi yao huwa wanaungana , pesa kitu kingine
Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
Kipindi hiki wanajishusha kama si wao, na tatizo mtu akipewa kitu kidogo anasahau shida zote, hajiulizi kesho itakuwajeNi wakati sasa na sisi kuungana na sio kukubali kutenganishwa na hawa wanasiasa hali ya kuwa wao huungana kwenye masilahi yao.
Mtu yupo bungeni vipindi 4-6 na kila kipindi analipwa pension, hii haki kweli? Ndiyo maana wataalamu wanaacha kazi zao wanaenda kupasha mikono na kusinzia hovyo hovyo
Wewe si muamuzi wa nani awe mbunge na nani asiwehata wabunge wetu wameshindwa kabisa kuwa watetezi wa wapiga kura wao! ni vyema wafanyakazi wote wakaungana na kutowapa ubunge wanaogombea kwa awamu ingine. tuwape wapya na tuwape jukumu la kwenda kupigania haki za wafanyakazi wanaoteseka.
Ni kweli, hilo haliepukiki....But not to this extent....
Hutuongelei usawa wa wote tuwe wabunge au mawaziri ama Marais kwa wakati mmoja. HAPANA...!!
Sawa wewe mbunge FIRST CLASS au DARAJA "A", kwa miaka mi5 tu ya utumishi una mafao ya Tshs. 230,000,000
Mwalimu ama nesi ama Daktari " THIRD CLASS" ama "DARAJA " C", miaka 32 ya Utumishi wa umma huohuo, mafao yake Tshs. 75,000,000...
å Kwanini hawa RAIA DARAJA LA KWANZA (wabunge, mawaziri, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi, RCs, DCs nk) mafao makubwa milioni 1000, 900, 500, 230 na wanajilipa haraka haraka kabla hata kustaafu rasmi??
å Kwanini sisi RAIA DARAJA LA TATU (walimu, manesi, polisi, madaktari, nk nk) miaka 38, 35,32, ama 25 ya utumishi, mafao milioni 80, 70, 50, 15, 10 na hata 5 lakini inachukua miaka, miezi kadhaa kulipwa? Why? Why?
Usawa tunaoutaka kwa steji hii ni kila mtu kwa kiwango chake kikubwa au kidogo akipate kwa wakati huo huo unaotakiwa...!!
Wewe endelea na kampeni zako za ubunge, wengine unafiki kwetu umepita pembeni,Unaongea sababu si mnufaika
Wewe endelea na kampeni zako za ubunge, wengine unafiki kwetu umepita pembeni,
hakuna anayeona wivu bali watu wanataka usawa
Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
Basi tulia endelea kula bataUsawa hautakuwepo kamwe
yupo mwalimu aliyefanya kazi miaka 32 (1988 - 2020) kwa taabu na shida nyingi. Amestaafu tangu mwezi Januari, 2020. Baada ya kukokotolewa kwa mafao yake ya mkupuo atapata kama Tshs. 75,000,0000 hivi.
Daa, ukweli mchungu sanaHii nchi haina usawa. Hii nchi haijapata kiongozi wa kuleta usawa ingalau kwa nusu tu miongoni mwa wananchi.
Tumesikia wimbo huu wa kinafiki kuwa, Rais John Pombe Magufuli ni Rais na kiongozi wa wanyonge, wananchi wa hali ya chini.
Si kweli, ni uongo mtupu na ni propaganda za kisiasa tu kwa ajili ya wapambe na wanafiki wachache wanaomzunguka huku uhalisia wa mambo ukiwa tofauti.
## Mfano wa kuthibitisha hili ni huu;
Bunge limevunjwa juzi tarehe 16/6/2020. Hawa wabunge lililovunjwa juzi wameingia kazini mwaka 2015. Wamefanya kazi yao miaka mitano (5) tu toka mwaka 2015 hadi mwaka huu 2020.
Inasemekana mafao ya kiinua mgongo kwa miaka mitano tu kila mmoja ni zaidi ya Tshs. 250,000,000.
Na inasemekana wakati Rais Magufuli (eti Rais wa wanyonge) anahutubia ndani hiyo juzi kulivunja bunge hilo, tayari mzigo wa fedha wa kila mbunge ulishaingia kwenye Bank Account yake.
## Hebu tazama upande wa pili wa wanyonge halisi kinachotokea.
Huko Sengerema (na naamini kwingine kote Tanzania nzima), yupo mwalimu aliyefanya kazi miaka 32 (1988 - 2020) kwa taabu na shida nyingi. Amestaafu tangu mwezi Januari, 2020. Baada ya kukokotolewa kwa mafao yake ya mkupuo atapata kama Tshs. 75,000,0000 hivi.
Kinacholeta shida ni kuwa, tangu huyu mwalimu masikini astaafu kwa mujibu wa sheria mwezi january hadi Juni hii mwaka huu, 2020 (miezi 6 sasa) bado anasotea mafao yake haya kidogo, hajalipwa.
## Sasa swali la kujiuliza ni hili;
Kati ya wabunge hawa ambao bunge linavunjwa leo huku mafao yao yakiwa yameshalipwa jana yake ama siku kadhaa hata kabla ya ku - sign off lakini huyu mwalimu ambaye ndiye mnyonge halisi kastaafu miezi sita (6) iliyopita na bado hajalipwa vijisenti vyake vya mafao, ni nani hasa mnyonge? Nini mantiki (logic) ya unyonge kwa mujibu wa CCM na viongozi wao?...
Na huu usawa katika nchi hii uko wapi? Iweje mbunge aliyefanya kazi miaka mitano tu alipwe mafao ya kiinua mgongo makubwa kiasi hicho karibu mara tano ya mtumishi was kawaida kama mwalimu ama nesi ama daktari aliyefanya kazi kwa miaka 35?
Huyu mtetezi wa wanyonge (Bwana Magufuli) anatetea wanyonge na unyonge upi hasa?
Mimi nasema Tanzania haina kiongozi Rais mtetezi wa wanyonge.....!!
Haijapata na hakuna kizuri wala kiongozi mzuri atakayetokana na CCM ili kubadilisha hali hii na kuleta TOFAUTI, HAKI na USAWA....
Tupaze sauti zetu kwa njia mbalimbali na zozote halali juu ya jambo hili. Haiwezekani wengine tufanyishwe kazi usiku na mchana kama watumwa, jasho letu likaliwe na RAIA wachache wanaojiita "FIRST CLASS CITIZENS"....
Sasa wakati ni huu kuamua kuwa, kazi za kisiasa kama ubunge, uwaziri, Urais nk ziwe kazi za WITO na siyo za UJIRA na MAFAO makubwa. Kwa njia tutapata viongozi halisi walio tayari kutumika kwa ajili ya wengine....
Hii ilipaswa iwe SAUTI KUU YA WATANZANIAHii nchi haina usawa. Hii nchi haijapata kiongozi wa kuleta usawa ingalau kwa nusu tu miongoni mwa wananchi.

Hii ilipaswa iwe SAUTI KUU YA WATANZANIA
Wabunge wanafaidi wao wakirudi majimboni story nyingiiiii hawana lolote
WABUNGE KWA NINI MAISHA YENU YAWE YA UHAKIKA ZAIDI KULIKO MTANZANIA
BUNGENI HUWA HAMUONGELEI POSHO MISHAHARA MIKOPO YENU??!
TUANZIE HAPA
HAMSTAHILI MEMA YA NCHI KULIKO MTANZANIA WA KAWAIDA
KWENYE MIKUTANO YENU TUNAOMBA MTUJIBU HILI
WABUNGE WA KUTEULIWA NI KICHAKA CHA UHUNI HAWANA WANALOFANYA BUNGENI
ALL THIS CRAP HAS TO STOP !
Tena hiyo milioni 75 ya mwalimu kwa mahesabu yangu mimi wala haifiki !
Kwa mujimu wa takwimu za utafiti wa shirika la TWAWEZA wastani wa mshahara wa Mwalimu ni 637,790/=
Kwa sheria ya PSSSF ya kanuni na vikokotoo vya mafao ya pensheni ya mkupuo, hela hiyo haikaribii hata robo ya milioni 75.
APE = Shilingi 637,790 kwa mwezi mara miezi 12 = Shilingi 7,653,480 kwa mwaka
PS = miaka 32 mara miezi 12 kwa mwaka = miezi 384
CF = 12.5
PF = 1/580
CR = 1/4
Hizo namba tano (APE, PS, CF, PF, CR) ukizizidisha unapata milioni 16 tu!
Haya, basi tuseme ni Mwalimu Mkuu labda anapata milioni 1 kwa mwezi, which is a pipe dream estimate, bado mkupuo wake ni 24.8 milion
Sasa hiyo milioni 75 ya mwalimu mnaipata wapi ????