Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,118
- 4,238
Mtandao na internet
Kuna maeneo Bado watu wanajitega kwa ajili ya kupiga simu na kuingia internet
Tigo na kujimwambafai kote Kuna maeneo Bado ni bilabila
Barabara na uchukuzi
Kuna maeneo Tanzania hii hii kipindi cha mvua wanakata muingiliano/mawasiliano ya kutoka na kuingia mpaka mvua zipungue au msimu wa mvua uishe kabisa
Maji
Kuna maeneo vijijini gharama za maji zipo juu kuliko jijini Dar es salaam. Maji ni taabu mkombozi mvua tu. Wabunge bungeni unawaangaliaa kisha unawaangalia tena halafu mwisho unabaki kuwa angalia na hupati Cha kuwaterm.
Huduma nyingine za kijamii
Kuna maeneo Bado shule watoto ni changamoto kutokana na umbali, huduma za afya na huduma muhimu nyinginezo za siku kwa siku watu hawapati au wanapata kwa usumbufu na/au gharama mkubwa
Pendekezo
Serikali ijitahidi kuboresha hususani kwenye huduma muhimu mfano Mkoa wa Lindi watani zangu Wasukuma wameuvamia kwa wingi sana unakuta eneo lina watu (Wasukuma) wa kutosha wameweka makazi lakini watu hao hawana shule, hawana zahanati, wala hawajui jambo lolote kuhusu serikali ya Kijiji
Wadau wengine wanaohusika nao waongeze nguvu katika maeneo hayo. Mfano ishu ya mtandao kwa uwingi wa Wasukuma maporini ulikuwa ni muda mwafaka wa mtandao ya simu kupigana bao katika kujizolea wateja. Yaani halotel na ttcl kweli za kukosekana maporini!?