Hii nchi ngumu kweli, eti mtu kashaliwa kichwa

Hii nchi ngumu kweli, eti mtu kashaliwa kichwa

Clark boots

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
6,770
Reaction score
6,202
Hii nchi ni ngumu sana wadau, eti hapo mtu kashaliwa kichwa Hali ya kuwa alishawahi kuitwa Interview 2 na akafanya.

Alafu hawataki hata kupitia tena majina maana wengine walipeleka kwa Hakimu Ila bado wameandikiwa vivyohivyo.

Hii nchi ngumu sana inafikia kipindi mtu unawaza Why umezaliwa nchi yenye watu wabaya namna hii kama hawa wasio na huruma, vyeti unavyo na hata ukifika Interview unakaguliwa Ila bado Unaonekana we ni mlaghai, Sasa hivi kupata kazi ni ngumu na hata kuitwa Usaili ni ngumu pia?

Nipo Frustrated sana wadau sijui kwanini wamenifanyia unyama namna hii, Just imagine wangeniita usahili hapa wangepungukiwa nini?

Nauli ya kwenda ni ya kwangu, kula na kalala ni juu yangu, nikateseke na maswali juu yangu Shida kwao Iko wapi sasa..!!
INASIKITISHA SANA

Screenshot_20220321-223030_1.jpg
 
Mkuu ndio maisha...nilishaapa katu sitakaa niombe ajira za utumishi miaka sasa
Duuh mkuu sio poa, hapa sijui wangeniita wao wangepungukiwa nini,, Nauli ya kwenda ni yangu, kula na kulala juu yangu KAMA SIO ROHO ZA NYOKA hizi kiwe nini mkuu. Hii nchi inawatu wabaya sana dadeq
 
Wanasema Bila connection ni kama kuandika moja kwenye maji.
Sasa connection mkuu ndo hata usahili, sisi tusio na watu majuu tushajishukuru kikubwa tunamtegemea Mungu kutest bahati,, Sasa babdo yanatokea mauzauza kama haya
 
We kijana wa wapi....
Hongera kwa kujaribu.

Vijana wa siku hizi hawaombi kazi wanatafuta connection tu
Sawa bhana,, nyie si ndo wenye connection.., hebu si tuendelee kutoa machozi ya samaki tu
 
Tuwasubiri mpaka Wastaafu wastaafu ndio Tuajiriwe!
 
Mkuu,utumishi wamekuandama sana..nin tatizo?

Niliona unalalamika kukatwa kuanzia majina ya TRA, brella na leo tena unalalamika.

Ebu fanya kucertify vyeti kama wanavyotaka wahusika.

Haiwezekan wewe tu ndio wawe wanakuonea kila siku, kama ni umaskini majority yetu sisi Watanzania ni maskini lakini mbona wengine tunaitwa kushiriki huo usahili.

Zingatia masharti yao waliyoweka, acha kulalamika.
 
Mkuu hivi katika hali kama hiyo huyo jamaa anaweza kuvitoa hivyo vyeti ambavyo havijawa certified na kuweka vilivyokua certified?.. Maana nilisikia kwenye ajira portal ukishaweka cheti huwezi tena kukitoa
 
achana na habari za kusikia.
 
Hii nchi ni ngumu sana wadau,, ety hapo mtu kashaliwa kichwa Hali ya kuwa alishawahi kuitwa Interview 2 na akafanya..

Alafu hawataki hata kupitia tena majina maana wengine walipeleka kwa Hakimu Ila bado wameandikiwa vivyohivyo...

Hii nchi ngumu sana inafikia kipindi mtu unawaza Why umezaliwa nchi yenye watu wabaya namna hii kama hawa wasio na huruma, vyeti unavyo na hata ukifika Interview unakaguliwa Ila bado Unaonekana we ni mlaghai, Sasa hivi kupata kazi ni ngumu na hata kuitwa Usaili ni ngumu pia..!!!?

Nipo Frustrated sana wadau sijui kwanini wamenifanyia unyama namna hii, Just imagine wangeniita usahili hapa wangepungukiwa nini..?
Nauli ya kwenda ni ya kwangu, kula na kalala ni juu yangu, nikateseke na maswali juu yangu Shida kwao Iko wapi sasa..!!
INASIKITISHA SANA

View attachment 2159841
Mkuu unaweza ukawa unalalamika, ila tatizo hapa ni wewe! Kama tangazo la kazi lilisema cheti kiwe certified, wewe ukapuuza ukapeleka bila ku certify, unategemea nini? Elewa kwamba baadhi ya hivi vigezo vinawekwa ili kuwatoa watu wazembe wazembe maana applicant ni wengi na nafasi ni chache.

Hapo utakuta kwenye CV umejinadi kwamba wewe ni mtu makini, mwenye kufuata maelekezo nk lakini kitu kidogo tu kinaku disqualify.
 
Back
Top Bottom