Hii nchi ni yetu sote. Bunge liyavunje maridhiano, DP World wasipewe banadari. Tutafute pesa na kuwekeza wenyewe

Hii nchi ni yetu sote. Bunge liyavunje maridhiano, DP World wasipewe banadari. Tutafute pesa na kuwekeza wenyewe

Mkuu Mkoloni wa Kiingereza alituachia Nchii ikiwa intact ikiwa na viwanda nk.

Tumeshindwa.
Viwanda vipi alivyotuachia mkoloni? Nenda wewe kajiuze na familia yako kama unapenda kutawaliwa
 
Haijaamua tu kufanya.
JPM ametuonyesha inawezekana, kabla hakuna aliyethubutu kusema inawezekana, amekufa tunarudishwa kwenye yale yale mawazo mfu na ya unyonge...Wanyonge wasituhamishie unyonge wao, sisi tunaweza kama wao hawawezi waachie ngazi
 
Kwa vifaa hivyo vilivyopo wakipewa watu walio serious bandari inajiendesha na kununua mitambo mingine ya kisasa bila kuomba pesa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwani ni lazima kuboresha bandari yetu kwa kutumia Dp World?

Kwani sisi hatuwezi kuwapa kandarasi wachina na kuboresha hayo maeneo muhimu na kuweza kuongeza ufanisi?

Bora kukopa China na kuwekeza hizo cranes kuliko kuuza Bandari ya Watanganyika. Kila kona ni kilio tu na hamuaminiki.
Bunge aliwezi kurekebisha itakuwa kuvunja maridhiano. Kinachoweza kufanyika "Makubaliano" hayo kutokuwa "Mkataba" Rais asiposaini hadi upande wa pili ukubali marekebisho, yarejeshwe tena Bunge kwa kuridhiwa. Lakini, kwa hali ya sasa tayari Bunge limeridhia na kumwachia Rais maamuzi.
 
Viwanda vipi alivyotuachia mkoloni? Nenda wewe kajiuze na familia yako kama unapenda kutawaliwa
Viwanda tulivyovitaifisha Reli Mashamba makubwa ya Mkonge nk.

Au umeshasahau mara hii.
 
Viwanda tulivyovitaifisha Reli Mashamba makubwa ya Mkonge nk.

Au umeshasahau mara hii.
Alivijenga mkoloni? Ulizaliwa lini wewe? Acha kujidharau...Kwa taarifa yako hivyo viwanda vilijengwa na Hayati Rais wa kwanza mwl JK Nyerere...Punguza kujiuza kwa weupe
 
HIVI kweli hatuwezi KUJIENDESHA WENYEWE, KAMA NI MITAMBO tuinunue HATA KAMA NI ya ghali basi MTAMBO MMOJA MMOJA kila MWAKA. Mbona Reli sgr tunajenga. Kama ni ujuzi Kama TEHEMA , tuwalipe watufundishe.kama Ni wizi HIVI kweli TAIFA la tanzania watanzania zaidi ya mil 60 wote wezi. Hao tunawaleta je Ni MALAIKA toka juu mbinguni????. HIVI tunadiliki kusema TUMESHINDWA aje fulani AENDESHE sisi TUKO tumeangalia tu. VYUO VIKUU MIAKA NENDA RUDI VINATOA WAHITIMU FANI MBALIMBALI. HAO WOTE WAPO TU.
 
Alivijenga mkoloni? Ulizaliwa lini wewe? Acha kujidharau...Kwa taarifa yako hivyo viwanda vilijengwa na Hayati Rais wa kwanza mwl JK Nyerere...Punguza kujiuza kwa weupe
Vingi vilitaifishwa kutoka kwa Wakoloni ni Kiwanda kimoja tu ndio tulijengewa bure na Wachina "Urafiki".

Kuhusu "weupe" Yesu mweupe Muhammad mweupe hiyo simu unayotumia imevumbuliwa na weupe Dini uliyonayo ya weupe nguo ulizovaa ni mitumba ya weupe.
Upo hapo?
 
Kwani ni lazima kuboresha bandari yetu kwa kutumia Dp World?
Yes, DPW wana uwezo, ability, capacity, capability.
Kwani sisi hatuwezi
Sisi hatuwezi na sio Bandari tuu, kuna vitu vingi tumeshindwa Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
kuwapa kandarasi wachina na kuboresha hayo maeneo muhimu na kuweza kuongeza ufanisi?
Hili limefanyika na likamgharimu Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu: Sioni sababu ya kujiuzulu
Bora kukopa China na kuwekeza hizo cranes kuliko kuuza Bandari ya Watanganyika. Kila kona ni kilio tu na hamuaminiki.
Kwanini tukope wakati DP World wanazo?.
P
 
Kwani ni lazima kuboresha bandari yetu kwa kutumia Dp World?

Kwani sisi hatuwezi kuwapa kandarasi wachina na kuboresha hayo maeneo muhimu na kuweza kuongeza ufanisi?

Bora kukopa China na kuwekeza hizo cranes kuliko kuuza Bandari ya Watanganyika. Kila kona ni kilio tu na hamuaminiki.
Hakune mbunge atarudi Bungeni ukiacha Mpina na yule Mama wa Mpanda
 
Vingi vilitaifishwa kutoka kwa Wakoloni ni Kiwanda kimoja tu ndio tulijengewa bure na Wachina "Urafiki".

Kuhusu "weupe" Yesu mweupe Muhammad mweupe hiyo simu unayotumia imevumbuliwa na weupe Dini uliyonayo ya weupe nguo ulizovaa ni mitumba ya weupe.
Upo hapo?
Hongera kwakua mtumwa wa weupe, mimi siyo sijawahi wala sintowahi kuwa...Na kwa habari ya viwanda upo mtupu, kuweza kupata majibu tumia hata google itakusaidia...Alamsiki!
 
Back
Top Bottom