Kwa maisha haya ya kibongo, mtu unaishije bila kupiga? Chukulia mfano wa mlinzi ambae ameajiriwa na kampuni ya ulinzi, awe analipwa mshahara kwa mwezi sh 300,000. Hapo akatwe kodi, na nssf, itakayobaki, atumie kwenye
1. Kodi ya nyumba ya kuishi
2. Chakula cha familia
3. Mavazi ya familia nzima
4. Umeme
5. Maji
6. Matibabu/bima ya afya
7. Ada za shule za watoto
8. Sare za shule za watoto
9. Madaftari na mahitaji mengine ya watoto
10. Mchango wa ulinzi shirikishi
11. Michango ya sherehe na misiba
12. Ulabu
13. Michepuko
14. Malezi ya mtoto/watoto wa kusingiziwa
15. Kubeti
16. Garama za waganga wa kienyeji kwaajili ya kulinda ajira na kupandishwa vyeo.
17. Michango ya kwenye nyumba za ibada.
Na mengineyo mengi. Hapo bado nae anataka anunue kiwanja, ajenge nyumba ya kuishi, waachane na nyumba za kupanga.
Hayo yote afanye kwa mshahara wa sh 300,000? utatoshaje? inabidi apige tu! Hakuna jinsi.
Kwa kifupi, umaskini ndio chanzo cha matatizo yetu yote. Hata viongozi wetu ni umaskini tu unawasumbua, hakuna kingine.
Taifa maskini kama la kwetu, lazma upigaji uwepo sana.